Posts

Showing posts from February, 2024

BIL. 1.5 ZATUMIKA TARIME UJENZI WA SHULE ZA MSINGI NA AWALI

Image
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Deogratius Ndejembi amesema kiasi cha Sh Bilioni 1.512 zimepelekwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara kwa ajili ya Mradi wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji   kwa Shule za   Awali na Msingi Tanzania Bara   BOOST.\n\nMhe Ndejembi ameyasema hayo leo wakati akieleza mafanikio ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwenye ziara ya Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa katika Halmashauri hiyo.\n\nMhe Ndejembi amesema Sh Bilioni 1.08 zilitolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule mbili mpya za msingi, Sh Milioni 325 zikitolewa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 13 mapya pamoja na Sh Milioni 69 ambazo zilitolewa kwa ajili ya madarasa ya mfano elimu ya awali.\n\n“ Fedha hizo siyo kwenye elimu ya msingi tu. Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia mradi wa kuimarisha ubora wa elimu ya sekondari SEQUIP tumeleta fedha Sh Milioni 470 katika Kata ya Sirari kwenye awamu ya kwanza, awamu ya pili Sh Milioni 584 kata ya Manga na Sh Milioni 100 kwa ajili ya nyumba ya wali

HALMASHAURI ZIAJIRI WATUMISHI WA MIKATABA KWA MAPATO YA NDANI

Image
Na. WAF - Lindi Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu   amezitaka Halmashauri ikiwemo ya Wilaya ya Kilwa kuajiri watumishi wa mikataba kwa kutumia mapato ya ndani ili kupunguza changamoto za uhaba wa wataalamu wa Afya katika Wilaya hizo. Waziri Ummy amesema hayo Februari 28, 2024 baada ya kupokea taarifa ya hali ya Afya katika Halmashauri ya Wilaya hiyo iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Lusajo Mwakajoka ambayo inaonyesha hali ya upatikanaji wa huduma za Afya katika Mkoa wa Lindi, upatikanaji wa Vifaa na Vifaa Tiba pamoja na changamoto. “Tutatumia njia kuu Tatu ili kupunguza changamoto za watumishi ikiwa ni pamoja na njia ya vibali vya ajira kutoka Ofisi ya Rais Utumishi, kuajiri watumishi kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri pamoja na   wadau wetu wa maendeleo katika Sekta ya Afya nao wanaajiri ajira za mikataba pamoja.” Amesema Waziri Ummy Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amemshukuru Waziri wa Afya Mhe. Ummy kwa kufanya ziara katika Mkoa   huo

RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA UONGOZI WA KANISA LA KILUTHERI AFRIKA MASHARIKI.

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Makamu Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki (KKAM), Askofu Dk.Philemon Mollel na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha Ikulu Zanzibar tarehe: 28 Februari 2024. Aidha, Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali inatambua mchango unaotolewa na Madhehebu ya Dini zote ikiwemo kuhubiri amani na utulivu   katika kuleta umoja nchini. Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amelipongeza Kanisa hilo kwa utayari wao wa kushirikiana na Serikali katika kutoa huduma za kijamii nchini ikiwemo afya na elimu. Naye Askofu Mollel amempongeza Rais Dk.Mwinyi kwa kuleta mabadiliko ya maendeleo na kuwaunganisha wananchi bila kujali itikadi za chama, kabila na Dini.

NCHI WANACHAMA EAPP ZAKUBALIANA KUIPA MSUKUMO MIRADI YA UMEME

Image
Baraza la Mawaziri wanaohusika na mfumo wa pamoja wa umeme kwa nchi za Mashariki mwa Afrika  (EAPP Council of  Ministers-COM) limekubaliana  kwa pamoja kuwa na usimamizi madhubuti wa miradi mbalimbali ya umeme katika nchi wanachama, ili iweze kukamilika kwa wakati na kuwapatia wananchi nishati ya kutosha. Kukamilika  kwa miradi kutoka vyanzo mbalimbali vya umeme, kutawezesha nchi hizo kusaidiana pale nchi mojawapo inapokuwa na upungufu wa umeme huku msisitizo ukiwekwa kwenye miradi ya usafirishaji umeme.(Transmission lines). Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko tarehe 27 Februari 2024 katika Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri wanaohusika na mfumo wa pamoja wa umeme kwa nchi za  Mashariki mwa Afrika (EAPP Council of  Ministers-COM) ambao unafanyika kwa siku mbili jijini Nairobi, Kenya. “ Baraza hili ni muhimu katika kuhakikisha nchi za Afrika zinaungana kwa ajili ya kuendeleza rasilimali za umeme zilizopo pamoja na kupata umeme wa uha

KUTOKA MAGAZETINI LEO FEBRUARI 28, 2024

Image