KAMATI YA BUNGE YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA YATEMBELEA KIWANDA CHA NYAMA CHA NGURU HILLS NA KURIDHISHWA NA UWEKEZAJI WA PSSSF KWENYE MRADI HUO
NA MWANDISHI MAALUM, MOROGORO. KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Jerry Silaa, imeridhishwa na uwekezaji uliofanywa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwenye Mradi wa Uendelezaji wa shamba (Rachi) ya kunenepesha Mifugo na Machinjio ya kisasa wa Nguru Hills Ranch ulioko Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro. Kufuatia kuridhishwa huko Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Jerry Silaa alitoa maagizo matatu kwa Bodi ya Wadhamini ya PSSSF kuhakikisha inaendelea kusimamia mkataba wa uwekezaji katika machinjio hayo ya Nguru Hills kwa kushirikiana na wawekezaji wenza kwa lengo la kuhakikisha uzalishaji unaanza haraka iwezekanavyo na kupata tija iliyokusudiwa. Pia Bodi ya PSSSF imeagizwa kuongeza kipengele kwenye makubaliano ya ubia na wawekezaji wenza kwenye machinjio hayo ya kukiuzia Ngozi kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro Leather Industry Company Limited (KLIC) ambacho PSSSF imewekeza na hivyo kiwanda cha KL