Posts

Showing posts from January, 2022

RC Kunenge: Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji

Image
  Bagamoyo.   Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amesema Serikali inaendelea kujenga na kuboresha mazingira bora ya wawekezaji ili waweze kuzalisha bidhaa zenye ubora na zitakazoweza kushindani katika masoko ya ndani na nje ya nchi. Kunenge amesema hayo leo Jumamosi Januari 29, 2022 akijibu changamoto zilizowasilishwa na baadhi ya wawekezaji wa viwanda wilayani Bagamoyo katika ziara yake ya kutembelea na kukagua shughuli zinazoendeshwa katika viwandani hivyo. "Niwahakikishie wawekezaji endeleeni kuwekeza, umeme wa kutosha upo , na nasema  hivi kwa sababu  Rais wetu Samia Suluhu ametuahidi kuziondoa na ameanza kwa mradi huu wa Nyerere Hydropower Project  huko Rufiji ambao umeme wake utazalishwa hapo na utatumika ukitokea hapa Chalinze inapojengwa mradi huo” amesema Kunenge Kuhusu maji, mkuu huyo wa mkoa ameeleza Serikali imesaini mkataba na mkandarasi anafanya upembuzi yakinifu kutoa maji kutoka bwawa la mto Rufiji utakao zalisha lita milioni 250 kwa siku yatakayotumika Pwani

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATATU JANUARI 31, 2022

Image
 

NAIBU WAZIRI MARY MASANJA AZINDUA MAFUNZO KWA WATOA HUDUMA ZA UTALII NCHINI

Image
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amezindua rasmi Mafunzo kwa Watoa Huduma za Utalii nchini kuhusu Mwongozo wa kukabiliana na janga la UVIKO-19 katika Sekta ya Utalii kwenye ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii Kampasi ya Bustani jijini Dar es Salaam leo. Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Masanja amesema mafunzo hayo yatawajengea uwezo watoa huduma za utalii kuhusu  namna ya kukabiliana na UVIKO 19. “Mafunzo haya yatawajengea uwezo watoa huduma za utalii nchini juu ya namna bora ya kukabiliana na janga la UVIKO-19 kwa kuzingatia matakwa ya kiafya na usalama pamoja na kuboresha huduma wanazotoa na hatimaye kimarisha ushindani wa nchi katika masoko mbalimbali ikiwemo kuvutia watalii wa kimataifa kuja nchini hasa katika kipindi hiki cha mtazamo mpya wa utoaji huduma za utalii na usafiri kukabiliana na UVIKO-19 yaani " _the new normal of tourism and travel_ ” amesisitiza Mhe.Masanja. Amemshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanz

BENKI YA AfDB YAMTAKA MKANDARASI WA MRADI WA UMEME TANZANIA – KENYA KUONGEZA KASI

Image
Na. Peter Haule, WFM, Arusha Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imemtaka Mkandarasi wa Ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Singida - Arusha hadi Isinya nchini Kenya unaogharimu dola za Marekani milioni 258 zilizotolewa kwa mkopo na Benki hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) na Serikali ya Tanzania, kuharakisha utekelezaji wa mradi huo ili ifikapo mwezi Desemba mwaka huu uweze kukamilika. Rai hiyo imetolewa jijini Arusha na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anaesimamia nchi tisa  za  A frika  ikiwemo   Tanzania, Kenya, Ethiopia, Rwanda, Seychelles, Sudan Kusini, Eritrea Uganda  na Somalia katika Benki hiyo, Bw. Amos  Cheptoo , wakati alipotembelea na kukagua Mradi wa Kituo cha Umeme cha Lemugur, mkoani Arusha, ambacho ni sehemu ya mradi mkubwa wa umeme wa Singida- Arusha hadi Isanya Kenya. Bw. Cheptoo ambaye yuko nchini kwa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi iliyopata fedha za mkopo nafuu kutoka Benki hiyo upande wa Zanzibar na Tanzania Bara, alisema n

WAZIRI MASAUNI KUKUTANA NA VIONGOZI WA JESHI LA POLISI

Image
Na WMNN, Dar es Salaam. KUTOKANA na mauaji ya kijamii yanayoendelea nchini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amepanga kukutana na Watendaji Wakuu wa Jeshi la Polisi ili kupokea taarifa ya matukio pamoja na kujadili jinsi ya kudhibiti mauaji hayo. Waziri Masauni amesema katika kikao hicho pia kitajadili jinsi ya kulifanya Jeshi la Polisi kuwa la kisasa katika kudhibiti matukio mbalimbali kiuhalifu nchini.  Akizungumza katika ziara yake ya siku moja ya kutembelea Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi (Forensic Bureua), jijini Dar es Salaam, leo, Masauni amesema lengo kuu la kukutana na viongozi hao siku ya Jumatatu Januari 31, 2022, ni kupata taarifa ya uchunguzi wa mauaji ambayo waliushaanza na kujua jinsi gani matukio hayo yanaweza kumalizwa katika jamii. “Siku ya Jumatatu nitakua na kikao na Viongozi wa Jeshi la Polisi wakiongozwa na IGP pale Wizarani kwa ajili ya kupitia matokeo ya kazi ya uchunguzi ambayo wanaifanya na Serikali tunategemea waifanye ili tuweze k

RAIS SAMIA AFANYA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MOJA NCHINI MSUMBIJI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisindikizwa na Mwenyeji wake Rais Philipe Nyusi wa Msumbiji alipokua akiondoka katika Uwanja wa ndege wa Pemba nchini Msumbiji baada ya kukamilisha ziara  yake ya kikazi ya siku moja Nchini humo leo tarehe 28 Januari 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais Philipe Nyusi wa Msumbiji alipowasili katika uwanja wa ndege wa Pemba nchini Msumbiji kwa ajili ya ziara  ya kikazi ya siku moja Nchini humo leo tarehe 28 Januari 2022 Nchini humo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Mwenyeji wake Rais Philipe Nyusi wa Msumbiji alipowasili  katika uwanja wa ndege wa Pemba nchini Msumbiji kwa ajili ya ziara  ya kikazi ya siku moja Nchini humo leo tarehe 28 Januari 2022 Nchini humo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Kikundi cha ngoma ya asili ya Msumbiji alipowasili  katika uwanja wa ndege wa Pemba nchin

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAMOSI JANUARI 29, 2022

Image