Posts

Showing posts from December, 2022

RAIS DKT. SAMIA AKUTANA NA FREEMAN MBOWE IKULU, DAR ES SALAAM

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndugu. Abdulrahman Kinana wakati akipokea taarifa ya Maendeleo ya mazungumzo ya mchakato wa maridhiano ya kisiasa, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Desemba 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu. Abdulrahman Kinana  mara baada ya kupokea taarifa ya Maendeleo ya mazungumzo ya mchakato wa maridhiano ya kisiasa, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Desemba 2022.

RAIS SAMIA AMLILIA PAPA MSTAAFU BENEDICT XVI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na taarifa za kifo cha Baba Mtakatifu Mstaafu Benedict XVI. Katika salamu sale fupu alizozitoa kupitia mitandao ya kijamii, Dkt. Samia ameandika, "Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Baba Mtakatifu Mstaafu Benedict XVI, ambaye alijitoa maisha yake kutumikia wengine. Natuma salamu za pole kwa Baba Mtakatifu Francisko, waumini wa Kanisa Katoliki Tanzania na Duniani kote. Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi. Amina."

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAMOSI DESEMBA 31, 2022

Image
 

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN MWINYI AHUTUBIA MAADHIMISHO SIKU YA KILELE CHA MWEZI WA SHUKRANI

Image
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa TUZO Maalumu na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Dkt. Saada Mkuya Salum na Kamishna wa ZRB Ndg.Yussuf J.Mwenda, wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Kilele cha mwezi wa Shukrani na Furaha kwa Walipakodi Zanzibar kwa mwaka 2021/2022, Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 29-12-2022.(Picha na Ikulu)  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakiangalia ngoma ya Kibati walipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja kuhudhuria Maadhimisho ya Siku ya Kilele cha mwezi wa Shukrani na Furaha kwa Walipakodi Zanzibar mwaka 2021/2022.Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) zilizofanyika katika ukumbi wa hoteli hiyo leo 29-12-

KIFO CHA PELE: BRAZIL YATANGAZA SIKU 3 ZA MAOMBOLEZO

Image
  Brazil imetangaza siku tatu za maombolezo kufuatia kifo cha gwiji wa soka dunia  Edson Arantes do Nascimento,  maarufu PELE kilichotokea huko Sao Paulo Desemba 29, 2022. Pele amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82 baada ya kuugua kwa miss mrefu. Atakumbukwa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusakata kabumbu. Anasifiwa kwa kufunga mabao 1,281 katika rekodi ya dunia katika mechi 1,363 katika kipindi cha miaka 21 ya maisha yake, yakiwemo mabao 77 katika mechi 92 za nchi yake. Mchezaji pekee aliyeshinda Kombe la Dunia mara tatu, akinyakua taji hilo mnamo 1958, 1962 na 1970, Pele alitangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Karne wa Fifa mnamo 2000. Alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya figo na kibofu katika miaka ya hivi karibuni. Pele alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye utumbo wake mnamo Septemba 2021 katika Hospitali ya Albert Einstein mjini Sao Paulo, baada ya uvimbe huo kugunduliwa katika vipimo vya kawaida. Alirejeshwa hospitalini mwishoni mwa Novemba 2022. Binti yake Kely N

KUTOKA MAGAZETINI LEO IJUMAA DESEMBA 30, 2022

Image