TANZANIA NA UHOLANZI ZATILIANA SAINI MKATABA WA MSAADA WA KUENDELEZA BONDE LA MSIMBAZI
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kulia) na Balozi wa Serikali ya Ufalme ya Uholanzi, Mhe. Wieber De Boer, wakionesha hati ya mkataba wa msaada wa euro milioni 30, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 82 za Tanzania, kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Undelezaji Bonde la Msimbazi, Jijini Dar es Salaam, iliofanyika katika Ofisi za Hazina Ndogo , Jijini Dae es Salaam . Msaada huo wa euro milioni 30 zilizotolewa na Uholanzi, ni sehemu ya gharama ya Mradi huo wa Undelezaji Bonde la Msimbazi utakaogharimu dola za Marekani milioni 260, ambapo kati ya kiasi hicho, Benki ya Dunia itatoa dola za Marekani milioni 200 na Serikali ya Hispania itatoa euro milioni 30 kama mkopo nafuu. Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kulia) na Balozi wa Serikali ya Ufalme ya Uholanzi, Mhe. Wieber De Boer, wakisaini mkataba wa msaada wa euro milioni 30, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 82 za Tanzania, kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Undelezaji Bonde la Msimbazi, Jij