Posts

Showing posts from August, 2023

PSSSF KUWEKEZA ZAIDI KWENYE TEHAMA, RASILIMALI WATU ILI KUONEGZA UBORA WA UTOAJI HUDUMA

Image
  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DAR ES SALAAM KATIKA kuhakikisha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) unaendelea kutoa huduma bora kwa wanachama wake, sasa unaelekeza nguvu zake katika matumizi ya TEHAMA na kuendeleza rasilimali watu ili kuongeza ubunifu na ufanisi, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba, amesema. CPA. Kashimba ameyasema hayo kwenye kikao kazi baina ya Mfuko, Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR) na Wahariri wa vyombo vya habari, wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko tangu kuanzishwa kwake Agosti, 2018 hadi Agosti, 2023, kwenye Makao Makuu ndogo ya PSSSF, jengo la Golden Jubilee Tower, jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2023, “Kama kuna namna ya kuufanya Mfuko uwe wa kisasa zaidi basi hayo ndiyo matamanio yetu na tumeanza, lengo ni kuifanya taasisi iwe rafiki zaidi kwa wanachama wake na yenye miundombinu ya kutoa huduma bora zaidi bila ya usumbufu wowote.” Alisema. Alisema kwa sasa Mfuko unatumia TEHAMA kwa zaidi ya

RAIS SAMIA KATIKA TAMASHA LA KIZUMKAZI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Acison, wakati akiwasili kwenye viwanja vya Paje kwa ajili ya kuhudhuria Tamasha la Kizimkazi (Usiku wa Samia) Paje, Zanzibar tarehe 30 Agosti, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia vikundi mbalimbali vya Sanaa vikitumbuiza kwenye Tamasha la Kizimkazi (Usiku wa Samia) katika viwanja vya Paje Zanzibar tarehe 30 Agosti, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekea Jukwaa Kuu kwa ajili ya kuhudhuria Tamasha la Kizimkazi (Usiku wa Samia) Paje Zanzibar tarehe 30 Agosti, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekea Jukwaa Kuu kwa ajili ya kuhudhuria Tamasha la Kizimkazi (Usiku wa Samia) Paje Zanzibar tarehe 30 Agosti, 2023.

KUTOKA MAGAZETINI LEO ALHAMISI AGOSTI 31, 2023

Image