9/30/2021

AFISA MTENDAJI MKUU NFRA AWEKA WAZI UTEKELEZAJI MRADI WA KUONGEZA UWEZO WA UHIFADHI NAFAKA KATIKA MAENEO NANE


Saymon Kobilesky Mhandisi Mjenzi wa Maghala ya Kuhifadhia Chakula mjini Sumbawanga kutoka Kampuni ya Unia Araj Poland akitoa Maelezo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bw. Bw. Milton Lupa wakati alipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa maghala ya kuhifadhia chakula mjini Mpanda mkoani Katavi  hivi karibuni. Kushoto ni Marwa Range Kaimu Meneja wa NFRA Kanda ya Sumbawanga.

Proches Kiwango Fundi Sanifu wa Mradi wa Maghala ya NFRA Mpanda akitoa maelezo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bw. Milton Lupa wa pili kutoka kushoto wakati alipokagua mradi huo unaotekelezwa na Kampuni ya Unia Araj Poland hivi karibuni, kushoto ni Marwa Range Kaimu Meneja wa NFRA Kanda ya Sumbawanga na Katikati ni Bw. Hudson Kamoga Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Kilimo

Muonekano wa mradi wa ujenzi wa maghala ya kuhifadhia chakula Mpanda mkoani Katavi.

Proches Kiwango Fundi Sanifu wa Mradi wa Maghala ya NFRA Mpanda akitoa maelezo kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bw. Bw. Milton Lupa wa wakati alipokagua mradi huo unaotekelezwa na Kampuni ya Unia Araj Poland mjini Mpanda mkoani Katavi hivi karibuni.

Agustino Mwadasi Mhandisi Mkazi wa Mradi wa ujenzi wa Maghala ya kuhifadhia ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Vwawa Mbozi mkoani Songwe kutoka TBA akitoa maelezo kwa Bw. Hudson Kamoga Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Kilimo wakati alipotembelea mradi huo na kuona hatua mbalimbali za utekelezaji hivi karibuni kushoto ni Eva Michael Kwavava Kaimu Meneja wa NFRA Songwe.

Proches Kiwango Fundi Sanifu wa Mradi wa Maghala ya NFRA Mpanda akitoa maelezo kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bw. Bw. Milton Lupa katikati wakati alipokagua mradi wa Maghala ya NFRA unaotekelezwa na Kampuni ya Unia Araj Poland mjini Mpanda mkoani Katavi hivi karibuni. kushoto ni Hudson Kamoga Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Kilimo.

...............................................

Na Mwandishi wetu, Mpanda Katavi

AFISA Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Milton Lupaa amesema Wakala huo unatekeleza mradi wa ujenzi wa maghala ili kuongeza uwezo wa hifadhi nafaka katika maeneo nane hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea ujenzi wa miradi hiyo iliyopo mjini Mpanda, Sumbawanga, Songwe, Makambaku, Babati, Dodoma na kujionea shughuli zinazoendelea katika ujenzi wa maghala hayo makubwa, yenye uwezo wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi zaidi ya tani 250,000. Bwana Lupa amesema, lengo ni kuongeza uwezo wa Taasisi na kupunguza adha ya wakulima kubaki na mazao yao nyumbani kwa kukosa soko au mahali pa kuhifadhi mara baada ya kuvuna.

"Gharama za mradi huo ni dola za Marekani milioni 67 ambazo kati yake dola milioni 55 ni mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Poland na dola milioni 12 ni fedha za ndani kutoka serikali. Ujenzi unatekelezwa na wakandarasi wawili wote kutoka nchini Poland ambao ni kampuni ya M/S FEERUM S.A ambayo inatekeleza maeneo matano na kampuni ya Unia Sp.zo.o ambayo inatekeleza maeneo matatu. Huku mhandisi mshauru wa mradi ni Wakala wa Ujenzi wa Tanzania(TBA)

"Katika maeneo ambayo wakandarasi hao wanatekeleza mradi zipo faida kwa watanzania kama vile wananchi kupata ajira ambapo wakandarasi wazawa wanaajiriwa kama "Sub Contracors" na shughuli zingine za kiuchumi zinaendelea wakiwemo Mama lishe, Baba Lishe na baadhi ya vibarua ambao wanafanya kazi za kusaidia mafundi pamoja na wataalam wetu kujiongezea ujuzi zaidi katika fani zao za uhandisi,"amesema.

