WANACHUO WA CHUO CHA UHASIBU, IAA JIJINI ARUSHA WACHANGAMKIA "BOOM VIBES NA NSSF" KWA KUJIUNGA NA MFUKO
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, ARUSHA KAMPENI ya “BOOM VIBES NA NSSF” yenye lengo la kuhamasisha Wanachuo kuhusu Hifadhi ya Jamii na Uwekaji Akiba imefanyika kwenye Chuo cha Uhasibu jijini Arusha (IAA) leo Mei 31, 2022. Kampeni hiyo ni mkakati wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) chini ya Mpango wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa sekta isiyo rasmi kutembelea taasisi mbalimbali za elimu ya juu na kati nchini ili kuhamasisha wanachuo kujenga tabia ya kujiwekea akiba kwa kujiunga na Mfuko na kuchangia kila mwezi ili hatimaye wanufaike na mpango wenyewe, Meneja wa Sekta Isiyo Rasmi, NSSF Bi. Rehema Chuma amewaambia wanachuo hao wakati akitoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii. Alisema wanachuo ni wanufaika wakubwa wa mpango huo kutokana na kipato wanachokipata wanaweza kutenga ziada na kujiwekea akiba NSSF kwa manufaa ya sasa na baadaye. “Ni muhimu wewe kama mwanachuo kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba kupitia NSSF, ukianza kuweka akiba mapema itakuwezesha kuwa na akiba ya kutosha