Posts

Showing posts from April, 2024

TUME YA MADINI YAENDESHA MAFUNZO YA PEPMIS

Image
Tume ya Madini kupitia Kurugenzi ya Huduma za Tume leo Aprili 29, 2024 imeendesha mafunzo maalum kuhusu utekelezaji wa mfumo wa upimaji wa utendaji kazi kwa watumishi (PEPMIS) kwa Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa jijini Dodoma Akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Huduma za Tume, Meneja wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Fatma Chondo amesema kuwa lengo la mafunzo ni kuongeza ufanisi wa watumishi na kuwezesha Tume ya Madini kufikia malengo ya Serikali hasa kwenye maeneo ya ukusanyaji wa maduhuli, ongezeko la wawekezaji kupitia utafiti, uchimbaji, uchenjuaji na biashara ya madini sambamba na kuongeza ushiriki wa watanzania katika Sekta ya Madini .

RAIS SAMIA AHUDHURIA MKUTANO WA IDA NAIROBI

Image
Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Kenya Mhe. Dkt. William Ruto alipowasili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi,  Kenya tarehe 29 Aprili, 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 ya IDA. Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Kenya Mhe. Dkt. William Ruto alipowasili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi,  Kenya tarehe 29 Aprili, 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika  wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA. Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA k

RAIS SAMIA KUSHIRIKI MKUTANO WA IDA NAIROBI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha (kulia) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 28 Aprili, 202 4   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaM he. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Afya  wa Kenya Susan Nakhumicha mara baada ya kuwasili katika  uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini  Nairobi nchini Kenya tarehe 28 Aprili, 2024. Rais Samia  anatarajia kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika w enye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze  Kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA. IDA ni Mfuko  Maalum wa Benki ya Dunia unaotoa mikopo nafuu na  misaada kwa nchi zinazoendelea. Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na baadhi ya Watanzania waliofika kumpokea Jijini Nairobi baada ya kuwasili kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumb

HATUA ZA DHARURA ZAENDELEA KUCHUKULIWA NA TANROADS MOROGORO KUREJESHA MIUNDOMBINU

Image
Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Morogoro imewataka Wananchi wa Mkoa huo kuwa watulivi wakati Serikali ikiendelea kuchukuwa hatua za dharura kurejesha miundombinu ya barabara na madaraja yaliyoharibika katika kipindi hiki cha mvua kubwa . Akizungumzia athari za mvua hizo tarehe 28 Aprili 2024; Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro Mhandisi Alinanuswe L. Kyamba ameeleza kuwa tayari Wakandarasi wapo katika maeneo yote yaliyo athirika na kazi ya urejeshwaji wa miundombinu hiyo inaendelea. "Mvua hizi sio Ulanga peke yake ni Nchi nzima, lakini kwa Ulanga Mwezi Februari liliondoka daraja katika Kijiji cha Mwaya daraja lile liliondoka kwa sababu ya mafuriko tukapeleka daraja la chuma la dharura, tumejenga daraja kwa wiki mbili kwa sasa hakuna shida panapitika" Ameainisha maeneo mengine yaliyo athiriwa na mvua hizo ni pamoja na Malinyi, Mlimba, Masagati na Uchendule ambapo pia ameeleza tuelewe kwamba mvua za mwaka huu zimekuwa kubwa kupita kiasi.

KUTOKA MAGAZETINI APRILI 29, 2024

Image