Posts

Showing posts from June, 2023

DKT. MSONDE ASISITIZA WALIMU KUPEWA HUDUMA BORA

Image
Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Charles Msonde akihimiza uwajibikaji kwa Menejimenti ya Halmashauri ya Mji wa Nzega katika kikao kazi chake cha kuhimiza uwajibikaji na kufanya tathmini ya ziara yake ya kukagua ujenzi wa miradi ya miundombinu ya elimu kwenye Halmashauri hiyo. Baadhi ya watendaji wanaounda Menejimenti ya Halmashauri ya Mji wa Nzega wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde wakati wa kikao kazi chake cha kuhimiza uwajibikaji na kufanya tathmini ya ziara ya kukagua ujenzi wa miradi ya miundombinu ya elimu kwenye Halmashauri hiyo. Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Charles Msonde akikagua moja ya miundombinu ya elimu inayojengwa katika Halmashuri ya Wilaya ya Uyui akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani humo.  

RC CHALAMILA ATOA WIKI MOJA KWA WAFANYABIASHARA MWENGE WALIOTELEKEZA VIBANDA KURUDI MARA MOJA.

Image
Ni kufuatia wafanyabiashara hao kuondoka eneo walilopangwa na kuhamishia biashara Barabarani.  Amuelekeza Mkandarasi anaejenga Majengo ya kituo Cha Afya Kinondoni kuzingatia ubora. Apongeza Halmashauri ya Kinondoni kwa kubuni mradi wa Stendi ya Mwenge na Uwanja wa Mpira. Ampongeza Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kutoa bilioni 1.5 kwaajili ya Maboresho ya Elimu program ya Boost. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe, Albert Chalamila ametoa muda wa wiki Moja kwa Wafanyabiashara wa Soko la Mwenge Coca cola walioacha vibanda vyao na kurudi kupanga biashara Barabarani kurudi kwenye eneo walilopangwa mara Moja. RC Chalamila ametoa maelekezo hayo wakati wa Ziara ya kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo Wilaya ya Kinondoni Akikagua mradi wa ujenzi wa Kituo Cha Mabasi Mwenge RC Chalamila amepokea malalamiko ya Wafanyabiashara waliosema kitendo Cha wafanyabiashara kupanga bidhaa chini imepekea kukosekana kwa wateja na kusababisha mitaji ya biashara kufa. Kutokana na Hilo RC Chalamila a

JAMII IENDELEE KUJIANDAA KUJIKINGA NA MAAFA- DKT YONAZI

Image
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizindua Jukwaa Shirikishi la Mawasiliano ya Kidijitali la Afya Moja na  namba ya dharura ya kupokea  taarifa za maafa Juni 30, 2023 Jijini Dodoma. Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa  Jukwaa Shirikishi la Mawasiliano ya Kidijitali la Afya Moja na  namba ya dharura ya kupokea  taarifa za maafa Juni 30, 2023 Jijini Dodoma. Washiriki wa Hafla ya  Uzinduzi wa Jukwaa  Shirikishi la Mawasiliano ya Kidijitali la Afya Moja na  namba ya dharura ya kupokea  taarifa za maafa wakiafuatilia matukio mbalimbali katika uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri  Mkuu  Juni 30, 2023 Jijini Dodoma. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda akifafanua jambo wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Jukwaa  Shirikishi la Mawasiliano ya Kidijitali la Afya Moja na  namba ya dharura ya kupokea  taarifa za maafa wakiaf

WIZARA YA UTAMADUINI, SANAA NA MICHEZO YATIA FORA MAONESHO YA SABASABA JIJINI DAR ES SALAAM

Image
 Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akirusha mpira wa kikapu kwenye goli la mchezo huo Juni 30, 2023 kwenye banda la Wizara hiyo Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 47 (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akiwa kwenye kwenye banda la Wizara hiyo Juni 30, 2023 katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 47 (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

