WAZIRI KAIRUKI AKAGUA UJENZI WA MRADI WA NYUMBA MSOMERA
Asisitiza Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu inalenga kuboresha maisha ya wananchi Na Happiness Shayo Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amekagua mradi wa ujenzi wa nyumba katika kijiji cha Msomera Wilayani Handeni kwa ajili ya wananchi wanaohama kwa hiari kutoka Ngorongoro kwenda Msomera, ikiwa ni awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba hizo. Mhe. Kairuki amefanya ziara hiyo leo Desemba 31,2023 kwa lengo la kuangalia maendeleo ya ujenzi wa nyumba hizo ambapo zoezi la kuwahamishia wananchi Msomera linaendelea. Katika kijiji cha Msomera wilayani Handeni Mkoani Tanga Serikali inajenga nyumba 2500 huku nyumba nyingine 1500 zikitarajiwa kujengwa katika kijiji cha Kitwai B wilayani Simanjiro na nyumba 1000 zitajengwa katika kijiji cha Saunyi wilayani Kilindi na kufanya jumla ya nyumba 5000 kwa mradi wote. “Tulishaendesha zoezi katika awamu ya kwanza kwa ajili ya kuhamisha wananchi kutoka katika eneo la hifadhi ya ngorongoro,tumemaliza vizuri na zaidi ya nyumba 500 ziliweza