6/30/2021

TFS WATOA MSAADA WA VITI, MEZA NA MADAWATI WILAYANI MUHEZA


Mkuu wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo kushoto akipokea msaada wa madawati,viti na meza  kutoka kwa Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema Mwasalanga kwa ajili ya shule za Sekondari ,Msingi na Ofisi za Watendaji vyenye thamani ya Milioni 17.4 vilivyotolewa na Wakala wa Misitu Tanzania ( TFS)
MKUU wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo kulia akimkabidhi msaada huo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza mara baada ya kuvipokea kulia ni Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema Mwasalanga
MKUU wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo akizungumza wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano iliyofanyika wilayani humo kulia  ni Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema Mwasalanga
Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema Mwasalanga akizungumza wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano
Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema Mwasalanga akizungumza wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano
Meneja Mawasiliano wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Martha Chasama akizungumza wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano
MKUU wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo katika akiwa na Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema Mwasalanga kulia akifuatiwa na  Meneja Mawasiliano wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Martha Chasama
Wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika makabidhiano hayo
Sehemu ya madawati yaliyotolewa

NA OSCAR ASSENGA, MUHEZA

WAKALA wa Huduma za Misitu TFS shamba la Lunguza lililopo wilayani Muheza mkoani Tanga wametoa msaada wa madawati, viti na Meza vyenye thamani ya sh mil17. 4

Msaada huo ambao ni kwa ajili ya shule za msingi na Sekondari Tatu ambazo ni pamoja na Ofisi za watendaji kata mbili zilizopo wilayani Muheza utasaidia kuondosha changamoto zilizokuwepo awali.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo, Mhifadhi wa shamba la miti Longuza Ellyneema Mwasalanga alisema kuwa msaada huo ni kwa ajili ya kusaidia kuboresha utoaji wa huduma.

"Tumetoa viti na Meza 17 kwa ajili ya Ofisi za watendaji na madawati 60 kwa shule za msingi na Sekondari" alisema Mwasalanga.


Awali akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo aliishuku TFS kwa namna walivyothamini elimu ya Watoto wa kitanzania na hivyo kwa msaada huo wataweza kuboresha utoaji wa elimu.

Mkuu huyo wa wilaya alitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa kuilinda misitu kuhakikisha hakuna uharibu unaofanyika.

"Niwaombe wananchi huu msitu unatunufaisha hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tunaulinda ili uweze kutusaidia katika kukuza kipato chetu na uchumi" alisema DC Bulembo

Naye kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Martha Chasama alisema wametoa madawati 60 ambapo kati ya hiyo madawati 30 wametoa kwenye shule ya Msingi Kwemdimu, madawati 30 shule ya Sekondari Potwe na madawati 30 wametoa shule ya Sekondari Amani.

Alisema pia wametoa viti na meza 17 ambavyo wametoa ambapo thamani hizo ni sh.milioni 17.1 wao kama wahifadhi wanasema wahifadhi wa baadae ni watoto wadogo ambao wamewatolea thamani hizo.

“Misaada hiyo wanayoitoa kwa shule hizo na ofisi za watendaji tunaomba thamani hizo zitunzwe pamoja na walimu waangalia watoto namna wanavyocheza kwa sababu wakati mwengine wanaweza wakawa wanabonda madawati  ili nao kama wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) waweze kupata nguvu ya kuendelea kutunzwa zaidi”Alisema
    

