Posts

Showing posts from January, 2024

CCM YAWATAKA VIJANA KUJITOKEZA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

Image
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka vijana kujitokeza wa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi huku kikiahidi kuwapa fursa kwa kuwapitisha kwa kuwa wanao uwezo wa kuongoza. Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana katika mkutano mkuu maalumu wa ukaribisho wa wananchama wapya 1,167 wa Seneti ya Vyuo Vikuu wa DIT, CBE, IFM na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kutoka tawi la Kibasila, Kata ya Upanga Mashariki. Kinana alisema Chama kinawategemea vijana kwa kuwa wanayo chachu ya mawazo kwa Chama, hivyo wasifikiri kuwa kuna sehemu nyingine mawazo yatatoka bali watambue kuwa wao ni taifa la leo. Alisema Chama kinawategemea kwa ushauri, kujenga hoja na kukosoa, hivyo watambue wao ni watu wa kisasa, wasomi na wanakwenda na kasi ya upatikanaji wa taarifa hususan kupitia mitandao ya kijamii. "Kutokana na hilo mnao uwezo mkubwa wa kutushauri, kutujenga na kutukosoa, tunakutegemeeni sana, toeni mawazo. mwaka huu tuna uc

AFRIKA TUMIENI VEMA FURSA ZA SOKO LA AFCFTA

Image
  Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) na Mwenyekiti wa Mkutano wa 13 wa Mawaziri wa Biashara wa Eneo Huru la Biashara Afika (AfCFTA) amezisitiza Nchi Wanachama wa Mkataba huo kutumia vema fursa zilizopo ili kukuza biashara. Dkt. Kijaji ameyasema hayo Januari 30, 2024 alipokuwa akifungua Mkutano wa 13 wa Mawaziri wa Biashara AfCFTA unaofanyika Durban, Afrika Kusini, Mkutano huo ambao utafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 30 hadi 31 Januari 2024. Aidha amezitaka Nchi hizo kuendelea kushirikiana katika kukamilisha Itifaki ya Uwekezaji, Itifaki ya Biashara ya Kidigitali, pamoja na majadiliano kwenye Vigezo vya Uasili wa Bidhaa na kukamilisha masuala muhimu yanayohusu mifumo ya utatuzi wa migogoro katika ufanyaji biashara kupitia Mkataba wa Eneo Huru la Biashara. Akifafanua zaidi, Dkt Kijaji amesema ushirikiano wa nchi hizo kupitia AfCFTA utachangia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu ya usafirishaji wa barabara, reli na usafiri wa a

SERIKALI YAWALIPA WAZABUNI TRIL 2.1 KWA MWAKA 2016 HADI 2023

Image
  Na. Khadija Ibrahim, WF, Dodoma Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameliambia Bunge, Mjini Dodoma kuwa katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2016/2017 hadi Desemba 2023, imewalipa wazabuni na wakandarasi wa ndani zaidi ya shilingi trilioni 2.1 kati ya madai ya zaidi ya shilingi trilioni 3.1 yaliyowasilishwa. Dkt. Nchemba amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina, aliyetaka kufahamu kiasi cha fedha ambacho Serikali imewalipa ama kukataa kuwalipa wazabuni na wakandarasi wa ndani baada ya kuwasilisha madai yao na kufanyiwa uhakiki. “Jumla ya madeni ya wazabuni na wakandarasi yaliyowasilishwa kwa uhakiki yalikuwa zaidi ya sh. bilioni 3,110.33, kati ya kiasi hicho madeni yaliyolipwa ni zaidi ya sh. bilioni 2,128.54 ambapo sh. bilioni 1,032.13 ni madeni ya wazabuni na sh. bilioni 1,096.41 ni madeni ya wakandarasi” alisema Dkt. Nchemba Alisema kuwa madeni ya sh. bilioni 981.79 yalikataliwa kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo kukoseka

TANZANIA YAPOKEA MSAADA WA Sh. TRIL 1.4 KUTOKA GLOBAL FUND

Image
  Na Farida Ramadhani, WF, Dodoma Tanzania na Global Fund zimesaini Mikataba minne ya misaada yenye thamani ya dola za Marekani milioni 606.9 (sawa na zaidi ya sh. trilioni 1.4) kwa ajili ya kupambana na maradhi ya UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na Uimarishaji wa mifumo ya afya nchini. Mikataba hiyo imesainiwa Jijini Dodoma kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), na Mkuu wa Global Fund- Afrika, Bw. Linden Morrison. Mhe. Nchemba alisema msaada kutoka Global Fund umepangwa kutekelezwa kwa miaka mitatu ambapo mpaka sasa Tanzania imepokea misaada kwa vipindi vinne ambavyo ni Julai 2012 – Desemba 2014, Julai 2015 – Desemba 2017, Januari 2018 – Desemba 2022 na Januari 2021 -Desemba 2023. “Miradi inayotekelezwa kupitia msaada wa Global Fund kwa kipindi cha kuanzia Januari 2024 hadi Desemba 2026 itatekelezwa na Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Wizara ya Fedha inaendelea kuwa Mpokeaji Mkuu wa Sekta ya Umma na Management and Development for Health (MDH) ni Mpo

KUTOKA MAGAZETINI LEO JANUARI 31, 2024

Image
 

RAIS SAMIA AZINDUA VIZIMBA VYA UFUGAJI WA SAMAKI NA BOTI ZA UVUVI ZIWA VICTORIA

Image
Rais Samia Suluhu Hassan akielekeza jambo kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati akielezea kuhusu Samaki wa aina mbalimbali wanaopatikana katika Ziwa Victoria mara baada ya uzinduzi wa Boti za kisasa pamoja na vizimba vya kufugia Samaki Mwanza 30 Januari, 2024. Rais Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati akielezea kuhusu Samaki wa aina mbalimbali wanaopatikana katika Ziwa Victoria mara baada ya uzinduzi wa boti za kisasa pamoja na vizimba vya kufugia Samaki Jijini Mwanza 30 Januari, 2024. Rais Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati akielezea kuhusu Samaki wa aina mbalimbali wanaopatikana katika Ziwa Victoria mara baada ya uzinduzi wa boti za kisasa pamoja na vizimba vya kufugia Samaki Jijini Mwanza 30 Januari, 2024. Rais Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa vizimba vya kufugia Samaki na Boti za Kisasa kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye h