Sunday, January 31, 2021

MKUTANO WA KIMATAIFA WA ELIMU BORA KUFANYIKA KUANZIA APRILI 20, 2021

MKUTANO wa Kimataifa wa elimu bora unatarajia kufanyika Tanzania jijini Dar es salaam kuanzia Aprili 20 hadi 22, 2021 huku ukibeba ujumbe wa mwaka huu kwamba, “Uwajibikaji wa pamoja katika kugharamia elimu bora”. Mkutano huo unatarajia kushirikisha wawakilishi wa mabunge ya Afrika, Wadau wa Maendeleo, Wanazuoni, Bodi za mikopo za elimu ya juu, Vyama vya walimu, Sekta binafisi, Sekta za mawasiliano, Wizara ya Elimu Sayansi na Tekinolojia (MoEST), TAMISEMI, Vyuo vya Ufundi, Wazazi, Wanafunzi na wadau wengine.  

Akizungumza na wanahabari juzi jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga alisema pamoja na mambo mengine mkutano huo mkubwa wa elimu unatarajiwa kujadili mada anuai zikiwemo mchango wa wadau wa maendeleo katika kuboresha ubora wa elimu Tanzania, Matumizi ya Tekinolojia katika kujifunza na kufundisha ili kuboresha elimu zaidi.

Alisema wadau wa elimu pia watajadili Mchango wa serikali katika kuimarisha elimu nyakati za maafa ikiwemo magonjwa ya mlipuko mfano COVID-19, Hatima ya elimu ya juu: Kwanini watahiniwa wengi hawaajiriki na masuala mengine ya elimu lengo ikiwa ni kuhakikisha kunakuwemo na maboresho na maendeleo yanaochagizwa na wadau wa sekta hiyo.

Aidha alisema mada husika zitawasilishwa na wataalam kabla ya washiriki kuanza kujadiliana katika mkutano huo, huku akiweka bayana kuwa ujumbe wa mwaka huu umelenga kuchochea na kutoa hamasa kwa wadau wa elimu ndani na nje ya Tanzania kuwajibika kwa pamoja kushirikiana na serikali katika kuboresha na kuwezesha utoaji wa elimu bora katika kufikia malengo ya maendeleo endelevuifikapo 2030. 

"...Mkutano huu wa kimataifa utarajia kuwa na wadau mbali mbali ndani na nje ya Tanzania wakiwemo; Wawakilishi wa mabunge ya Afrika,Wadau wa Maendeleo, Wanazuoni, Bodi za mikopo za elimu ya juu, Vyama vya walimu, Sekta binafisi, Sekta za mawasiliano, Wizara ya Elimu Sayansi na Tekinolojia (MoEST), TAMISEMI, Vyuo vya Ufundi, Wazazi, Wanafunzi nk," alisisitiza Bw. Wayoga.

Aliongeza kuwa mtandao wa TEN/MET unapenda kutoa rai kwa wadau wa elimu ndani na nje ya nchi, kushiriki katika mkutano huo wa kimataifa ili kuweza kujifunza njia na mbinu mbalimbali zinazoweza kutumika katika kuendelea na kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia. 

Hata hivyo, Bw. Wayoga aliongeza kuwa mkutano huo utaendeshwa katika mfumo wa mijadala, ambapo mada mbalimbali zinazohusiana na elimu zitajadiliwa ili kutoa fursa kwa wadau kujadiliana zaidi. Na kutakuwa na uwasilishaji wa tafiti za kielimu wenye lengo la kuufahamisha umma hali na mwenendo wa elimu ya Tanzania kuanzia ngazi ya elimu ya awali, elimu ya msingi, sekondari hadi chuo kikuu. 

Kwa miaka kumi na moja sasa, TEN/MET imekuwa ikiandaa mkutano wa kutathimini na kujadili utolewaji wa elimu ubora nchini Tanzania. Katika mkutano huu, TEN/MET imekuwa ikiwashirikisha wadau mbalimbali wa elimu katikakufanya tathmini nakujadili changamoto katika utolewaji wa elimu bora nchini na kwa pamoja kuazimia mapendekezo ya nini kifanyike katika kutatua changamoto zinazoathiri utoaji wa elimu bora. Ama kwa hakika mkutano huu umekuwa ukileta tunu katika sekta ya elimu na kwa wadau wa elimu kwa ujumla. 