WANAOPINGA UWEKEZAJI WA DP WORLD KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM NI MAADUI WA MAENDELEO NCHINI

Image
    Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Comred Rajabu Abdurhaman akizungumza  wakati wa dua maalumu iliyofanywa na waumini dini ya Kiislamu katika Taasisi ya Tamta kwa ajili ya kumuombea Rais Dkt Samia Suluhu iliyodhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Comred Rajabu Abdurhaman akizungumza  wakati wa dua maalumu iliyofanywa na waumini dini ya Kiislamu katika Taasisi ya Tamta kwa ajili ya kumuombea Rais Dkt Samia Suluhu iliyodhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba. MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza wakati wa dua hiyo maalumu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba katika akiwa kwenye dua hiyo wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman Waumini wa dini ya Kiislamu katika Taasisi ya Tamta wakimsikiliza Mwenmyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman mara baada ya kumalizika Dua Maalumu ya Kumuombea Rais Dkt Samia Suluhu Na Oscar Assenga, TANGA CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga kimesema k

TAKUKURU TANGA YAWAPANDISHA KIZIMBANI WATUHUMIWA WA MAKOSA YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI

Image
Na Oscar Assenga,TANGA. TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Tanga imewapandisha kizimbani watuhumiwa wane(8)kwa makosa ya rushwa na uhujumu uchumi na kuisababisha Serikali matumizi batili ya zaidi ya shilingi milioni 28. Waliopandishwa kizimbani ni William Nguluko Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Mabokweni jijini Tanga ambaye anakabiliwa na ashitaka la ubadhirifu na ufujaji kinyume na kifungu cha 28(1)(2) sharia na kuzuia na kupambana na rushwa sura ya 329 marejeo ya mweka 2022. Kosa jingine ni kula njama , kutenda makossa ya rushwa kinyume na kifungu na kifungu 32 sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa , kuisababishia hasara serikali kinyume na aya ya 10(1) ya jedwali la kwanza na kifungu cha 57(1) na 60(2) sharia ya uhujumu uchumi sura ya 200 marejeo ya mwaka 2002. Mshitakiwa wa pili ni Sudi Mshamu, mwalimu wa fedha katika shule hiyo , ambaye yeye anakabilwa na na makosa 31 likiwemo kosa la kughushi kinyume na kifungu cha 333,335(111) na 338,340(2)A sharia ya kanuni

PSSSF YAVIPATIA VIFAA TIBA VITUO SITA VYA AFYA, BARA NA VISIWANI

Image
NA K-VIS BLOG, BUTIAMA MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetoa msaada wa vifaa tiba kwa vituo sita vya afya ikiwa ni kuunga mkono juhudi kubwa wanazofanya watumishi wa umma katika kuwahudumia wananchi kwenye maeneo tofauti ikiwemo eneo la utoaji huduma za afya. Vituo vilivyonufaika na msaada huo ni pamoja na kituo cha Afya Kirumi kilichoko Wilaya ya Butiama Mkoani Mara ambacho kimekabidhiwa Ijumaa, Juni 30, 2023 na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF CPA. Hosea Kashimba. Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo, CPA. Kashimba alisema vituo vingine vitano vikiwemo Mkunguni na Dimbani vilivyoko Kizimkazi, Zanzibar, Ikombe, Mtwara, Mji, Lindi na Ilembo Mkoani Katavi, vilikabidhiwa vifaa kama hivyo wakati wa Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofikia kilele chake  Juni 23, 2023. “Hapa tuko mahala pake, nyote ni watumishi wa Umma mko hapa kuihudumia jamii ya wana Kirumi tunaamini vifaa hivi tulivyokabidhi vitasaidia kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa we

MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MAMA MARIAM MWINYI AHUDHURIA MKUTANO WA "CHINA-AFRICAN WOMEN FORUM"

