Posts

Showing posts from June, 2022

AMIRIJESHI MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA, RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AMUAPISHA MKUU MPYA WA MAJESHI (CDF)

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania (Chief of Defense Forces-CDF) Jenerali Jacob John Mkunda mara baada ya hafla ya uapisho iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Juni, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania (Chief of Defense Forces-CDF) Jenerali Jacob John Mkunda katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Juni, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvalisha Cheo kipya cha Luteni Jenerali Salum Haji Othman kabla ya kumuapisha kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (Chief of Staff -C of S) katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Juni, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoj

MWENYEKITI WA BODI, SUMA JKT, MEJA JENERALI (MSTAAFU) FARAH ABDI MOHAMMED AIPONGEZA TAASISI HIYO KWA KUZALISHA BIDHAA BORA

Image
NA KHALFAN SAID, SABASABA Meja Jenerali (mstaafu) wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Farah Abdi Mohammed, amesifu ubora wa bidhaa zinazozalishwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) wakati alipotembelea Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 46 ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye viwanja vya Julius Nyerere, maarufu Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Juni 29, 2022. Meja Jenerali (mstaafu) Farah, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo linaloendelea kukua kwa kasi, aliyasema hayo wakati alipotembeela banda la Suma JKT ili kujionea jinsi watendaji wa taasisi hiyo wanavyowahudumia wananchi wanaofika kwenye banda hilo. Baadhi ya shughuli zinazotekelezwa na SUMA JKT ni pamoja na Viwanda, Biashara, Ujenzi na Uhandisi, Kilimo na Ufugaji. Baadhi ya bidhaa zilizowekwa katika maonesho hayo ni pamoja na zitokanazo na mazao ya misitu kama vile samani za ofisini, shule na nyumbani, asali, vifaa vya kilimo, bidhaa za ngozi kama vi

KUTOKA MAGAZETINI LEO ALHAMISI JUNI 30, 2022

Image
   

KUTOKA MAGAZETINI LEO ALHAMISI JUNI 30, 2022

Image