"...Tunapenda kutoa wito na kuwakaribisha wadau mbali mbali wa elimu kuungana nasi kwa kushiriki katika mkutano huu wa kimataifa utakaojadili taswira ya elimu Tanzania," alibainisha Mratibu wa TEN/MET, Bw. Wayoga kwa wanahabari alizungumzia mkutano huo

 

DAYANA VIVIAN MABULA ALIVYOMEREREMETA KATIKA SEND OFF MWANZA


Dayana Vivian Mabula mtoto wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula akipunga mikono kuwaaga waalikwa wakati akitoka katika sherehe yake ya Send Off iliyofanyika katika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza tarehe 30 Januari 2020.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula akimkabidhi Hati ya Kiwanja mtoto wake Dayana Vivian Mabula na kumtaka kuhakikisha analipa kodi ya pango la ardhi ili kuepuka tozo ya adhabu wakati wa sherehe yake ya Send Off iliyofanyika kwenye ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza tarehe 30 Januari 2021. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake (UWT) Mwalimu  Queen Mlozi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akizungumza kabla ya kumkabidhi zawadi Dayana Vivian Mabula ambaye ni mtoto wa Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula katika sherehe ya Send Off iliyofanyika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza tarehe 30 Januari 2021.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akizungumza kabla ya kumkabidhi zawadi Dayana Vivian Mabula ambaye ni mtoto wa Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula katika sherehe ya Send Off iliyofanyika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza tarehe 30 Januari 2021.
Waandishi wa Habari wa mkoa wa Mwanza wakimtunza zawadi Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula kutokana ushirikiano anaouonesha kwao wakati wa sherehe ya Send Off ya mtoto wake Dayana Vivian Mabula iliyofanyika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza tarehe 30 Januari 2021.(PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA WIZARA YA ARDHI) 
Dayana Vivian Mabula mtoto wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula akimkabidhi zawadi mumewe mtarajiwa wakati wa sherehe ya Send Off iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza tarehe 30 Januari 2021.
 
Dayana Vivian Mabula mtoto wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula (Kulia) akimkabidhi zawadi ya picha mama yake mzazi wakati wa sherehe yake ya Send Off iliyofanyika katika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza tarehe 30 Januari 2020.

WILAYA ITAKAYOKUMBWA NA NJAA DC ATAONDOKA: MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Manyoni mjini mkoani Singida wakati akiondoka mara baada ya kuwahutubia leo tarehe 31 Januari 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Manyoni mjini mkoani Singida wakati akiondoka mara baada ya kuwahutubia leo tarehe 31 Januari 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na watoto mara baada ya kuwahutubia wananchi wa Manyoni mjini mkoani Singida Januari 31, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na watoto mara baada ya kuwahutubia wananchi wa Manyoni mjini mkoani Singida Januari 31, 2021.(Picha na IKULU).

NA MWANDISHI MAALUM.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewahimiza wananchi kufanya kazi kwa bidii kwani kuba kila dalili ya uwepo wa uhaba wa chakula Duniani kwa vile mataifa mengi wamejidu gia (lockdown).

"Mataifa mengi hawafanyi kazi kwa sababu wamejifungia, wana lockdown, tuutumie muda huu sisi kufanya kazi, sintatoa chakula kwenye Wilaya itakayokumbwa na njaa na Wilaya itakayokuwa na njaa Mkuu wa Wilaya atao doka na huo ndio ukweli," Alisema RAIS WILAYANI Bahi wakati akiwa njiani kuelekea jijini Dodoma akitokea mkoani Tabora leo Januari 31, 2021.


 

Saturday, January 30, 2021

NAIBU WAZIRI MABULA AWABANA WATENDAJI SEKTA YA ARDHI KUONGEZA KASI UTOAJI HATI

 

Na Munir Shemweta,

WANMM, MARA

 

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka Watendaji wote wa sekta ya ardhi katika halmashauri kushiriki zoezi la kuandaa hati za ardhi ili kuongeza kasi ya utoaji hati katika maeneo mbalimbali nchini.

 

Dkt Mabula ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki alipozungumza na wataalamu wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Mara akiwa katika ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya Serikali kupitia kodi ya pango la ardhi katika mkoa huo.

 

Alisema, baadhi ya halmashauri nchini zimekuwa na kasi ndogo ya uandaaji hati za ardhi kwa kisingizio cha kuwa na wataalamu wachache wa kuandaa hati wakati halmashauri hizo zina wataalamu mbalimbali wa sekta hiyo na kutolea mfano wataalamu wa Mipango Miji, Warasimu Ramani, Wapimaji na  Wathamani aliowaeleza wamekuwa wakisoma chuo kinachotoa taaluma ya sekta ya ardhi.

