WIZARA YA MADINI YAJA NA MKAKATI KABAMBE KUWAANDAA WATANZANIA WENYE USHINDANI
#Yageukia Vyuo vikuu, kati kutengeneza wataalam #Iko mbioni kurekebisha mitaala kuongeza tija Sekta ya Madini #Yadhamiria kutafsiri Vision 2030 kwa vitendo Serikali iko mbioni kupitia na kurekebisha mitaala ya elimu kwa Vyuo Vikuu na vya Kati kwa ajili ya kutengeneza wataalam wa kutosha na wenye ushindani mkubwa kuhudumia Sekta ya Madini nchini. Hayo yalielezwa na Kamishna wa Tume ya Madini, Janet Ruben Lekashingo, Oktoba 30, 2023, jijini Dodoma, katika mahojiano maalum na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Madini. Alisema katika kutafsiri Maono 2030, Madini ni Maisha na Utajiri, Wizara ya Madini imeamua kuongeza nguvu katika nyanja ya uboreshaji wa tija kwa watumishi pamoja na watoa huduma katika sekta ya madini. Kamishna Janet alisema katika kusimamia ushirikishwaji wa Watanzania katika mnyororo mzima wa Sekta ya Madini, Serikali itashirikiana na Kampuni zilizowekeza sekta ya madini hapa nchini ili kujua uhitaji wao kwenye huduma wanazopatiwa na Watanzania katika miradi