Asilimia 77.3 ya Vijiji Kagera Vyaunganishwa na Umeme wa REA
Na Lilian Lundo na Veronica Simba Vijiji 512 kati ya Vijiji 662 vya Mkoa wa Kagera ambayo ni sawa na asilimia 77.3 ya vijiji vya mkoa huo vimepata huduma ya umeme kupitia miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ikiwemo Mradi wa REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza, REA Awamu ya Pili na REA Awamu ya Kwanza. Vijiji 150 ambavyo bado havijaunganishwa na umeme mkoani humo, vitaunganishwa na umeme kupitia Mradi wa REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili, ambapo tayari mkandarasi anaendelea na kazi za mradi huo. Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy amesema jumla ya shilingi bilioni 80 imetolewa na Serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya usambazaji wa umeme vijijini mkoani humo. “Kupitia Wakala wa Nishati Vijijini ndani ya Mkoa wa Kagera imewekeza shilingi bilioni 80 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kusambaza umeme vijijini, na hivi ninavyoongea ndani ya mkoa huu kuna miradi mitano inatekelezwa,” amesema Mhandisi Saidy wakati wa hafla wa uwashaji wa umeme Kijiji cha Mub