 

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliongeza kwa kusema kuwa, iwapo watendaji wa sekta ya ardhi watafanya kazi kwa ushirikiano na kupeana malengo ya kuandaa Hati basi kasi ya utoaji hati itaongezeka na hivyo kuifanya wizara kuongeza makusanyo ya   maduhuli ya serikali kupitia kodi ya pango la ardhi.

 

"Ninyi nyote mmesoma katika chuo cha aina moja na mnazifahamu kazi za sekta ya ardhi  mnaweza kupeana malengo na kila mmoja akashiriki kuandaa Hati na inapofika hatua ya kukamilisha ndiyo apewe Afisa Ardhi Mteule ili kukamilisha" alisema Dkt Mabula

 

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, kama watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri hawatakuwa wabunifu na kufanya kazi kwa kujiwekea malengo kasi ya utoaji hati itakuwa ndogo na utaifanya wizara kutofikia malengo yake ikiwemo ya makusanyo ya kodi ya pango la ardhi ambayo kwa mwaka 2020/2021 ni bilioni 200.

 

Naibu Waziri Dkt. Mabula alieleza kupitia kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa wa Mara kuwa, wakati Serikali ikifikia nusu mwaka wa fedha 2020/2021 makusanyo ya kodi ya ardhi katika halmashauri nyingi yako chini ya asilimia 50 jambo alilolieleza kuwa linatia shaka kama halmashauri hizo zitaweza kutimiza malengo katika muda uliosalia.

 

Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Mabula aliwaambia watendaji hao wa sekta ya ardhi kuwa,  katika robo ya mwaka wa fedha 2020/2021 anataka kuona halmashauri zote zinaongeza kasi ya makusanyo kwa kuhakikisha zinawabana wadaiwa sugu ili kulipa malimbikizo ya kodi ya ardhi na na wale wadaiwa watakaokaidi kulipa basi wafikishwe kwenye Mabaraza ya Ardhi ya Nyumba na Wilaya kwa hatua zaidi.

 

Aliwaeleza wataalam hao wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Mara kuwa, kwa mujibu wa kifungu Na 48(1) (g) cha sheria ya ardhi, Afisa Ardhi anayo mamlaka ya kufuta umiliki wa ardhi kwa mmiliki aliyekaidi kulipa kodi ya pango la ardhi katika kipindi cha miezi sita baada ya kutumiwa ilani ya madai.  

 

Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa Mara Jerome Kiwia alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula kuwa, mkoa huo hadi sasa  umeweza kukusanya takriban milioni 890.3 za kodi ya pango la ardhi na kubainisha kuwa, ofisi ya Ardhi katika mkoa huo imejiwekea mikakati  ya kuhakikisha kasi ya makusanyo inaongezeka ikiwemo kusambaza ilani za madai kwa wadaiwa sugu na kutumia vyombo vya habari kuhamasisha ulipaji kodi ya pango la ardhi. Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Kulia) akisalimiana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Walemavu) Ummy Nderiananga walipokutana ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mara mwishoni mwa wiki alipokuwa katika ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na kuhamasisha ulipaji kodi ya pango la ardhi katika mkoa huo. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi Hati ya Ardhi mmoja wa wakazi wa Musoma mkoa wa Mara alipokuwa katika ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na kuhamasisha ulipaji kodi ya pango la ardhi katika mkoa huo mwishoni mwa wiki.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na Watendaji wa Sekta ya Ardhi katika mkoa wa Mara mwishoni mwa wiki alipokuwa katika ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na kuhamasisha ulipaji kodi ya pango la ardhi katika mkoa huo.
Sehemu ya Watendaji wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Mara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (hayupo pichani) mwishoni mwa wiki wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na kuhamasisha ulipaji kodi ya pango la ardhi katika mkoa huo.

URASIMISHAJI WAWEZESHA WANANCHI NJOMVE KUKOPA TZS BILIONI 3.1


Na Mwandishi  Wetu- Njombe

WAFANYABIASHARA na wakulima waliorasimisha biashara, ardhi na makazi yao katika Halamashauri ya Mji wa Njombe, wametumia hati za hakimili za kimila kukopa zaidi ya Shilingi bilioni 3.1 katika taasisi za fedha zikiwemo benki za NBC, CRDB, NMB na Benki ya Posta kati ya mwaka 2018 na 2020.

Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kutembea wanufaika wa Mpango huo leo Januari 29, 2021, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Balozi (Mstaafu) Daniel Ole Njoolay, amesema Halmashauri ya Mji wa Njombe ni mfano bora wa kuigwa na halmashauri nyingine kwa namna ilivyotekeleza kikamilifu dhana ya urasimishaji hali iliyowawezesha wananchi kupata mikopo katika taasisi za fedha baada ya urasimishaji tasilimali zao na kupata hati za hakimiliki za kimila.

“Viwanja zaidi ya elfu 10 vimepimwa hapa katika Mji wa Njombe na hii ni ishara kuwa urasimishaji umekuwa na matokeo chanya, hivyo nawapongeza wananchi na viongozi wa Njombe kwa kutumia fursa hii iliyoletwa na MKURABITA,” alisema Njoolay.

Amesema kila halmashauri ina jukumu la kutenga bajeti kila mwaka ili kutekeleza dhana ya urasimishaji kwa vitendo hali itakayowawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi kwa kutumia rasilimali zilizopo ikiwemo ardhi na biashara zao.

Mratibu wa MKURABITA, Dkt. Seraphia Mgembe, amesema maafisa biashara kote nchini wanalo jukumu la kuwaelimisha wananchi kuhusu namna bora ya kuendesha biashara zao huku wakitumia huduma za vituo jumuishi vya biashara vilivyopo katika kalmashauri kama Njombe Mji hali itakayokuza biashara zao na kuongeza tija.

“MKURABITA ilijenga uwezo kwa Halmashauri ya Mji Njombe na sasa imeonesha mfano kwa kuendeleza dhana hii ya kuwawezesha wananchi kupitia rasilimali zao ikiwemo ardhi na tayari matokeo chanya yameanza kuonekana kupitia kwa wajasiriamali hapa Njombe nah ii ndiyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano,”alisisitiza Dkt. Mgembe

Mmoja wa wanufaika wa urasimishaji ardhi katika Halmashauri ya Mji wa Njombe Bibi  Lucy Yona Kitavile  anayemiliki kiwanda cha Mama Seki Group Ltd kinachoongeza thamani mahindi kwa kuzalisha unga amesema kuwa baada ya urasimishaji ardhi alianza kukopa shilingi laki 4 hadi sasa ameweza kukopa milioni zaidi ya 400 zilizomuwezesha kuanzisha kiwanda hicho mwaka 2019.

“ Kwa siku kiwanda changu kinazalisha unga tani 30 hivyo niwashauri akinamama wote kujituma na kutumia fursa zinazotokana na urasimishaji kujikwamua kiuchumi ikiwemo kuanzisha viwanda vidogo”, alisisitiza Bi. Kitavile

Akieleza zaidi amesema kuwa MKURABITA imewezesha wananchi waliorasimisha biashara na mashamba yao kujikwamua kiuchumi baada ya kupata mikopo katika Taasisi za fedha.

Halmashuri ya Mji wa Njombe ni moja ya Halmashauri zilizonufaika na mpango wa urasimishaji wa biashara,makazi na ardhi hapa nchini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA), Mhe. Balozi (Mstaafu) Daniel Ole Njoolay akieleza faida za urasimishaji kwa wananchi wa halmashauri ya mji wa Njombe walionufaika na mpango huo  Januari 29, 2021 wakati wa ziara ya Kamati hiyo na Menejimenti ya MKURABITA wilayani humo kujionea maendeleo yaliyofikiwa na wanufaika hao.
Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Dkt. Seraphia Mgembe akieleza faida wanazopata wananchi waliorasimisha mashamba yao na kupatiwa hatimilki za kimila za kumiliki ardhi Katika Halmashauri ya Mji wa Njombe mkoani Njombe wakati wa ziara ya Kamati ya Uongozi ya MKURABITA inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Balozi (Mstaafu) Daniel Ole Njoolay.
PIX6Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) wakiwa kwenye Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Njombe wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Halmashauri hiyo.
PIX7. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bibi Illuminatha Mwenda akisisitiza jambo kwa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA ) wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Halmashauri hiyo.
(Picha zote na MAELEZO)