Image
MKE wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama  Mariam Mwinyi akihutubia katika mkutano wa “China –Afrika Women Forum” uliohudhuriwa na baadhi ya Wake Marais wa Afrika na Viongozi wa Wanawake wa China na Afrika, uliofanyika katika ukumbi wa Xiangjiang Jimbo la Hunan China.(Picha na Ikulu) MKE wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama  Mariam Mwinyi akihutubia katika mkutano wa “China –Afrika Women Forum” uliohudhuriwa na baadhi ya Wake Marais wa Afrika na Viongozi wa Wanawake wa China na Afrika, uliofanyika katika ukumbi wa Xiangjiang Jimbo la Hunan China.(Picha na Ikulu) WASHIRIKI wa Mkutano wa Uhushirikiano Kati ya China na Afrika “China-Afrika Woman Forum” wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar ma Mama Mariam Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika katika ukumbi wa mkutano wa Xiangjiang Jimbo la Hunan China. WASHIRIKI wa Mkutano wa Uhushirikiano Kati ya China na Afrika “China-Afrika Woman Forum” waki

TAARIFA YA KUPOTEA MTOTO HANS SAMWEL KUZIGANIKA

Image
  TAARIFA YA KUPOTEA MTOTO. JINA HANS SAMWEL KUZIGANIKA, ANASOMA DARASA LA II SHULE YA MSINGI MWEMBENI -MALINYI MKOA WA MOROGORO, AMEPOTEA AKIWA MAKULU DODOMA, YEYOTE ATAKAEMUONA AWASILIANE NA WAZAZI WALE KWA SIMU 0786340691/ 0683060965, AU KUTOA TAARIFA KITUO CHOCHOTE CHA POLISI.

GAVANA TUTUBA: SHILINGI YA TANZANIA IMEENDELEA KUIMARIKA

Image
NA HUGHES DUGILO, DAR ES SALAAM. GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Emmanuel Tutuba ameseSma hilingi ya Tanzania kwa muda mrefu imeendelea kuwa imara ikilinganishwa na sarafu nyingine kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.   Gavana Tutuba ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari alipofanya ziara ya kutembela Banda la BoT katika Maonesho ya Biashara ya 47 ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.  Amesema tathimini imeonyesha kuwa katika kipindi cha miaka kumi iliyopita Shilingi ya Tanzania imeshuka thamani kwa asilimia 1.4 tu, ambapo ni sarafu chache sana Ulimwenguni zenye uhimilivu kama ilivyo sarafu ya Tanzania.  “Kinachofanya Shilingi yetu kuwa himilivu ni sababu ya vyanzo vya shughuli za uzalishaji, unajua uhimilivu wa shilingi unategemea na aina ya biashara na huduma ambazo zinaenda kufanya mzunguko wa fedha.  “Kwa muda mrefu thamani ya Shilingi yetu imeendelea kuw

RAIS DKT. MWINYI AMEZIKARIBISHA KAMPUNI ZAIDI ZA CHINA KUWEKEZA TANZANIA NA AFRIKA KWA UJUMLA

Image
Changsha,  Hunan China Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi amezikaribisha kampuni nyingi za China kuwekeza Tanzania na Bara la Afrika kwa ujumla, kwani kuna ardhi ya kutosha, nguvu kazi nyingi na Afrika ina uthubutu wa kufanya biashara. Dkt. Mwinyi aliyasema hayo  wakati wa sherehe za ufunguzi wa mkutano wa tatu wa ushirikiano wa Biashara kati ya China na Afrika, uliofanyika katika jiji la Changsha jimbo la Hunan China. Dkt. Mwinyi alisifu ushirikiano baina ya China na Tanzania ambao sasa umetimiza miaka 60 na akaonesha matumaini yake ushirikiano huo utazidi kukua na kuimarika. Amesema katika miaka miwili iliyopia Afrika imeshuhudia ushirikiano mkubwa na China ambapo biashara imeongezeka kwa zaidi ya dola bilioni 74. Amefurahi kuona wawekezaji wakubwa wa China wamehudhuria mkutano huo na akabainisha hiyo ni fursa kwa Afrika kujitutumua zaidi na kukaribisha wawekezaji hao barani humo. Mapema akifungua mkutano huo kwa niaba ya Afrika Rais wa