11/30/2020

WABUNGE WAWILI WALIOTEULIWA NA MHE. RAIS WAAPISHWA BUNGENI JIJINI DODOMA

Wabunge wa Kuteuliwa na Mheshimiwa Rais, Mhe. Riziki Lulida na Mhe. Humphrey Polepole wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge Mhes. Job Ndugai na Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai mara ya kuapishwa kwenye viwanja vya Bunge hii leo Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Mbunge wa Kuteuliwa na Mheshimiwa Rais, Mhe. Riziki Lulida akila kiapo mbele ya Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai katika viwanja vya Bunge hii leo Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Mbunge wa Kuteuliwa na Mheshimiwa Rais, Mhe. Humphrey Polepole akila kiapo mbele ya Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai katika viwanja vya Bunge hii leo Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge)
 

    

RAIS DK.MWINYI AHUTUBIA SEMINA YA VIONGOZI WAANDAMIZI NA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI ILIOANDALIWA NA BENKI YA CRDB HOTELI YA VERDE ZANZIBAR

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Semina Maalum ilioandaliwa na Benki ya CRDB Tanzania kwa Viongozi Waandamizi na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, iliofanyika katika viwanja vya Marina Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar jana usiku 28/11/2020.

MAKAMU Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB Tanzania Profesa Neema Mori  akizungumza na kutowa neno la shukrani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani)  baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya Semina kwa Viongozi Waandamizi na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, iliofanyika katika viwanja vya Marina Hoteli ya Verde Mtoni
Jijini Zanzibar jana usiku 28/11/2020.

WASANII wa Kikundi cha Siti Band wakitowa burudani wakati wa hafla ya Semina ya Viongozi Waandamizi na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliofanyika katika viwanja vya Marina Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar jana usiku 28/11/2020.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB Profesa Neema Mori alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Verde Marina Mtini  Jijini Zanzibar kuhudhuria Semina Maalum  iliyoandaliwa na Benki kwa Viongozi Waandamizi na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliofanyika jana usiku  28/11/2020
katika viwanja vya Marina na (kulia kwa Rais) Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Ndg. Abdulmajid Mussa Nsekela.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi  akisalimiana na kuzungumza na Msanii wa Siti Band Amina Omar Juma, baada ya kumalizika kwa hafla ya Semina ya Viongozi Waandamizi na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliofanyika katika viwanja vya Marina Hotel ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango
Zanzibar.Mhe.Jamal Kassim Ali.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi  akizungumza na kuagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Tanzania Ndg. Abdulmajid Mussa Nsekela na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, wakiwa katika viwanja vya Marina Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar.

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati akihutubia katika hafla ya Semina ya Viongozi Waandamizi na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, ilioandaliwa na Benki ya CRDB Tanzania katika viwanja vya Marina Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa amesimama na Viongozi wa meza kuu wakati ukipigwa wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla Semina ilioandaliwa na Benki ya CRDB kwa Viongozi Waandamizi na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar , iliofanyika katika viwanja vya Marina Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar na (kulia kwa Rais) Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Ndg. Abdulmajid Mussa Nsekela na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamal Kassim Ali na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdull 

BAADHI ya Viongozi wa CRDB na Serikali wakiwa katika ukumbi wa Marina wamesimama baada ya kuwasili Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) ukipigwa wimbo wa Taifa, wakati wa hafla ya Semina maalum ilioandaliwa na Benki ya CRDB kwa Viongozi Waandamizi na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliofanyika kjatika viwanja vya Marina Hoteli ya Verde Mtoni
Jijini Zanzibar jana usiku 28/11/2020

SHEIKH  Abdulkadir Said Abdalla akisoma Quran kabla ya kuaza kuaza kwa Semina Maalum ilioandaliwa na Benki ya CRDB Tanzania kwa Viongozi Waandamazi na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliofanyika katika viwanja vya Marina Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar  jana usiku 28/11/2020

 

MKURUGENZI Mtendajhi wa Benki ya CRDB Tanzania Ndg. Abdulmajid Mussa Nsekela akiwasilisha Mada ya Maendeleo ya Benki ya CRDB kwa Washiriki wa hafla hiyo Viongozi Waandamizi na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, iliofanyika katika viwanja vya Marina Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar jana usiku 28/11/2020.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi  akifuatilia Mada ya Maendeleo ya Benki ya CRDB ikiwasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Ndg. Abdulmajid Mussa Nsekela, iliofanyika jana usiku 28/11/2020 katika viwanja vya Marina Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar na (kulia kwa Rais) Spika wa
Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid na (kushoto kwa Rais) Waziri  wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamal Kassim Ali na Makamu wqa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemede Suleiman Abdulla

WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Jamal Kassim Ali akizungumza wakati wa hafla ya Semina ya Viongozi Waandamizi ba Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar , iliofanyika katika viwanja vya Marina Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar iliofanyika jana usiku 28/11/2020,kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar
kuzungumza kjatika hafla hiyo.