Ameongeza kuwa, mradi huo ukikamilika utaongeza tani laki 250,000 za uhifadhi wa chakula na kufikisha tani laki 501,000 ambapo kwa sasa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ina uwezo wa kuhifadhi tani 251,000.

Pia, uwekezaji huo wa maghala una tija kubwa kwa serikali, wakulima na wananchi kwa sababu ni jukumu la NFRA kununua chakula kwa wakulima na kukihifadhi ili kunapotokea changamoto ya njaa au bei ya mazao kwa wakulima kuwa chini NFRA iyanunuwe na kuhifadhi.

"Kwasababu hawa wakulima wa chini hawana uwezo wa kuhifadhi mazao hayo kitaalam hili linafanyika kwa sababu ya kuwalinda wasitetereke kiuchumi katika shughuli nzima ya kilimo chao. Kuhusu ununuzi wa mahindi, Bwana Lupa amesema NFRA inaendelea kununua mahindi kwa wakulima katika vituo vyake vyote hapa nchini na tayari imenunua zaidi ya tani elfu 40,000 na inanunua mahindi kwa vyama vya ushirika na mtu moja mmoja. "Utaratibu wa kununua umeshawekwa ambapo kila mkulima atauza mahindi kati ya gunia 1 mpaka magunia 300. Serikali inawalenga zaidi wakulima wa kawaida kwa sababu uwezo wao wa kuhifadhi mahindi ni mdogo hivyo ni muhimu kuwalinda ili waweze kuendelea na kilimo chao katika msimu ujao,"amesema.

Amesema, vifaa vyote vinavyohusika katika ununuzi wa mazao hayo vimeshapelekwa katika vituo vyote vya kununulia na kama kutakuwa na changamoto yoyote wakulima wasisite kutoa taarifa zishughulikiwe mara moja ili kutokwamisha zoezi la ununuzi wa mazao hayo.

Amewaomba, wakulima hao kuwa watulivu na kufuata maelekezo na taratibu watakazopewa na maofisa wa NFRA ili waweze kuuza mahindi yao yote kwa utaratibu uliowekwa ambapo pia amewataka kutokuwa na wasiwasi wowote katika zoezi zima la ununuzi wa mahindi yao.

    

BALOZI MASHIBA AWATOA HOFU MADEREVA WA TANZANIA HUKO MALAWI

 Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Benedict Mashiba amewatoa hofu Watanzania kuwa Madereva wa Malori wa Tanzania wapo salama licha ya kulengwa na wenzao wa Malawi.

Kwa mujibu wa Balozi Mashiba, visa vya kushambuliwa kwa Malori yanayoe deshwa na Madereva wa Tanzania nchini Malawi vilianza Jumatatu Septemba 27, 2021 ambapo Madereva wa Malori wa Nchini Malawi waliitisha mgomo wakidai maslahi Bora kutoka kwa waajiri wao.

Taarifa za vyombo vya habari zikinukuu vyanzo mbalimbali kutoka nchini Malawi vilisema, Madereva wa Malawi waliamuru Malori yote ya mizigo kuegeshwa na yasiobekane barabarani Hadi hapo madai yao yatakapopatiwa ufumbuzi. 

Hata hivyo Madereva wa Malori kutoka Tanzania hawakujihusisha na mgomo huo kwasababu hakuwa ukiwahusu na waliendelea na kazi Hali iliyowakasitisha wenzao na hivyo kuyashambulia Malori yao kwa mawe na kuharibu vioo.

 Balozi Mashiba jana Septemba 29, 2021 alikutana na baadhi ya Madereva wa Tanzania na kushauriana nao kuhusu namna Bora ya kuepuka mashambulizi hayo.

Aidha Polisi nchini Malawi wametoa idhini Madereva wa Tanzania waendelee na safari zao. 

" Sisi Ubalozini tunafuatilia hatua zinazochukuliwa na serikali kuhakikisha usalama wa watu wetu kupitia Wizara yao ya Mambo ya Nje." Alisema Balozi Mashiba.

Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Benedict Mashiba (katikati mwenye suti) akiwa katika picha na baadhi ya Madereva wa Tanzania waliokumbwa na msukosuko huko Malawi.

