RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA UONGOZI WA KANISA LA KILUTHERI AFRIKA MASHARIKI.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Makamu Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki (KKAM), Askofu Dk.Philemon Mollel na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha Ikulu Zanzibar tarehe: 28 Februari 2024.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali inatambua mchango unaotolewa na Madhehebu ya Dini zote ikiwemo kuhubiri amani na utulivu  katika kuleta umoja nchini.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amelipongeza Kanisa hilo kwa utayari wao wa kushirikiana na Serikali katika kutoa huduma za kijamii nchini ikiwemo afya na elimu.

Naye Askofu Mollel amempongeza Rais Dk.Mwinyi kwa kuleta mabadiliko ya maendeleo na kuwaunganisha wananchi bila kujali itikadi za chama, kabila na Dini.









Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"