Posts

Showing posts from February, 2022

NAIBU WAZIRI KIKWETE APOKEA TAARIFA YA MIGOGORO ARDHI PWANI

Image
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete (katikati) akiwa katika kikao cha kupokea taarifa ya migogoro ya ardhi ya mkoa wa Pwani kilichofanyika leo jijini Dar es salaam.   Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete (katikati) akiwa katika kikao cha kupokea taarifa ya migogoro ya ardhi ya mkoa wa Pwani kilichofanyika leo jijini Dar es salaam. Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa maelekezo katika kikao cha kupokea taarifa ya migogoro ya ardhi ya mkoa wa Pwani kilichofanyika leo jijini Dar es salaam. Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete akisisitiza jambo katika kikao cha kupokea taarifa ya migogoro ya ardhi ya mkoa wa Pwani kilichofanyika leo jijini Dar es salaam. Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Pwani Bi. Lucy Kabyemera akiwasilisha taarifa ya migogoro ya ardhi ya Mkoa wa Pwani kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.

RAIS SAMIA AREJEA NCHINI KUTOKA UAE

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam wakati akitokea Umoja wa Falme za Kiarabu UAE leo tarehe 28 Februari, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam wakati akitokea Umoja wa Falme za Kiarabu UAE leo tarehe 28 Februari, 2022.

WAKUU WA MIKOA WATAKIWA KWENDA MKOA WA PWANI KUJIFUNZA

Image
 KITUO CHA HUDUMA ZA PAMOJA MKOANI PWANI CHAMKOSHA WAZIRI BASHUNGWA * Awataka Wakuu wa Mikoa kuiga mfano wa Pwani * Waziri wa  nchi ofisi ya Rais , TAMISEMI  Mhe. Innocent Bashungwa amefurahishwa na Kituo cha Huduma za Pamoja ( One Stop Center) kilichoanzishwa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa kwa maelekezo ya Mkuu WA Mkoa huo Mhe. Aboubakar Kunenge kwajili ya kutoa huduma za haraka kwa Wananchi wa Mkoa huo. Akizungumza akiwa ziarani Mkoani Pwani Mhe. Bashungwa amesema uwepo Huduma muhimu sehemu moja inamrahishia mwananchi kutohangaika kuzunguka mji mzima kutafuta Ofisi mbalimbali za kutatua shida zake. “Katika kituo hiki tunaona huduma mbalimbali zinapatikana katika eneo mona hapa tunawaona TRA, Uhamiaji, DAWASA, Magereza,TANROAD,TARURA na wengine wengi sasa mwananchi wetu wanaweza kunaliza shida zao sehemu moja na sio ile mtu anafunga safari mpaka Ofisi flani kisha unaambiwa suala hili sio la hapa nenda Ofisi nyingine inachosha lakini kwa hapa mahitaji mengi ya wananchi 

TUTAENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA UMOJA WA AFRIKA-MAJALIWA

Image
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania itaendelea kuunga mkono na kuimarisha ushirikiano uliopo na Umoja wa Afrika hasa katika kuzingatia misingi ya haki za binadamu na utawala bora, demokrasia na utawala wa sheria. Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumatatu, Februari 28, 2022) alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa mkutano wa 64 wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu. Mkutano huo unafanyika jijini Arusha. Mheshimiwa Majaliwa amesema kwama Serikali ya Tanzania ipo tayari kuwapokea na kushirikiana nao pale watakapohitaji ushauri wa aina yoyote. Mkutano huo umefunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho (Majimbo) ya Nigeria Prof. Yemi Osibanjo. Amesema Mahakama hiyo ilianzishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kwa lengo la kusimamia haki za binadamu, ambapo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Samia alipata fursa ya kueleza dhamira ya Tanzania katika kuunga mkono jitihada za mahakama hiyo kufanya kazi. Naye, Makamu wa

WAZIRI MKUU MAJALIWA AMUWAKILISHA RAIS SAMIA UFUNGUZI WA MWAKA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA

Image
Waziri Mkuu KassimMajaliwa leo Februari 28, 2022 amemuwakilisha Mheshimiwa Rais SAMIA Suluhu Hassan katika ufunguzi wa mwaka wa Mahakama ya Afrika, Jijini Arusha. Mgeni rasmi katika ufunguzi huo alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho (Majimbo) ya Nigeria Prof. Yemi Osibanjo .  

TANZANIA YAINGIA MAKUBALIANO YA UWEKEZAJI NA UAE

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akizungumza na Wafanyabiashara na Wawekezaji   kutoka Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji lililofanyika leo tarehe 27 Februari, 2022, Dubai, UAE.   Wafanyabiashara mbalimbali wa Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) wakiwa katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji lililofanyika leo tarehe 27 Februari, 2022, Dubai, UAE.    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akiwa pamoja na viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja na baadhi ya Watanzania Waishio Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) leo tarehe 27 Februari, 2022, Dubai, UAE. PICHA NA IKULU   Sehemu ya Watanzania Waishio Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) wakimsikiliza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  wakati akizungumza nao leo tarehe 27 Februari, 2022, Dubai, UAE

BALOZI KOMBO AKUTANA NA WADAU WA NGO’s JIJINI ROMA

Image
  Na Mwandishi wetu, Roma Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amekutana na kufanya mkutano na wadau wa NGO’s takribani sitini na nne zinazofanya shughuli zake nchini Tanzania mwishoni mwa wiki Jijini Roma, Italia. Mkutano huo ulihudhuriwa pia na wadau mbalimbali wa Diaspora pamoja na wadau wa NGO walimpongeza Mhe. Balozi kwa kuwapa nafasi ya kujitambulisha na kutoa fursa ya kuwasikiliza mafanikio yao sambamba na changamoto wanazopitia katika kufanikisha shughulika zao nchini Tanzania. Pamoja na kuwasikiliza lakini pia Balozi alitumia nafasi hiyo kuwashauri kuwa na ushirikiano wa pamoja ili kuleta ufanisi zaidi kwenye maeneo wanayo yafanyia kazi. Aidha, katika mkutano huo Balozi Kombo aliongea mubashara na Balozi wa Italia nchini Tanzania Mhe. Marco Lombardi na kumpa fursa ya kutoa salaam zake moja kwa moja kwa njia ya mtandao. Balozi wa Italia nchini Tanzania aliwahakikishia wadau hao kuwa wapo kwenye mikono salama ya Balozi wa Tanzania Rome na chini ya uongozi w

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATATU FEB. 28, 2022

Image
 

RAIS SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA AIRTEL AFRIKA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Airtel Afrika Olusegun Ogunsanya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Airtel Afrika Mashariki Ian Ferrao na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Beatrice Singano, mara baada ya mazungumzo na viongozi hao wa Kampuni ya Airtel Afrika leo tarehe 27 Februari, 2022 Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu UAE Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Airtel Afrika Olusegun Ogunsanya pamoja Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Airtel Afrika Mashariki Ian Ferrao leo tarehe 27 Februari, 2022, Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu UAE   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Airtel Afrika Olusegun Ogunsanya pamoja Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Airtel Afrika Mashariki Ian Ferrao leo tarehe 27 Februari, 2022, Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu UAE