HALMASHAURI KUU CCM WAAZIMIA KUTOA TAMKO KUMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA YA KUONGOZA NCHI

 KIKAO cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) kimefanyika Jumanne  leo Juni 29, 2021 chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa White House Dodoma.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa wameazimia na kutoa tamko la kumpongeza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Husein Ali Mwinyi  kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuiongoza nchi na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM 2020 - 2025.
Kupitia taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Juni 29,2021 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka amesema aidha wajumbe hao wamebainisha kuwa tokea nchi ilipopata msiba mkubwa wa kuondokewa na aliyekuwa  Rais, Hayati Dkt. John Magufuli, ndani ya siku  100 za uongozi  wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa na kuonyesha dira ya serikali anayoiongoza kuwa inazingatia uadilifu, Utawala wa Sheria, Haki, Usawa, kuimarisha misingi ya demokrasia, umoja na mshikamano zaidi kuendelea kutunza Amani na usalama wa nchi.
Pia katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan  amesisitiza juu ya azma ya Serikali inayoiyongoza kuhakikisha inakamilisha na kuiratibu vyema  miradi yote ya kimkakati iliyoanzishwa na inayoendelea kutekelezwa sambamba na kuhakisha uchumi wa nchi unakuwa kwa kasi.
“Miradi yote iliyopo kwenye maeneo yenu viongozi wa CCM mnao wajibu wa kuifatilia, kuikagua na kujua uendelevu wake bila uwoga kwani  huo ni wajibu wenu wa msingi katika kutusimamia Serikali, hilo liende sambamba na kuhakikisha mnasaidia kuona mapato ya Serikali hayapotei.
"Katika vyanzo vyote vya  ukusanyaji, ikumbukwe ninyi ndio kioo cha kutumurika, kwavile  ilani inayotekelezwa ni ya Chama Cha Mapinduzi lazima ifanikiwe kwa kiwango kikubwa” Ndugu Samia Suluhu Hasasan Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza na waandishi wa habari kuhusu yaliyojadiliwa kwenye kikao cha kawaida cha NEC
    

SERIKALI YAZINDUA MPANGO WA TATU WA MAENDELEO WA TAIFA WA MIAKA MITANO

 

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, akizindua Kitabu cha Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano jijini Dodoma. Kushoto kwa Waziri Mkuu  ni Spika wa Bunge la Tanzania Mhe.  Job Ndugai. Kuanzia kulia kwa Waziri Mkuu ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango  Mhandisi Hamad Yusuff Masauni, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Daniel Sillo.

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, akionesha Kitabu cha Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano baada ya kukizindua, Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, kulia kwa Waziri Mkuu ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.  Mhandisi Hamad  Yusuf Masauni, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, jijini Dodoma.

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, akimkabidhi Kitabu cha Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango huo.

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, akimkabidhi Kitabu cha Mpango wa Tatu wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya uzinduzi mpango huo jijini Dodoma.


Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, akimkabidhi Kitabu cha Mpango wa Tatu Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango huo jijini Dodoma.


Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, akimkabidhi Kitabu cha mwakilishi wa Mabalozi nchini, Balozi wa Korea Mhe. Kim Yong Sung wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango huo jijini Dodoma.

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel Tutuba akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano jijini Dodoma.

 


Wadau mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (hayupo pichani), wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano jijini Dodoma.
Meza Kuu ikiongozwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (wa nne kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri, Manaibu Waziri, Katibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano jijini Dodoma.

 (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WFM – Dodoma).

 

Na Saidina Msangi, WFM,

Serikali imezindua rasmi Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 hadi 2025/26 unaotarajiwa kugharimu shilingi trilioni 114.8 ambapo Serikali itachangia Sh. trilioni 74.2 na sekta binafsi itachangia Sh. trilioni 40.6.

Mpango huo unaotarajiwa kutekelezwa kwa ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi umezinduliwa jijini Dodoma na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri kuu Mhe. Kassim Majaliwa (Mb), alisema kuwa Mpango huo umezingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025, sera na mikakati mbalimbali ya kisekta, matokeo ya tafiti zilizofanywa na vyuo na taasisi mbalimbali hapa nchini pamoja na dira ya Afrika Mashariki ya 2050.

“Mpango huu una dhima ya kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu na umejikita katika kuchochea uchumi shindani na shirikishi na kuimarisha ukuaji wa uzalishaji wa ndani na utoaji huduma, kukuza uwekezaji na biashara, kuchochea maendeleo ya watu na kuendeleza rasilimali watu”, alisema Mhe. Majaliwa.

Mhe. Majaliwa alisema kuwa katika mpango huu wa tatu Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya kielelezo kama ilivyokuwa katika mpango wa pili hususani ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Standard Gauge (SGR), Ujenzi wa Mradi wa Kufua Umeme wa Maji Julius Nyerere (JNHPP) – 2,115 MW, Ujenzi wa Bomba la Mafuta - East African Crude Oil Pipeline (EACOP) na Ununuzi wa Meli na Ujenzi wa Bandari ya Uvuvi (Mbegani).

“Mpango huo una ushirikishwaji wa kitaifa na kimataifa na kuwa wote kwa pamoja tuna jukumu la kuhakikisha utekelezaji wake unafanikiwa kikamilifu”, alisisitiza Mhe. Majaliwa.

