Kamishna
Msaidizi wa
Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani Grace Lobora akizungumza kuhusu
tukio la kukamatwa kwa wahamiaji haramu karibu na hifadhi ya Taifa ya
Saadani
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius
Chatanda akizungumza kuhusu tukio hilo kulia ni Mkuu wa wilaya ya
Pangani Zainabu Abdallah Issa kushoto ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Baraka Batenga
Kamishna
Msaidizi wa
Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani Grace Lobora kushoto
akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina
Matagi wakati wa tukio hilo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius
Chatanda kushoto akisisitiza jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Pangani kulia Zainabu Abdallah Issa na anayefuatia ni Kamishna Msaidizi wa
Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani Grace Lobora
Kamishna
Msaidizi wa
Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani Grace Lobora kushoto akisisitiza
jambo wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda kuhusu namna
walivyofanikisha ukamataji huo wa wahamiaji haramu
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda kushoto akiwa na Mkuu wa
Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi wakiwahoji wahamiaji
haramu hao
Mkuu
wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi kulia akisisitiza
jambo wakati akieleza namna wahamiaji hao walivyokamatwa
Sehemu ya Wahamiaji haramu hao waliokamatwa
ASKARI wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wilayani Pangani
wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 32 waliokutwa wakiwa karibu na hifadhi
hiyo wakisafirishwa kupelekwa nchi za kusini mwa Afrika.
Akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa wahamiaji hao Kamishna Msaidizi wa
Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani Grace Lobora alisema kwamba wahamiaji
hao walikamatwa Septemba 27 mwaka huu usiku.
Alisema
ukamatwa huo waliofanya baada ya kupata taarifa kutoka wananchi wa Kijiji cha
Buyuni kupitia Mwenyekiti wa Kijiji hicho Diwani Akida ambaye aliwaeleza uwepo
wa mazingira yasiyoridhisha kwenye eneo lake hasa eneo la bahari baada ya boti
moja kukwama.
Alisema
baada ya kupata taarifa hiyo wao kama wahifadhi wana jukumu la kulinda
maliasili na kuangalia usalama kwenye miji yote inayowazunguka waliandaa kikosi
kazi cha kwanza waliokwenda eneo la tukio na walipofika waliwakuta wahamiaji
hao eneo la bahari karibu na hifadhi hiyo katika kijiji cha Buyuni.
“Tulipofika tuliwaweka chini ya ulinzi na
baadae tukawasiliana na Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi
ambaye alitoa ushirikiano mkubwa kwa sababu wanaandaa askari kwa kuwapa msaada
baada ya kuangalia umbali kutoka Pangani mpaka eneo la tukio”Alisema
Alisema
baadae hapo waliamua kutuma kikosi cha pili na ndipo walipofika na kufanikiwa
kukaweka chini ya ulinzi wahamiaji 28 ambao ni raia wa Ethiopia lakini alfarji ya leo wakapata taarifa nyengine
ya uwepo wa wahamiaji wengine wanne ambao ni raia wa Somalia na wakatuma kikosi
na kufanikiwa kuwaweka chini ya ulinzi.
“Kati
yao wapo wahamiaji 32 raia wa Ethiopia 28 na raia wa Somalia wanne akiwemo
mwanamke mmoja kwa hiyo baada ya kufanikisha tukio hilo tumewafikisha na
kuwakabidhi kwenye mamlaka ya Polisi kwa ajili ya hatua zaidi”Alisema
Awali
akizungumza kuhusiana na tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius
Chatanda aliwapongeza askari wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani kwa kazi nzuri kwa
kushirikiana na askari wa Jeshi la Polisi wilaya ya Pangani.
