MHE. JENISTA AWATAKA WATUMISHI WA OFISI YAKE KUTOA USHIRIKIANO WA KIUTENDAJI KWA VIONGOZI WAPYA ILI KUENDELEA KUUBORESHA UTUMISHI WA UMMA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akizungumza na watumishi wa ofisi yake kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wake Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa kwanza kulia) kuzungumza na watumishi hao mara baada ya kuripoti rasmi katika ofisi hizo zilizopo Mtumba jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Juma Mkomi. Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (wa pili kutoka kushoto) akipokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake kutoka kwa mtangulizi wake, Dkt. Laurean Ndumbaro (wa kwanza kulia) mara baada ya Bw. Mkomi kuripoti rasmi katika ofisi hiyo iliyopo Mtumba jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete. Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma aliyemaliza