Mhe. Majaliwa ameielekeza Wizara ya Fedha na Mipango kuhakikisha inatoa elimu ya kutosha ili kuwezesha kila mmoja kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wake.

Aidha Mhe. Majaliwa ameagiza wizara zote, taasisi za umma, idara zinazojitegemea wakala wa Serikali, sekta binafsi na wadau wote wa maendeleo kuhakikisha kuwa ofisi zao zina nakala ya mpango huo ili kuwezesha utekelezaji wa viwango.

Amesisitiza kuwa Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa malengo ya mpango huo yatafikiwa na kuwa Serikali haitafumbia macho ukwepaji kodi, uzembe kazini, ufujaji wa fedha na rushwa. 

Akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Massauni (Mb) alisema kuwa mpango huo ni nyenzo muhimu katika kuharakisha maendeleo ya nchi.

Alisema maandalizi ya mpango huo yameshirikisha kikamilifu makundi mbalimbali ya wadau wakiwemo sekta binafsi, asasi za kiraia, mashirika yasiyo ya kiserikali, washirika wa maendeleo na jamii kwa ujumla umezingatia mahitaji halisi ya makundi yote.

“utekelezaji wa Mpango huu utahitimisha utekelezaji wa Mpango Elekezi wa Muda Mrefu (2011/12 – 2025/26) ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambayo ni: maisha bora kwa wananchi; amani, utulivu na umoja; utawala bora; jamii iliyoelimika na inayopenda kujifunza; na uchumi imara na shindani”, alisema Mhandisi Massauni.

Alifafanua kuwa  Serikali imeanza maandalizi ya Dira mpya itakayotekelezwa baada ya kuhitimishwa kwa Dira ya sasa mwaka 2025. Dira hiyo itaendeleza maono na mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Dira 2025 ikijumuisha kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya watu.

Awali akizungumza katika ufunguzi huo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Tutuba alisema kuwa mpango huo umejikita katika maeneo makuu Matano ya kipaumbele ikiwemo kuchochea uchumi shindani na shirikishi.

Pia mpango huo umejikita katika kuimarisha uwezo wa uzalishaji wa viwanda na utoaji wa huduma ambapo itajikita katika kujumuisha miradi ya viwanda  inayolenga kuongeza thamani kwa kuzalisha bidhaa zitakazotumia rasilimali za ndani.

“Serikali inalenga kujumuisha programu za kuimarisha masoko ya ndani na kutumia fursa za masoko ya kikanda na kimataifa kwa bidhaa zinazozalishwa nchini kukuza uwekezaji na biashara”alisema Bw. Tutuba.

Aliongeza kuwa mpango huo pia unalenga kuchochea maendeleo ya watu ambapo Serikali inakusudia kutekeleza miradi itakayoboresha maisha ya watu ikijumuisha eneo la elimu na mafunzo eneo la afya na ustawi wa jamii, upatikanaji wa huduma za maji na uhifadhi mazingira.

Alisema katika kuendeleza rasilimali watu Serikali inajumuisha programu na mikakati mbalimbali ambayo inalenga kuendeleza maarifa na ujuzi wa rasilimali watu nchini katika ngazi zote za elimu ili kuwawezesha vijana waweze kujiajiri.

Aidha katika kuhakikisha vipaumbele vilivyoelezwa vinatekelezwa kwa ufanisi na fedha zinazopatikana kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa wakati mpango huo umeainisha mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ili kuwezesha uwepo wa uwajibikaji.

Naye Mwakilishi Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Nchini (UNDP) Bi. Christina Musisi, alipongeza Serikali kwa kukamilisha mpango huo kwa wakati na kueleza kuwa wananchi, Serikali, wadau wa maendeleo sekta binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali watatumia mpango huo kama nyenzo muhimu ya utekelezaji katika kufikia malengo ya dira ya maendeleo 2025 na ajenda 2030.

Alisema kuwa mashirika ya Umoja wa Mataifa yatashirikiana na Serikali katika kutekeleza mpango huo wa maendeleo kwa miaka mitano ijayo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Sekta Binafsi Bw. Zaki Mbena alisema kuwa mpango huo umetoa nafasi na fursa kwa sekta binafsi kutekeleza majukumu yake na kupata wigo mpana wa kufanya kazi na kupata maelekezo ili kufanikisha mpango huo kwa ufanisi.

