TANZANIA TUKO MILIONI 61.7; RAIS SAMIA
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema idadi ya Watu
nchini imefikia Milioini 61,741,120.
Rais
ametangaza hayo Oktoba 31, 2022 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma wakati akitoa
matokeo ya mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika Nchi nzima Agosti 23,
2022.
Mhe.
Rais Samia amesema matokeo hayo yanaifanya Tanzania bara kuwa na Idadi ya Watu
Milioni 59,851,357, wakati Zanzibar ina
watu Milioni 1,889,773.
Matokeo hayo yanaonyesha Wanawake ni wengi kuliko wanaume na wanafanya idadi yao kuwa Milioni 31,687,990 sawa na asilimia 51% huku Wanaume wakiwa Milioni 30,053,130 sawa na asilimia 49%.
Aidha kwa upande wa majengo, Tanzania kuna jumla ya Majengo Milioni 14,348,373. Tanzania Bara Ina majengo Milioni 13,907,951, huku Tanzania Zanzibar Kuna majengo Milioni 440,420.
Sensa
ya Watu na Makazi ni zoezi la kitaifa linalofanyika kila baada ya miaka 10
ambapo Sensa ya mwisho kufanyika nchini ni ile ya mwaka 2012 ambapo Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ilikuwa na idadi ya watu Milioni 44,929,002.
Hivyo
Sensa ya mwaka 2022 ilikuwa ni sensa ya Sita (6) kufanyika nchini baada ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964. Sensa nyingine zilifanyika mwaka
1967, 1978, 1988, 2002 na 2012.
Umuhimu
wa kipekee wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ni pamoja na pamoja na
kuisadia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa
utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na
jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa;
Taarifa
za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa
mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na
kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali.
Taarifa
za msingi za hali ya kidemografia, kijamii na kiuchumi za idadi ya watu na
makazi za mipango katika ngazi zote;
Kigawio
katika kukokotoa viashiria vingine mfano Pato la mtu mmoja mmoja, Pato la
Taifa, Ajira na ukosefu wa Ajira na kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi;
Taarifa
itakayowezesha serikali kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na
viashiria vingine, ambavyo ni muhimu kwa usimamizi wa mazingira na Msingi wa
utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia.
Comments
Post a Comment