Posts

Showing posts from April, 2022

MWENYEKITI WA CCM RAIS SAMIA APIGA KURA UCHAGUZI WA CCM SHINA LA IKULU CHAMWINO

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitumbukiza karatasi ya Kura kwenye boksi kuwachagua Wajumbe wa Shina namba 1 la Chama hicho Chamwino Ikulu Jijini Dodoma tarehe 30 Aprili, 2022. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wanachama wa CCM mara baada ya kupiga kura kumchagua Mwenyekiti pamoja na Wajumbe wa Shina namba 1 la Chama hicho Chamwino Ikulu Jijini Dodoma tarehe 30 Aprili, 2022. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo kabla ya kumpigia kura Mwenyekiti na Wajumbe wa Shina namba 1 la Chama hicho Chamwino Ikulu Jijini Dodoma tarehe 30 Aprili, 2022. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aki

NAULI MPYA ZA DALADALA NA MABASI YA MIKOANI KUANZA KUTUMIKA WIKI MBILI ZIJAZO: LATRA

Image
  Mamlaka ya udhibiti wa usafiri nchi kavu (LATRA) imetangaza bei mpya za nauli za mabasi na daladala nchini. Akitangaza kiwango hicho kipya cha nauli leo Jumamosi Aprili 30, 2022 Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Gilliard Ngewe amesema kiwango hicho kipya kitaanza kutumika baada ya siku 14. Ngewe amesema nauli mpya ya daladala kuanzia KM 0-10 itakua Tsh. 500 kutoka Tsh. 400 na KM 11-15 nauli itakua Tsh. 550 kutoka Tsh. 450 na bei ya mwisho ya daladala kwa KM 36 hadi 40 itakua Tsh. 1100 kwa daladala tu. Kwa upande wa nauli za mabasi yaendayo mikoani zimepanda kwa daraja la kawaida ni Tsh. 41.29 kwa KM moja kutoka Tsh. 36.89 huku daraja la kati likipanda kwa shilingi 56.88 kutoka Tsh. 53.22. Nauli kwa wanafunzi imebakia kuwa Tsh. 200 kwa daladala.

MASHAMBA YA TANZANIA PLANTATIONS LTD YAKABIDHIWA KWA SERIKALI

Image
Na  Munir Shemweta, WANMM ARUSHA   Serikali imekabidhiwa mashamba yaliyokuwa yakimilikiwa na Kampuni ya Tanzania Plantations Ltd yenye ukubwa wa ekari 6,176.5 katika wilaya za Arusha na Arumeru mkoani Arusha na hivyo kumaliza mgogoro wa muda mrefu.    Mgogoro kati ya Kampuni ya Tanzania Plantations Ltd na Serikali uliibuka mwaka 1999 baada ya kampuni hiyo kupinga ubatilisho wa mashamba yake uliofanywa na serikali kutokana na kampuni hiyo kushindwa kutimiza masharti ya umiliki jambo lililoifanya kufungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Arusha mwaka 2015.   Hata hivyo, katika kutafuta suluhu nje ya Mahakama Serikali kupitia Wakili Mkuu wa Serikali Mei 15, 2019 aliwasilisha ombi la kufanya majadiliano na mdai kwa lengo la kumaliza shauri nje ya mahakama ambapo Mahakama iliridhia pande mbili za shauri kumaliza suala hilo nje ya mahakama.   Makabidhiano ya mashamba hayo yaliyokuwa yakijulikana kama Karangai na Lucy Estate yanahitimisha mgogoro kati ya serikali na Kampuni ya Tanzania Plantations

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAMOSI APRILI 30, 2022

Image
 

TANZANIA, BURUNDI NA DRC ZATAFUTA FEDHA KUJENGA RELI YA KISASA YA PAMOJA

Image
Na Benny Mwaipaja, Washington DC   Nchi za Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zimewasilisha maombi ya kupatiwa mkopo wenye masharti nafuu kwenye Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Uvinza-Msongati- Gitega, yenye urefu wa Km 939, uliokisiwa kugharimu dola za Marekani milioni 900.   Majadiliano ya awali kati ya Benki hiyo na Mawaziri wa Fedha wa Nchi hizo tatu, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba wa Tanzania, Mhe. Nicolas Kazadi wa DRC na Mhe. Dkt. Domitien Ndihokubwayo wa Burundi, yamefanyika Washington DC, kando ya Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, Washington DC, nchini Marekani. Akizungumza baada ya kikao hicho, Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alisema kuwa reli hiyo ni muhimu kwa ustawi na maendeleo ya kiuchumi ya nchi zote tatu kwa sababu itakapokamilika itarahisha usafirishaji wa mizigo, abiria na kukuza biashara na maendeleo ya viwanda ya