   

WAGENI Waalikwa wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Husseinn Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia katika hafla ya Semina ya Viongozi  Waandamizi  na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar  ilioandaliwa na Benki ya CRDB Tanzania katika ukumbi wa Viwanja vya Marina Hoteli ya
Verde Mtoni Jijini Zanzibar iliofanyika jana usiku 28/11/2020.(Picha na Ikulu)

    

JENERALI MABEYO ATUNUKIWA NISHANI MAALUM YA MLIMA KILIMANJARO

Chuo Kikuu cha Iringa (zamani Tumaini University) kimemtunukia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Salvatory Venance Mabeyo (pichani juu) Nishani Maalum ya Mlima Kilimanjaro (University of Iringa Miunt Kilimanjaro Award) ambayo hutolewa kwa Viongozi wa juu Serikalini ambao wametoa mchango wa kutukuka kwa Chuo au Tasnia ya Elimu kwa ujumla. Tukio hilo limefanyika wakati wa Mahafali ya 23 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika "campus" ya Chuo Mjini Iringa tarehe 28 Nov 20.

Mwingine aliyetunukiwa Nishani hiyo Maalum ya juu wakati wa Mahafali hiyo ni Mkurugenzi wa TAKUKURU, Brigedia jenerali John Julius Mbungo. Kwa mara ya kwanza Nishani hiyo ilitunukiwa kwa aliyekuwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa wakati wa Mahafali ya 22 ya Chuo hicho mwaka 2019.

Jenerali Salvatory Venance Mabeyo
 Brigedia jenerali John Julius Mbungo
 

    

11/29/2020

TANESCO MSHINDI WA JUMLA MASHINDANO YA SHIMMUTA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeibuka mshindi wa jumla katika mashindano ya SHIMMUTA baada ya kunyakua vikombe tisa na kuibuka kidedea katika mashindano hayo ya michezo ya mwaka 2020, yanayofanyika Mkoani Tanga.

Matokeo hayo yanaifanya TANESCO kuwa mshindi wa jumla katika mashindano ya SHIMMUTA mwaka huu yaliyomalizika Mkoani Tanga.

Michezo ambayo TANESCO imeibuka na ubingwa ni wavu wanaume na wanawake, kikapu wanaume na wanawake. Aidha, TANESCO imekuwa mshindi wa pili mchezo wa pete.

Hii ni mara ya nne mfululizo timu ya kikapu wanaume wanakuwa washindi, na mara ya pili mfululizo kwa timu ya wavu wanaume inaibuka na ushindi. 

Kwa upande wa michezo ya jadi TANESCO imeshinda mchezo wa bao wanawake, karata wanaume na mshindi wa pili bao kwa wanaume. 

Mbali ya vikombe hivyo, TANESCO pia imepata medali saba ambapo Polycaps Ernest amekuwa mahindi wa tatu mbio za mita 100 na mita 200, Kulwa Mangala mshindi wa pili mita 1500, Grace Moshi mshindi wa pili mita 400 na 800, mshindi wa tatu mita 100, Imelda Hango 3000 wa tatu.

Akimwakilisha Meneja Mwandamizi Rasilimali Watu, Festo Mkolla ambaye ni, Meneja Usimamizi Utekelezaji Kazi TANESCO, ameishukuru Menejimenti kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Tito Mwinuka kwa kuona thamani ya michezo na kuipa kipaumbele.

Aidha, amewapongeza wanamichezo wa TANESCO kwa nidhamu, juhudi na hali ya kutetea Shirika kwenye mashindano ambayo wameionesha katika kuhakikisha kila mchezo wanaibuka na ushindi.

"Niwaagize viongozi wa timu ambazo hazikuibuka na ubingwa kuhakikisha mnaweka mikakati ili mwakani tuondoke na vikombe vyote" alisema Mkolla.

 Aliongeza, kwa upande wa uongozi wa TANESCO utahakikisha yanafanyika mashindano ya Kanda za kitanesco ili kupata vipaji vipya vitakavyoongeza nguvu kwa wachezaji waliopo.