    

9/29/2021

BENKI YA DUNIA YAJA NA NEEMA KWA TANZANIA

 Na. Farida Ramadhan na Josephine Majura WFM- DODOMA

Benki ya Dunia imeahidi kuisaidia Tanzania kukabiliana na athari za kiuchumi zilizosababishwa na ugonjwa wa UVIKO – 19 pamoja na kusaidia kutekeleza miradi itakayosaidia kukuza ajira kwa vijana, kuboresha miundombinu ya afya na elimu pamoja na kuendeleza rasilimali watu.
Ahadi hiyo imetolewa Jijini Dodoma na Makamu wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Hafez Ghanem alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.
Aliyataja maeneo muhimu yatakayosaidia kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira hususan kwa vijana kuwa ni pamoja na kuwekeza katika mifumo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA), kuimarisha sekta ya nishati ya umeme, kuboresha miundombinu ya usafirishaji na kuimarisha sekta binafsi ili iweze kuchangia katika kutoa ajira na kukuza uchumi wa nchi.
“Tumejadiliana mambo mengi lakini suala la muhimu ni kuhakikisha sekta binafsi inawekewa mazingira mazuri ya kuwekeza katika miradi itakayochochea ukuaji wa uchumi ikiwemo nishati, kukuza ajira, pamoja na kuwekeza kwenye maeneo yatakayosaidia kuboresha afya ya mama na mtoto pamoja na suala zima la elimu” alisema Dkt. Ghanem.
Ili kutimiza azma hiyo, Dkt. Ghanem aliishauri Serikali kuangalia namna ya kuboresha sera na sheria zitakazochochea wawekezaji wengi wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza mitaji na technolojia vitakavyochochea mapinduzi ya viwanda kupitia mfumo wa ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP).
Aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kusimamia vizuri masuala ya uchumi licha ya kuwepo kwa changamoto ya ugonjwa wa UVIKO -19 ikilinganishwa na nchi nyingine ambapo kiwango cha ukuaji wa uchumi wa Tanzania kimefikia wastani wa asilimia 4.6.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, aliishukuru benki hiyo kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miradi mitano iliyosainiwa hivi karibuni inayogharimu zaidi ya shilingi trilioni 1.3.
Dkt. Nchemba alisema hadi sasa benki hiyo imewekeza zaidi ya dola bilioni 5.5 kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo na kuishuru benki hiyo kwa ahadi ya kuendeleza ushirikiano katika kuendeleza miradi mingine mipya ya kimkakati ikiwemo kuboresha Jiji la Dar es Salaam pamoja na Miji mingine 45 nchini.
“Leo tumeongelea maeneo mengine mawili ya Mkakati wa Maendeleo ambapo tumekubaliana kuweka nguvu kubwa katika kukuza Sekta Binafsi inayolenga kutengeneza ajira nyingi kwa vijana na mpango wa kuwawezesha wanafunzi wengi kupata elimu bila kuacha masomo” alisema Dkt. Nchemba.
Aliihakikisha Benki ya Dunia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Benki hiyo katika masuala mbalimbali ili kuhakikisha maendeleo yanapatikana katika nchi kwa haraka zaidi.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia (WB), Dkt. Hafez Ghanem, yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku 4 ambapo anatarajia kukutana na viongozi mbalimbali wa nchi ili kujadiliana kuhusu masuala ya ushirikiano kati ya Benki hiyo na Tanzania, changamoto zinazoikabili Tanzania na fursa zilizopo ndani ya Benki hiyo.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem (katikati) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Mhe. Mara Warwick, wakiteta jambo baada ya mkutano wao uliofanyika jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto) akiishukuru Benki ya Dunia (WB) kwa kutoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya Maendeleo, wakati wa kikao na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem (wa kwanza kulia), jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akieleza kuhusu suala la ajira kwa vijana wakati wa mkutano na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem (hayupo pichani), jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia (WB) Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem, akieleza nia ya WB kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kupambana na umasikini wakati wa mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem (katikati) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Mhe. Mara Warwick, wakiteta jambo baada ya mkutano wao uliofanyika jijini Dodoma.
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bi. Mara Warwick, akifafanua jambo wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem (kushoto), jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem (katikati) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bi. Mara Warwick, wakiteta jambo baada ya kumalizika kwa mkutano wao uliofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa tatu kulia), Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem (katikati) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bi. Mara Warwick (wa tatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe kutoka Benki ya Dunia na Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akimwongoza mgeni wake, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem kuelekea chumba chake cha mikutano, wakati Makamu huyo wa Rais wa Benki ya Dunia alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo Jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem akiteta jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao Jijini Dodoma.(Picha na WFM, Dodoma