WCF YAZOA TUZO TATU MAADHIMISHO YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

Image
  Mwandishi wetu - DODOMA Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umepata tuzo tatu katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi Duniani mwaka 2022 ambapo kwa Tanzania yamefanyika katika viwanja vya Kituo cha Mikutano Jakaya Kikwete, jijini Dodoma. Akizungumza wakati wa kilele hicho, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amewataka waajiri na wafanyakazi kuendelea kushirikiana pamoja ili kuweka mazingira yenye usalama na afya katika maeneo ya kazi ikiwemo kuzuia vihatarishi. Amefafanua kuwa, kuweka mazingira salama kunapunguza gharama kwa sababu wafanyakazi wanapopata ajali au ugonjwa kutokana na kazi inavuruga mipango ya uzalishaji kwa pande zote mbili. “Waajiri na wafanyakazi ni lazima wafahamu suala la afya na usalama mahali pa kazi ni mkakati wa pamoja na ni sehemu ya utekelezaji wa Mfumo wa haki na wajibu ulioainishwa kimataifa na kanuni ya kuzuia vihatarishi inapewa kipaumbele cha juu

VIONGOZI WAHIMIZA MSHIKAMANO ZAIDI KATIKA KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA.

Image
Viongozi wa dini,  Serikali na siasa nchini  wamehimiza umuhimu wa  kuendelea kumwombea dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuwatumikia Watanzania  kwa haki, usawa na uadilifu ili kuharakisha upatikanaji wa Maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.  Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ali, Naibu Waziri wa Mifugo Abdallah Ulega na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, walieleza hayo (jana)  Alkhamis 28 Aprili 2022 waliposhiriki katika  dua maalumu ya  kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe  Samia Suluhu Hassan  iliyofanyika katika msikiti wa Mtoro Jijini Dar Es Saalam. Dua hiyo iliambatana na mkesha wa ibada ya usiku maalumu wa  "Lailatul al Qadir' ilihudhuriwa na viongozi na waumini mbalimbali wa dini ya Kiislamu nchini. 

MCHUNGAJI PETER MSIGWA "AMWAGIA SIFA" RAIS SAMIA, NI KUTOKANA NA FILAMU YA THE ROYAL TOUR

Image
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID MJUMBE wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kufuatia juhudi kubwa anazofanya za kuitangaza nchi kupitia filamu ya The Royal Tour. Mchungaji Msigwa ameita kitendo hicho cha Mhe. Rais kuwa ni jambo la kizalendo na anapaswa kutiwa moyo na kila Mtanzania. Akiandika kwenye ukurasa wake wa tweeter Mchungaji Msigwa ameendelea kusema kuwa Kwa namna iwayo yote ile hii ni hatua kubwa positive. “Inawezekana kunaweza kuwa na mapungufu kwenye Filamu ya ROYAL TOUR! Lakini jambo alilolifanya Mh SSH ni jambo la kizalendo na la kutiwa moyo. Mara nyingi nikiwa bungeni nimeshauri kuitangaza Tanzania kwa nguvu kimataifa. Kwa namna iwayo yote ile hii ni hatua kubwa positive.” Ameandika Mchungaji Msigwa. Tayari filamu ya The Royal Tour imeshazinduliwa nchini Marekani na sasa inaendelea kufanyiwa uzinduzi nchini ambapo Aprili 28, 2022 ilizinduliwa kwenye mji wa kitalii wa Arush

RAIS MWINYI NA MAKAMU WAKE WA RAIS WASHIRIKI FUTARI ILIYOANDALIWA NA UBALOZI WA OMAN

Image
 Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Husein Ali Mwinyi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman, pamoja na viongozi wengine wakiwa katika Iftar ya pamoja iliyoandaliwa na Balozi mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar, Mhe. Said Salim Al-sinawy, iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar, Aprili 28.