“Kwa
kweli niwapongeze askari wa hifadhi ya Taifa ya Saadani ka kazi nzuri
kufanikisha kukamatwa kwa wahamiaji hao kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi
Pangani niwaambie tu kwamba mawakala wanaojishughulisha na usafirishaji wa
wahamiaji haramu mkoani Tanga hawatasalimika tutawasaka popote iwe ni nchi
kavu,majini na kisha kufikishwa mahakamani
Hata hivyo amesema kwamba hivi sasa wametangaza vita mpya kwa mawakala wanaojishuhulisha na usafirishaji wa
wahamiaji haramu mkoani Tanga kwamba hawatasalimika watasakwa popote iwe ni
nchi kavu, majini na kisha kufikishwa mahakamani.
Alisema
juhudi hizo ni nzuri na zinapaswa kuwa endelevu ili kuweza kuhakikisha
wahamiaji haramu hawapiti tena kwenye maeneo hayo ikiwemo wananchi kuendelea
kuwafichua wanapowaona watu na kuwatilia mashaka.
“Labda
niwaambie tu kwamba wale wanaojihusisha na usafirishaji wa wahamiaji haramu
mkoani hapa hawatabaki salama kwa sababu huo ni uhalifu unaovuta mipaka na
uhalifu huu hauwezi kukubalika hapa nchini”Alisema
“Sisi
sote tunafahamu kinachoendelea nchini Somalia tunauhakika gani wanaweze wakawa
wanapita wakaenda hawawezi kwenda kuungana na wenzao nchini msumbiji …tuna
uhakika gani hawawezi kubaki masalia nchini wakafanya wanayoyafanya huko
walipotoka”Alisema
Naye
kwa upande wake Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Baraka Batenga alisema ni kweli
lipo wimbo la wahamiji haramu kutoa pembe ya afrika kuja Tanzania kwa nia ya kupitia
kwenda kusini mwa Afrika kwea lengo la kwenda kujitafutia maisha bora.
Alisema
katikati kulikuwa kumetulia hasa kwenye kipidi cha ugonjwa wa Corona labda wanaamini
hiyo ilitokana na majirani zao walikuwa wameweka vizuizi vya watu kutoka sehemu
moja kwenda jengine.
Alisema
lakini hivi karibuni wimbi hilo limeanza kupanda na wao wanakabilia nalo na walianza
kukabiliana nalo kwa wilaya za Mkinga ambao wanaingilia maeneo ya moa,jasini
kupitia mwakijembe kwa sasa wameweka task force ndogo kama sehemu ya mkakati ya
kukabilia na wimbi la wahaamiaji haramu na wamekuwa na mafanikio makubwa na
kuweza kudhibiti kwa kiasi kikubwa.
“Kwani
Katika kipindi cha Agosti mpaka leo wilaya ya Mkinga wamekamatwa wahamiaji
haramu kutoka nchini Ethiopia 37 na Muheza 7, Handeni waethipia 8 ambao
walikuwa hawakutani nao ni wasomali na hivyo ni kesi ya kwanza kutokana na
kwamba hawajakamtwa muda mrefu”Alisema
Hata
hivyo alisema wanaofanya mambo hayo ni watanzania na kibaya zaidi hivi karibuni
wilaya ya Muheza walimkamata mwenyekiti wa kijiji cha Upare naye ameingia
kwenye kundi hilo hawakumuacha salama yupo kwenye mikono ya sheria .
Hata
hivyo Mwenyekiti wa Kijiji cha Buyuni Diwani Akida alisema kijiji hicho
kimepakana na hifadhi ya Taifa ya Saadani alisema hali ya usalama sio nzuri
kiupande wao huku wanawashukuru wenzao wa hifadhi ya Taifa ya Saadani wanatoa
msaada sana kwao wakati panapojitokeza matatizo yoyote wanakuwa karibu
kuwasaidia.
Alisema
kama Septemba 27 mwaka huu saa moja
usiku walifika wasomali na boti yao hatukujua wana silaha gani lakini
walipofika ikabidhi tukawazingira na kutoa taarifa kwa Saadani kwa sababu wapo wakafika
wakawadhibiti na baadae pia kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi wilaya ya Pangani
walipofika wakawachukua.