Posts

Showing posts from April, 2023

NIMERIDHISHWA NA MAANDALIZI KUELEKEA SHEREHE ZA MEI MOSI-MAJALIWA

Image
  MOROGORO WAZIRI MKUU,  Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na Maandalizi kuelekea sherehe za siku ya wafanyakazi duniani zitakazofanyika kesho Mei 1, 2023 kitaifa Mkoani Morogoro katika Uwanja wa Jamhuri. Ameyasema hayo leo Jumapili (Aprili 30, 2023)alipopokea taarifa na kukagua maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe hizo. Mgeni rasmi atakuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza kamati inayoratibu sherehe hizo na kuwataka kuhakikisha wanakamilisha maeneo ambayo yanahitaji maboresho. Awali,  akitoa taarifa ya maandalizi hayo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi Bi. Fatuma Mwasa amesema maandalizi yamekamilika kwa kiasi kikubwa. Kwa upande wake,  Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tumaini Nyamhokya amesema kwa upande wa vyama vya wafanyakazi maandalizi yamekamilika na wanamatarajio kuwa mahudhurio yatakuwa makubwa na sherehe hizo kuwa za mafanikio.  

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAPILI APRILI 30, 2023

Image
 

MKURUGENZI MKUU WA WCF AKUTANA NA WANUFAIKA WA FIDIA

Image
  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MOROGORO Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma (katikati) akisalimiana na Wanufaika wa Fidia inayotolewa na WCF, Bw. Deus Anthony (kulia) na Bw. Ramadhan Juma kwenye kilele cha siku ya kimataifa ya usalama na afya mahali pa kazi katika viwanja vya Tumbaku mjini Morogoro Aprili 28, 2023. Wawili hao wamepata ulemavu wa kudumu baada ya kuumia kwa nyakati tofauti wakati wakitekeleza majukumu ya waajiri wao. Wakati Bw. Deus Anthony ambaye aliumia wakati akishiriki ujenzi wa barabara kati ya Iringa-Igawa alikatika mguu na kufaidika na fao la matibabu kutoka WCF hadi alipopona. “Nilikatika mguu   wa kushoto wakati nikiwa kazini mwaka 2017, WCF wamekuwa na mimi katika matibabu hadi kupona na kasha kunipa mguu w abandia, naweza kutembea bila ya shida yoyote.” Amefafanua , Bw. Anthony. “Nawashukuru WCF kwa kuniwezesha kuyamudu maisha, pensheni ninayolipwa kila mwezi kutokana na ulemavu wangu wa kudumu,  nimekuwa nikidundu

PSSSF YAPEWA TUZO YA UZINGATIAJI SAHIHI WA SERA YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

Image
  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MOROGORO MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetwaa tuzo ya mshindi wa kwanza kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa kuwa na Sera Bora za Usalama na Afya Mahali pa Kazi. (OSH) Tuzo hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi iliyokwenda sanjari na Maonesho ya shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na taasisi za umma na binafsi kwenye viwanja vya Tumbaku mjini Morogoro Ijumaa Aprili 28, 2023 na kupokelewa na Meneja wa PSSSF Kanda ya Mashariki aliyefuatana na Mkurugenzi wa Manunuzi na Ugavi, PSSSF Bw.Ernest Khisombi ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu CPA. Hosea Kashimba. Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi hufanyika Aprili 28 kila mwaka ambapo Tanzania huungana na mataifa mengine duniani kuiadhimisha siku hi

NSSF YANG'ARA MAADHIMISHO SIKU YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI DUNIANI

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako (kulia) akimkabidhi Meneja wa NSSF Mkoa wa Morogoro, Rose Meta (kushoto) tuzo ya ushindi wa jumla kwa Taasisi za Umma zinazotoa Huduma ya Hifadhi ya Jamii katika sekta binafsi. Rose amepokea tuzo hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba  wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi Duniani iliyofanyika kitaifa viwanja vya Tumbaku mjini Morogoro.

PROF. NDALICHAKO: SERIKALI YA AWAMU YA SITA KUENDELEA KUIMARISHA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI

Image
NA MWANDISHI WETU, MOROGORO Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kusimamia masuala ya usalama na afya mahala pa kazi kwa kuwa ni haki ya msingi wa kila mfanyakazi nchini.  Prof. Ndalichako ameyasema hayo leo Aprili 28, 2023 katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahala Pa Kazi kwenye viwanja vya Tumbaku, mkoani Morogoro. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Mazingira salama na yenye afya kazini ni kanuni na haki ya msingi mahali pa kazi.”  Amesema Rais Samia amekuwa kinara katika kuhakikisha nguvu kazi ya Taifa inalindwa kwa kuendelea kuimarisha Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA). Waziri Ndalichako amewataka OSHA kuendelea kutoa elimu kwa waajiri na wafanyakazi kuhusu masuala ya usalama na afya mahali pa kazi na  kuwahamasisha waajiri kuweka mifumo sahihi ya usalama na afya katika maeneo yao ya kazi n

KAMBI YA MATIBABU YA MOYO YAOKOA MIL. 493

Image
Na Salome Majaliwa. Taasisiya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeokoa kiasi cha shilingi milioni 493 ambazo Serikali ingetumia kama wagonjwa 15 wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo wangepelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu hayo. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Dkt. Peter Kisenge alisema katika kambi hiyo maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo iliyofanywa na wataalam wa afya wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Madaktari Afrika la nchini Marekani wameweza kuwafanyia upasuaji wagonjwa ambao walihitaji kurekebishiwa mfumo wa umeme wa moyo kwa ufasaha wa hali ya juu. Dkt. Kisenge alisema pamoja na wataalam hao kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa pia wametoa mafunzo kwa wataalam wa afya wa JKCI hivyo kuendelea kuboresha huduma za matibabu ya mfumo wa umeme wa moyo katika Taasisi hiyo. “Gharama za matibabu za wagonjwa hawa 15 ni shilingi milioni 253 lakini kama wagonjwa hawa wangeenga

MIFUMO YA GePG NA NPMIS KUCHOCHEA MAENDELEO

Image
Wanafunzi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Dodoma (IRDP), wakielekezwa namna ya kutumia mfumo wa GePG kulipa ada, wakati wa maadhimisho ya wiki ya Ubunifu yanayofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma. Mkurugenzi wa Ubunifu na Teknolojia kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Dkt. Gerald Kafuku, akisikiliza maelezo kuhusu Mfumo wa GePG kutoka kwa mtaalamu wa Mfumo huo kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Maendaenda, wakati wa maadhimisho ya wiki ya Ubunifu yanayofanyika kitaifa Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma. Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA), Prof. William Pallangyo, akisikiliza maelezo kuhusu Mfumo wa Kitaifa wa Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo na Programu (NPMIS) kutoka kwa mtaalamu wa Mfumo huo kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Subira Msabaha, wakati wa maadhimisho ya wiki ya Ubunifu yanayofanyika kitaifa Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma. Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pembejeo (AGITF), Bw. Omar Jumanne Bakari, a

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAMOSI APRILI 29, 2023

Image