Posts

Showing posts from October, 2022

TANZANIA TUKO MILIONI 61.7; RAIS SAMIA

Image
Kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu Sura 351 ya 2015, na kwa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025 Ibara 206, na kwa Mamlaka niliyopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ninawatangazia rasmi kuwa Tanzania ina idadi ya watu wapatao 61,741,120 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akinyanyua Kitabu cha Muongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 katika sherehe zilizofanyika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma tarehe 31 Oktoba, 2022. Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Vitabu vya Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 pamoja na Kitabu cha Muongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua Kitabu cha Muongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 katika sherehe zilizofany

WAZIRI UMMY ATEMBELEA DAR ES SALAAM KUANGALIA UTAYARI WA KUIKABILI EBOLA

Image
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Ally Mwalimu ameridhishwa na kiwango cha maandalizi ya utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola endapo utaingia jijini Dar es Salaam. Mhe. Ummy Ameyasema hayo Oktoba 30, 2022 alipotembelea jiji hilo endapo jiji la Dar es Salaam litapata wagonjwa. Hata hivyo alisema bado kuna kazi ya kufanya katika maandalizi na utayari. “Shirika la Afya Duniani WHO limeahidi kuleta nchini Tanzania wataalamu ambao waliwahi kutoa matibabu kwa wagonjwa wa Ebola ikiwamo huko Liberia na kusisitiza hadi sasa Tanzania haina mgonjwa wa Ebola” amesema Waziri Ummy. Alisema "Ebola ni tishio jana Waziri wa Afya wa Uganda ameniambia wamepata wagonjwa wapya 5 inafanya idadi ya waliopata maambukizi hayo tangu mlipuko {Septemba, 2022) kufikia sasa ni jumla ya watu 126." Mhe. Waziri Ummy alibainisha kuwa inatia wasiwasi  baada ya Ugonjwa wa Ebola kufika Jijini Kampala na Entebbe, kuna mwingiliano mkubwa wa shughuli za kiuchumi na kijamii kati Uganda na Tanzania KATIKA mini hiyo.  &q

JIJI LA TANGA LAMWAGA MIKOPO YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 2

Image
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe. Abdulrahman Shiloo akizungumza wakati wa kukabidhi  h undi  kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu kwa ajili ya vikundi vya kiuchumi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu kutoka katika asilimia kumi (10%) ya mapato yake ya ndani kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana  Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana akizungumza wakati wa halfa hiyo  Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shilloo Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Jiji la Tanga Bw. Simon Mdende akizungumza wakati wa halfa hiyo Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe. Abdulrahman Shiloo wa tatu kutoka kushoto akieleza jambo kabla ya kukabiudhi hundi hizo Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe. Abdulrahman Shiloo akikabidhi hundi kwa moja ya vikundi vya wakina mama wajasi

SERIKALI KUFANYA MABORESHO MAKUBWA YA MFUMO WA UNUNUZI

Image
  Na. Peter Haule na Haika Mamuya, WFM, Iringa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande, amesema kuwa Serikali imeweka udhibiti wa mianya ya rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma uliosababishwa na kasoro katika Mfumo wa Ununuzi wa Umma (TANePS) kwa kufanya maboresho makubwa ya mfumo huo. Hayo yamebainishwa mkoani Iringa wakati alipofanya ziara ya kukagua maboresho ya mfumo huo yanayofanywa na wataalamu wa ndani kwa lengo la kuondoa changamoto zilizopo na kukidhi mahitaji halisi ya Serikali na wazabuni. Mhe. Chande alisema kuwa kumekuwa na changamoto ya kupata thamani halisi ya fedha katika huduma na bidhaa kutokana na mianya ya rushwa iliyokuwepo katika mfumo wa manunuzi ambayo inasababisha utofauti mkubwa wa gharama kwenye eneo moja. “Kumekuwa na usiri mkubwa katika michakato ya  ununuzi, hali inayofanya mtu ajiulize huu usiri una nini katikati yake, ununuzi unatakiwa ufanyike kwa uwazi na haki hivyo wataalamu mnaofanya maboresho haya mnaweza kututengenezea mfumo una

BENKI YA CRDB YAZINDUA PROGRAMU YA UWEZESHAJI KWA VIJANA NA WANAWAKE WAJASIRIAMALI KIUCHUMI (IMBEJU)

Image
  Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 50 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela ikiwa ni uwezeshaji kwa biashara bora changa za TEHAMA (digital startups)  kupitia programu ya uwezeshaji kwa vijana na wanawake ya benki hiyo inayofahamika kama "IMBEJU" ambayo imezinduliwa katika Kongamano la Sita la TEHAMA lililofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar Ijumaa iliyopita. Wengine pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib, Iddrisa Kitwana (watatu kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano, na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (wapili kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano, na Teknolojia ya Habari, Mohammed Abdull (wakwanza kushoto),Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya TEHAMA, Prof. Leornad Mselle (wapili kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga. Picha zote na Othman Michuzi. =======  =======  ======= Ikiende

WAZIRI MKUU MAJALIWA AREJEA NCHINI

Image
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri (Kushoto) wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Oktoba 30, 2022. Mheshimiwa Majaliwa amerejea nchini leo akitoka Korea baada ya kukamilisha ziara yake ya kikazi nchini humo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATATU OKTOBA 31, 2022

Image