Wananchi walionufaika na urasimishaji ardhi, biashara na makazi katika Halmashauri ya Mji wa Njombe mkoani Njombe wakifuatilia hotuba ya  Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA, Mhe. Balozi (Mstaafu) Daniel Ole Njoolay wakati wa mkutano kati yao na kamati hiyo mjini Njombe kilicholenga kujionea hatua zilizofikiwa baada ya urasimishaji.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Bibi Immaculata  Senje akieleza jambo kwa wananchi walionufaika na MKURABITA kupitia urasimishaji ardhi, biashara na makazi katika Halmashauri ya Mji wa Njombe mkoani Njombe wakati wa ziara ya  Kamati hiyo.
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Bw. Mujungu Masenene akieleza jambo wakati wa mkutano kati ya Kamati ya Uongozi ya MKURABITA na wanufaika wa urasimishaji ardhi, makazi na biashara katika Halmashauri ya Mji wa Njombe mkoani Njombe wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Halmashauri hiyo  .
WAZIRI MHAGAMA AZINDUA MPANGO KAZI WA KUSIKILIZA NA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA WADAU KATIKA SEKTA YA KAZI NA AJIRA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.  Jenista Mhagama akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa Kusikiliza na Kushughulikia Malalamiko ya Wadau katika sekta ya kazi na ajira uliofanyika ukumbi wa mikutano wa NSSF mkoani Morogoro Januari 29, 2021, kulia kwake ni rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, Tumaini Nyamhokya, kushoto kwake ni Mwakilishi wa ILO Bw. Maridadi Phanuel, wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Loata Sanare, wa pili kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Bw. Andrew Massawe na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Dkt. Aggrey Mlimuka.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.  Jenista Mhagama akihutubia wakati wa uzinduzi wa Mpango Kazi wa Kusikiliza na Kushughulikia Malalamiko ya Wadau katika sekta ya kazi na ajira uliofanyika mkoani Morogoro, Januari 29, 2021.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.  Jenista Mhagama akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, wakati wa hafla ya uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loata Sanare akitoa salamu za mkoa wake wakati wa uzinduzi huo.
Bw.Tumaini Nyamhokya rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi akizungumza masuala ya vyama vya wafanyakazi wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri (ATE) Dkt. Aggrey Mlimuka akitoa salamu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa Kusikiliza na Kushughulikia Malalamiko ya Wadau katika sekta ya kazi na ajira.
Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) Bw. Maridadi Phanuel akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda akieleza masuala ya Afya na Usalama Mahala Pa Kazi wakati wa uzinduzi wa Mpango huo.
Kamishna wa Kazi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Brigedia Jenerali Francis Mbindi akichangia jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa Kusikiliza na Kushughulikia Malalamiko ya Wadau katika sekta ya kazi na ajira.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Masha Mshomba akichangia jambo wakati wa hafla hiyo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.  Jenista Mhagama akikabidhi Mpango Kazi wa Kusikiliza na Kushughulikia Malalamiko ya Wadau katika sekta ya kazi na ajira kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loata Sanare mara baada ya kuuzindua rasmi mpango huo.

Sehemu ya wadau walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa Kusikiliza na Kushughulikia Malalamiko ya Wadau katika sekta ya kazi na ajira wakifuatilia mkutano huo.

Sehemu ya wadau walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa Mpango Kazi wa Kusikiliza na Kushughulikia Malalamiko ya Wadau katika sekta ya kazi na ajira wakifuatilia mkutano huo.

Mkurugenzi wa uendeshaji kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw. Mbaruku Magawa akichangia jambo wakati wa hafla hiyo.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

 Na.Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Wazri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.  Jenista Mhagama amezindua Mpango Kazi wa Kusikiliza na Kushughulikia Malalamiko ya Wadau na Kikosi Kazi cha kufanya ukaguzi maalum katika sekta ya kazi na ajira wenye lengo la kutatua changamoto wanazokabiliana nazo na kuhakikisha kunakuwa na mazingira rafiki kwa wafanyakazi, waajiri na wadau wengine wanaohudumiwa na Ofisi yake.

Uzinduzi huo umefanyika tarehe 29 Januari, 2021 katika Ukumbi wa Mikutano wa NSSF uliopo Mkoani Morogoro na kuhudhuriwa na viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loate Sanare, Mkurugenzi wa shirika la Kazi Duniani (ILO),Wakuu wa Taasisi zilizochini ya ofisi hiyo ikiwemo;WCF, NSSF, PSSSF, OSHA na CMA, Viongozi wa vyama vya waajiri, pamoja na Watendaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye ulemavu).

