WAKUU WA MIKOA WATAKIWA KWENDA MKOA WA PWANI KUJIFUNZA

 KITUO CHA HUDUMA ZA PAMOJA MKOANI PWANI CHAMKOSHA WAZIRI BASHUNGWA

*Awataka Wakuu wa Mikoa kuiga mfano wa Pwani*

Waziri wa  nchi ofisi ya Rais , TAMISEMI  Mhe. Innocent Bashungwa amefurahishwa na Kituo cha Huduma za Pamoja ( One Stop Center) kilichoanzishwa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa kwa maelekezo ya Mkuu WA Mkoa huo Mhe. Aboubakar Kunenge kwajili ya kutoa huduma za haraka kwa Wananchi wa Mkoa huo.

Akizungumza akiwa ziarani Mkoani Pwani Mhe. Bashungwa amesema uwepo Huduma muhimu sehemu moja inamrahishia mwananchi kutohangaika kuzunguka mji mzima kutafuta Ofisi mbalimbali za kutatua shida zake.

“Katika kituo hiki tunaona huduma mbalimbali zinapatikana katika eneo mona hapa tunawaona TRA, Uhamiaji, DAWASA, Magereza,TANROAD,TARURA na wengine wengi sasa mwananchi wetu wanaweza kunaliza shida zao sehemu moja na sio ile mtu anafunga safari mpaka Ofisi flani kisha unaambiwa suala hili sio la hapa nenda Ofisi nyingine inachosha lakini kwa hapa mahitaji mengi ya wananchi  yanatatuliwa sehemu moja” alisema Bashungwa.

Sasa Niwatake Wakuu wa Mikoa Mingine yote nchini kuiga mfano huu na muanzishe One Stopcenter kwenye Ofisi zenu ili wananchi wa maeneo yenu waweze kupata huduma bora kwa urahisi na sio kusumbuka kama zamani.

Kituo cha Huduma za Pamoja Mkoani Pwani kimeanza takribani mwezi mmoja sasa na kinajumuisha Taasisi  zote Wezeshi kutoka huduma katika eneo moja.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais , TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa akiwa na Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhe. Aboubakar Kunenge, wakati akiwa kwenye Kituo cha Huduma za Pamoja ( One Stop Center) kilichoanzishwa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.





Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"