Aliongeza kuwa Sekta binafsi nchini itatoa mchango wake kwa Serikali unaokadiriwa kuwa shilingi trilioni 40.6 na hata kuzidi kwa kuwa sekta hiyo imeshirikishwa ipasavyo wakati wa maandalizi ya mpango huo ambao ameuelezea kuwa ni muhimu na unaungwa mkono.

Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22-2025/26 ni wa mwisho katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na unatarajiwa kuanza utekelezaji wake kuanzia mwaka wa fedha 2021/22.

Mpango huo ni mwendelezo wa jitihada za Serikali za kusimamia rasilimali za ndani ya nchi ikijumuisha rasilimali za madini, maliasili, gesi asilia, fedha na rasilimali watu kwa lengo la kuboresha hali ya Maisha ya Watanzania wote.

    

BoT IKO TAYARI KUWAHUDUMIA WANANCHI WATAKAOTEMBELEA MAONESHO YA SABASABA BARABARA YA KILWA,DAR ES SALAAM.

  Meneja Msaidizi wa Idara ya Uhusiano wa Benki Kuu ya Tanzania BoT, Vicky Msina akizungumza na baadhi ya maofisa wa benki kuu katika banda lao leo kwenye  maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam katika  viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Juni 29, 2021.

 

 Baadhi ya wananchi wakipata maelezo kutoka kwa maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania BoT waliotembelea banda hilo kwenye maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Juni 29, 2021.

 

Mmoja wa wananchi waliotembelea katika banda la Benki Kuu ya Tanzania BoT akiuliza swali kwa maofisa wa benki hiyo kwenye  maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Juni 29, 2021.

Baadhi ya Maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania BoT wakiwa tayari kabisa kuwahudumia wananchi watakaotembelea katika banda hilo katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Juni 29, 2021.

    

BANCABC YASHIRIKI KONGAMANO LA KUCHOCHEA UCHUMI TEGEMEZI KWA WATU WENYE ULEMAVU JIJINI DODOMA

 


Mgeni Rasmi wa Mkutano Mkuu wa Uchumi na Mapendekezo ya Siku ya Mwanamke Mwenye Ulemavu Tanzania, Dk Tulia Ackson akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dodoma, jana. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju na Mwenyekiti wa Taasisi iliyoandaa mkutano huo ya Ikupa Trust Fund, Stella Ikupa (wa tatu kushoto)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya ABC, Imani John Bgoya akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchumi na Mapendekezo ya Siku ya Mwanamke Mwenye Ulemavu Tanzania uliofanyika jijini Dodoma, jana. Katikati ni Mgeni Rasmi wa mkutano huo, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson. Mkutano huo uliandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Ikupa Trust Fund.

Baadhi ya watendaji wa Benki ya ABC wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchumi na Mapendekezo ya Siku ya Mwanamke Mwenye Ulemavu Tanzania uliofanyika jijini Dodoma, jana.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angelina Mabula akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya ABC, Imani John Bgoya pamoja na Watendaji wa benki hiyo mara baada ya Mkutano Mkuu wa Uchumi na Mapendekezo ya Siku ya Mwanamke Mwenye Ulemavu Tanzania uliofanyika jijini Dodoma, jana.



====== ======= ======


HOTUBA YA MKURUGENZI MTENDAJI BANCABC KWENYE KONGAMANO LA SIKU MOJA JIJINI DODOMA KUHUSIANA NA KUCHOCHEA UCHUMI TEGEMEZI KWA WATU WENYE ULEMAVU TAREHE 28 JUNI 2021

Ndugu Mgeni Rasmi Mh Deputy Speaker (Naibu Speaker) Dr. Tulia Ackson,

Wabunge walikwa

Mwenyekiti wa Ikupa Trust Fund,

………………………………………………
Wateja wa BancAbc,
watu wenye ulemavu,
Waandishi wa Habari,

Wafanyakazi wenzangu,

Wageni Waalikwa,
Mabibi na Mabwana,

Habari za Asubuhi/Habari za Mchana,

Ni heshima kubwa kwangu kusimama mbele yenu kwenye kongamano hili ambalo nia yake ni kuwajengea uchumi tegemezi kwa watu wenye ulemavu. Sisi BancABC tunayo furaha kubwa kuungana na Ikupa Trust Fund kuwawezesha watu wenye ulemavu kupata haki ya elimu, maarifa pamoja na ujuzi kwa kuwajengea uwezo wa kufikia mafanikio yao na familia zao ili wamudu kujikimu kimaisha wakati wowote.

