Posts

Showing posts from November, 2022

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHIMIZA ELIMU YA BIMA BARANI AFRIKA

Image
 “Hapa Tanzania,  Rais wetu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa kipaumbele kwenye suala la kuwezesha jamii kwa kuwainua kiuchumi wanawake na vijana ikiwa ni utekelezaji wa Azimio la Ouagadougou (“Ouagadougou+10”) la Utekelezaji wa Mpango wa Ajira na kutokomeza umaskini ambalo lilipitishwa na Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika Januari 2015 kama Ajenda ya AU ya 2063. “Ni wakati muafaka mifuko yetu ya jamii kusaidiana na Serikali zetu kuondoa umasikini miongoni mwa watu wetu. Nitoe rai kwa washiriki wa mkutano huu muangalie  uwezekano wa kujadili kwa mapana kuhusiana na namna ya mifuko ya hifadhi ya jamii inavyoweza kusaidia kuinua uchumi wa watu wetu na kusaidia kuondoa umaskini hasa kwa wanawake, vijana na wakulima. Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki hao, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba alisema eneo la bima lilishatolewa maelekezo na Rais Samia Suluhu Hassan Aprili 22, 2021 wakati alipohutubia Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani

RAIS SAMIA ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA UDAKTARI WA FALSAFA NA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa Cheti mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa wa Heshima ikiwa ni Shahada ya Udaktari wa Juu katika Humanitia na Sayansi Jamii na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa wa Heshima ikiwa ni Shahada ya Udaktari wa Juu katika Humanitia na Sayansi Jamii na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

SHAHADA YA UDAKTARI WA HESHIMA NI UTHIBITISHO WA KAZI KUBWA ANAZOZIFANYA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa wa Heshima ikiwa ni Shahada ya Udaktari wa Juu katika Humanitia na Sayansi Jamii na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022. (PICHA NA IKULU) NA MWANDISHI MAALUM. Chama Cha Mapinduzi (CCM) tumeguswa na kufurahishwa na uamuzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kumtunuku shahada ya udaktari wa heshima Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mahafali ya 52 duru ya 5 yaliyofanyika leo Jumatano, 30 Novemba, 2022 ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Uamuzi huo ni uthibitisho wa dhahiri wa kazi kubwa na nzuri inayofanywa na serikali ya CCM, awamu ya sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt.

WATOTO 324,968 KUCHANJWA CHANJO YA POLIO AWAMU YA NNE RUKWA

Image
  Na OMM Rukwa Mkoa wa Rukwa umekamilisha maandalizi ya utoaji chanjo ya polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano wapatao 324,968 katika awamu ya nne itakayoanza Desemba mosi mwaka huu. Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Ally Rubeba amewaambia waandishi wa habari leo (Novemba 30,2022) mjini Sumbawanga kuwa mkoa umekamilisha maandalizi yote na uzinduzi utafanyika kijiji cha Kirando Wilaya ya Nkasi ambapo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga atazindua. “Chanjo zinazotolewa zina manufaa kwa jamii kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa wa polio unaosababisha kupooza au ulemavu wa kudumu na hatimaye kifo,” alisema Rubeba. Kwa upande wake Mratibu wa chanjo mkoa wa Rukwa Ndenisia Ulomi alisema uzinduzi wa chanjo awamu ya nne umelenga kufikia asilimia mia moja ya watoto wapatao 324,968 kwenye halmashauri zote. Ndenisia aliongeza kusema serikali kwa kushirikiana na wadau ikiwemo Shirika la Afya Duniani (WHO) na UNICEF inaendesha kampeni ya chanjo ya polio ili kudhibiti kusambaa kwa