Akizungmza wakati wa uzinduzi huo Waziri amesema uwepo wa mpango huo utasaidia Wafanyakazi, Waajiri na Wananchi kufahamu mamlaka sahihi ya kuwasilisha malalamiko yanayohusu sekta ya kazi na ajira, uwepo wa njia nyepesi ya kushughulikia malalamiko na kero za wadau na kuweka utaratibu rahisi wa kutoa ushauri na elimu.

Mpango unalenga pia, kuwepo kwa njia nyepesi ya utoaji wa ushauri na elimu ya Sheria za Kazi, mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Masuala ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi pamoja na kuisaidia Serikali kuwa karibu na Waajiri na Wafanyakazi.

Aidha alibainisha kuwa, uwepo wa mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025, kwani inaelekeza kuwa Chama kitaisimamia Serikali kuhakikisha inazingatia haki na wajibu wa wafanyakazi na waajiri na kuimarisha taasisi za hifadhi ya jamii.

Waziri Mhagama alieleza kuwa kila mdau katika eneo lake aone umuhimu na tija kubwa katika kuhakikisha wanatatua malalamiko ya wafanyakazi na waajiri kwa wakati na kupunguza gharama zisizo za lazima katika utoaji wa huduma.

“Mpango utasaidia katika kupunguza gharama na muda unaotumika na wadau katika kushughulikia na kufutlia malalamiko yao na hii itarahisisha uwepo wa muda wa kutosha katika kuendelea na kazi za kujenga uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja,”Alisisitiza

Alisema kuwa, kupitia Mpango huu, malalamiko na kero za wafanyakazi na waajiri zitapokelewa kila siku ya Ijumaa ya mwisho wa mwezi katika kituo/ofisi katika kila Mkoa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana kisha Idara ya kazi, mifuko ya Hifadhi ya jamii, Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi pamoja na vyama vya wafanyakazi na waajiri vitatoa majibu na kushauri hatua za kuchukua kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.

Sambamba na hilo, Waziri aliwataka Watendaji wa Ofisi yake kuhakikisha Mpango Kazi huo unatekelezwa ipasavyo kwa kuzingatia umuhimu wake.

“Kila Ofisi itekeleze majukumu yake kwa ufanisi ili kuwaondolea wadau wa sekta ya kazi na ajira changamoto ambazo zilikuwa zikiwakabili katika maeneo yao bila kupotea muda na rasilimali fedha kuzunguka nchi nzima kutafuta haki,”alisisitiza Waziri

Waziri alitumia fursa hiyo pia kuzindua rasmi Mpango wa Ukaguzi Maalum nchini ambao utatekelezwa na kikosi kazi maalum ambacho kitakuwa jumuishi katika kuimarisha utekelezaji wa Sheria za Kazi (Labour Law Compliance) na maeneo watakayokagua ni pamoja na  vibali vya kazi vya raia wa kigeni, vibali vya kazi vya Watanzania katika miradi ya kimkakati kwa lengo la kuhakikisha vibali vinatolewa kwa kada au ujuzi ambao ni adimu katika soko la ndani la ajira na tulionao.

“Hatua hii itawezesha kulinda ajira za Watanzania na kurithisha ujuzi walionao raia wa kigeni kwa wazawa na kuhakikisha mapato ya kodi yanapatikana,”alieleza

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) Bw. Maridadi Phanuel aliipongeza Serikali kuona haja ya kuwa na mpango huo na kuahidi kuendelea kuunga mkono jitihada hizo kwa kuzingatia malengo chanya yaliyobeba dhana ya uanzishwaji wake.

Aliongezea kuwa, ILO itaendelea kushirikiana na Serikali na vyama vya waajiri na wafanyakazi kwa kutoa misaada mbalimbali ambayo inasaidia katika mikutano ya Utatu yenye lengo la kutatua changamoto zinazohusu sekta ya kazi na ajira.

“Ni vyema kuwa na mpango huu ambao utasaidiia kuendeleza jitihada za utatuzi wa migogooro mahali pa kazi ili kuendelea na uzalishaji kisha kuleta tija ambayo itachochea uwepo wa maendeleo katika Nyanja mablimbali nchini,”alisema Maridadi

Aliongezea kuwa, ni vyema malalamiko sehemu za kazi yakaendelea kushughulikiwa kwa kuzingatia ni njia bora ya kuwepo kwa mahusiano mazuri ya wafanyakazi na waajiri na ni hatua nzuri yenye nia njema itakayochochea maendeleo ya Taifa kwa ujumla