Uamuzi wa serikali kurekebisha sheria ya fedha ya LGA ya kutenga asilimia kumi kwa ajili ya Wanawake na vijana na sasa kuwajumuisha watu wenye ulemavu ni moja ya sababu kubwa inayodhihirisha kwamba kundi linapaswa kupewa kipaumbele sio tu na serikali bali pia na jamii kwa ujumla na ndio sababu sisi BancABC, pia tumeunganisha nguvu na Ikupa Trust Fund ili kuweza kufanikisha kongamano hili la siku mbili ili mafanikio yake yaweze kuleta suluhisho la kifedha kwa watu wenye ulemavu.

Mheshimiwa Mgeni Rasmi, BancABC kwa kushirikiana na serikali imejizatiti kuendeleza suluhisho la kifedha kwa kutanua wigo wa huduma za kifedha na kuzileta karibu na wananchi wa Tanzania kwa nia ya kupunguza idadi ya wananchi ambao hawajafikiwa na huduma za kifedha na kusaidia kuinua maisha ya wananchi kwa kuongeza upatikanaji wa huduma zetu hapa nchini Tanzania. Mwaka 2018, BancABC ilizindua tawi lake hapa Dodoma kwa lengo hilo hilo, Pia hadi leo tunavyoongea hapa, BancABC tunazo ofisi 10 ndogo za mauzo ambazo zinatoa huduma ya mikopo kwa wafanyakazi wa serikali kwa mkoa huu wa Dodoma.

BancABC iko kwenye mazungumzo na wadau ili kuja na pendekezo la dhamana kwa huduma za kifedha kwa watu wenye ulemavu hapa nchini.

Tukiwa na lengo la kuongeza chachu kwa watanzania kujua na kuwa na utamaduni wa kuweka akiba, kupata riba na kisha kukopa, tumeweza kuzindua huduma ambazo zinawafanya wateja wetu kupata riba kutoka kianzio cha chini cha 10,000 na kisha baadae kukopa kulingana na amana yake na hivyo kuweza kuwawezesha wateja wetu kifedha.

BancABC tunaedelea kuongeza suluhisho katika sekta ya huduma za kifedha kupitia huduma zetu mbalimbali tunazotoa kwa wateja wetu nchini wa soko la kawaida na hata wale wa makampuni tanzu kupitia kwenye matawi yetu yote, mawakala wetu zaidi ya 300 pamoja na ofisi zetu ndogo za mauzo zaidi ya 100 zilizoenea kote nchini. Kwa kupitia njia hii tumefanikiwa kusambaza huduma, na kuwafikia Watanzania walio wengi. Kupitia BancABC Mobi USSD na applikesheni, huduma za benki kwa njia ya mtandao ambazo zinawawezesha wateja wetu kupata huduma za kutoa fedha, kuweka na kupata riba wakiwa popote pale.

Vile vile tunazo kadi za malipo ya kabla ambazo zinapatikana kwenye sarafu 6 ambazo zinawawezesha wateja kufanya malipo bure kwa njia ya mtandao na kwenye vituo vya malipo yaani POS. Vile vile wanaweza kutoa fedha kwenye mashine za ATM za VISA wakati wowote na popote duniani.

Mheshimiwa Mgeni Rasmi,

Nikudhihirishie kwamba kwa hayo yote BancABC imedhamiria kuendelea kuunga mkono watu wanaoishi na ulemavu kwa sababu afya na ulemavu ni moja ya lengo letu Kubwa la kuweza kurundisha kwa jamii.

Mwaka 2018 tulishirikiana na Ikupa Trust Fund kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani – kupitia tukio hilo la kila mwaka lenye lengo la kuongeza uelewa kwa watu wenye ulemavu – kukuza maendeleo yenye ujumuishi na watu wenye ulemavu kwenye jamii. Sisi bado tutaendelea kuja na ubunifu zaidi wa mbinu tofauti tofauti ili kukuza ushirikiano huu zaidi na kufanya kazi sambamba na malengo ya serikali kwa lengo la kuendelea kuleta suluhisho la huduma za kifedha kwa makundi yote hapa nchini.

Asanteni sana kwa kunisikiliza na tunaungana na kauli mbiu ya sasa ‘Kazi iendelee’