MILA, DESTURI ,UKOSEFU WA ELIMU VIMETAJWA KUWA NI SABABU YA KUWEPO KWA VITENDO VYA UKATILI MKOANI SINGIDA

Image
  Mmoja wa Shujaa kutoka Taasisi ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA)  akitolewa damu kwa ajili ya kuchangia akiba ya damu wakati Mashujaa kutoka SMAUJATA  walipotembelea Hospitali ya Makiungu iliyopo wilayani Ikungi kwa ajili ya kutoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili, pamoja na kuwajulia hali wagonjwa ambapo pia walifanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Hospitali hiyo katika ziara iliyofanyika jumamosi. Uchangiaji wa damu ukifanyika. Mashujaa wakifanya usafi kuzunguka viunga mbalimbali vya Hospitali hiyo. Usafi ukiendelea. Mashujaa wa SMAUJATA wakiwafariji wagojwa kwa kufanya maombi pamoja. Sabuni zikitolewa kwa wagonjwa. Picha ya pamoja wakati wa ziara hiyo. Na Dotto Mwaibale , Singida MILA na desturi na ukosefu wa elimu vimetajwa kuwa sababu ya kuwepo kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii kwa watoto ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwepo kwa vitendo vya ukeketaji kwa watoto wadogo. Sababu hizo zimetolewa na wananchi wa Wilaya ya Singida na Iiku

MAJARIBIO YA TRENI KUINGIA NDANI YA BANDARI YA TANGA YAFANYIKA

Image
 ZOEZI la majaribio ya kuingiza treni ndani ya bandari ya Tanga limefanyika kufuatia kikao cha maboresho ya bandari hiyo.  Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Usafirishaji Mhandisi A.Kissaka  amesema mara ya mwisho treni kuingia bandarini Tanga ilikuwa miaka 20 iliyopita, ameongeza kuwa  uwepo za treni hizo utapunguza gharama za usafirishaji kwa mteja.

KAMATI YARIDHIA HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA BoT KATIKA UTEKELEZAJI WA SERA YA FEDHA

Image
  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID KAMATI ya Sera ya Fedha (Monetary Policy Committee) imeridhia   Benki Kuu ya Tanzania (BoT)  iendelee na utekelezaji wa sera ya fedha inayolenga kupunguza ongezeko la ukwasi  katika uchumi kwa mwezi Novemba na Desemba 2022. Tamko hilo la Kamati limetolewa kufuatia kikao chake cha Novemba 28, 2022 ambapo ilifanya tathmini ya utekelezaji wa sera ya fedha na mwenendo wa uchumi na kwa kuzingatia athari za mtikisiko wa uchumi duniani kwenye mfumuko wa bei na shughuli za uchumi. Kwa mujibu wa Taarifa ya Brnki Kuu iliyotolewa kwa vyombo vya Habari Novemba 29, 2022 imesema utekelezaji huu wa sera ya fedha unalenga kuhakikisha kuwa mfumuko wa bei unaendelea kubakia ndani ya lengo na kuwezesha ukuaji wa uchumi nchini. Taarifa kamili inapatikana hapo chini. Gavana wa Benki Kuu, Prof. Florens Luoga (Picha ya Maktaba)

TANZANIA, UNAIDS WAZINDUA RIPOTI YA KIDUNIA HALI YA UGONJWA WA UKIMWI 2022 NCHINI.

Image
Na WAF, DSM Kuelekea katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Desemba 01, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Ukimwi (UNAIDS) pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo wamezindua Ripoti ya Kidunia ya hali ya Ugonjwa wa Ukimwi kwa Mwaka 2022. Hafla ya Uzinduzi wa Ripoti hiyo imeongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Utawala Mheshimwia George Simbachawene, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel Mkurugenzi Mtendaji UNAIDS Bi. Winnie Byanyima pamoja na Watendaji wa Taasisi zinazoshughulika na masuala ya UKIMWI. Ripoti hiyo iliyopewa jina la ‘Dangerous Inequalities’ imebainisha jinsi kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia kunavyopelekea athari katika kufanya maamuzi sahihi kwenye mapambano dhidi ya VVU kwa watoto na watu wazima. “Hali ya kutokuwa na usawa wa kijinsia ina mchango mkubwa katika maambukizi mapya ya VVU, Vijana wadogo hasa wasichana wako katika hatari mara tatu zaidi kupata maambukizi ya VVU dhidi ya ukilinganisha na vi