Posts

Showing posts from December, 2021

RAIS WA ZANZIBAR AMTEUA CHARLES HILARY KUWA MKURUGENZI WA MAWASILIANO IKULU

Image
  Charles Martin Hilary Mkurugenzi Mteule wa Idara ya Mawasiliano, Ikulu Zanzibar

NAIBU WAZIRI WA AFYA DKT. MOLLEL AUTAKA UONGOZI WA HOSPITALI YA MWANANYAMALA KUBORESHA HUDUMA KWA WATEJA

Image
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel ametembelea na kukagua hali ya utaoaji wa huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala na kuwataka kuboresha hali ya utoaji huduma kwa wateja. Akiwa  katika ziara hiyo ya kawaida, Dkt. Mollel aliwatoa hofu wafanyakazi na kuwataka kuwa kitu kimoja ilikukamilisha lengo la kusaidia Wananchi na kutoa huduma bora za tiba na kuokoa maisha ya wananchi. “Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan amewekeza vifaa na mambo mengine na kufanya kazi nzuri sana ya kuboresha hii Hospitali hivyo nimekuja nikae na watumishi wenzangu sisi sasa tuelekee kwenye kufanya kazi haina sababu tena kwa Wananchi kulalamika." Amsema Dkt. Mollel. Aidha Dkt. Mollel ameupongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kuanza kufanyia kazi changamoto zilizokuwepo awali na kuwataka kujikita zaidi katika kuboresha utendaji kazi wa watumishi na nidhamu kazini. "Mimi niwapongeze, nimeingia kwenye idara ya akina Mama pale nimeona kwam

WAZIRI JAFO ASITISHA SHUGHULI ZA UCHIMBAJI MADINI YA NICKEL MLIMA WA YOBO,CHAMWINO JIJINI DODOMA

Image
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesitisha shughuli za uchimbaji wa madini ya nickel katika eneo la mlima wa Yobo wilayani Chamwino mkoani Dodoma kutokana na kutokidhi Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004. Ametoa maelekezo hay oleo Desemba 30, 2021 wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya    kutembelea na kukagua shughuli za mazingira katika maeneo ya wachimbaji wilayani humo Dkt. Jafo alimtaka mwekezaji huyo wa kuusajili mradi huo katika ofisi za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kati ili wataalamu wajiridhishe kuhusu athari za mazingira katika eneo hilo. “Hawa watu huko chini wataathrika na athari zinazoweza kutokea kutokana na uchimbaji huu usiofuata matakwa ya sheria na baadaye watakuja kuilaumu Serikali kwa hiyo namuagiza aanze mara moja mchakato wa kupata Cheti cha Athari kwa Mazingira (EIA),” alisema Dkt. Jafo. Alisema pamoja na kwamba wachimbaji wengi wanadai wana mpango kazi wa kulinda mazi

ASKOFU MKUU MSTAAFU KANISA LA TAG AZIKWA KIJIJINI KWAO VWAWA,MBOZI MKOANI SONGWE

Image
  Naibu Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson akitoa heshima zake za mwisho wakati wa ibada ya mazishi ya Askofu Mkuu mstaafu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Dk Ranwell Mwenisongole iliyofanyika Uwanja wa CCM Songwe .Kulia Kwake ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof, Elisante Ole Grabiel. Askofu Mkuu mstaafu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Dk Ranwell Mwenisongole alifariki Dunia Desemba 25, 2021 katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa Matibabu akiwa na Umri wa miaka 75. Maziko yake yamefanyika kijijini kwao Vwawa wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe. Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi akishiriki ibada ya mazishi ya Askofu Mkuu Mstaafu  wa Kanisa la TAG Ranwell Mwenisongole, ibada iliyofanyika Uwanja wa CCM Songwe.Waziri Mahundi ametoa pole kwa Kanisa,waumini na mtoto wa marehemu ambaye ni Mbunge wa Mbozi George Mwenisongole.

KUTOKA MAGAZETINI LEO IJUMAA DISEMBA 31, 2021

Image
 

KUTOKA MAGAZETINI LEO ALHAMISI DISEMBA 30, 2021

Image