12/31/2020

RAIS MAGUFULI AWASILISHA FOMU YAKE TUME YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 31 Desemba, 2020 amewasilisha fomu zake za maadili katika ofisi ya makao makuu ya Sekratarieti ya Maadili ya viongozi Jijini Dodoma.

Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike (pichani chini). amekabidhi fomu hizo kwa Kamishna wa Maadili, Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi.


Leo ni siku ya mwisho ya kuwasilisha fomu za maadili kwa viongozi wote kwa mujibu wa Sheria namba 13 ya mwaka 1995 ya Maadili ya Viongozi wa Umma.




    

ZIARA YA NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU AKITEMBELEA MIRADI YA UZALISHAJIMALI YA WATU WENYE ULEMAVU JIJINI DAR ES SALAAM

Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara wenye Ulemavu (UWAWADA) akieleza jambo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (wa pili kutoka kushoto) alipofanya ziara katika eneo la Machinga Complex ya kutembelea vikundi vya watu wenye ulemavu ambavyo vinajihusisha za shughuli za uzalishajimali.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (wa pili kutoka kushoto) akizungumza na Ndg. Galus Buriani (aliyekaa wenye ulemavu) wakati wa ziara yake ya kutembelea vikundi vya watu wenye ulemavu ambavyo vinajihusisha za shughuli za uzalishajimali na kuona namna walivyonufaika na mikopo inayotolewa na serikali kupitia halmashauri 10% (Wanawake 4%, Vijana 4% na Watu wenye Ulemavu 2%).
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga (kulia)akimsikiliza Meneja Karakana ya Disabled Aid & General Engineering (DAGE), Ndg. Henry Chacha (katikati wenye ulemavu) wakati wa ziara yake ya kutembelea vikundi vya watu wenye ulemavu ambavyo vinajihusisha za shughuli za uzalishajimali kupitia uwezeshaji wa mikopo inayotolewa na serikali kupitia halmashauri.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga akisaini kitabu cha wageni alipotembelea kikundi cha watu wenye ulemavu cha Disabled Aid & General Engineering (DAGE) kinachojishughulisha na ufundi vyuma katika eneo la SIDO jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa kikundi cha watu wenye ulemavu cha Disabled Aid & General Engineering (DAGE) Bw. Patrick Mdachi.
Muonekano wa Baiskeli ya Matairi Matatu inayotengenezwa na kikundi cha watu wenye ulemavu cha Disabled Aid & General Engineering (DAGE) kilichopo SIDO, Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (kulia) akimsikiliza Katibu wa Kikundi cha Disabled Living Art Group kinachojishughulisha na uzalishaji wa viatu vya Ngozi katika eneo la Machinga Complex alipotembea vikundi hivyo kuona namna walivyonufaika na mikopo inayotolewa na serikali kupita halmashauri 10% (Wanawake 4%, Vijana 4% na Watu wenye Ulemavu 2%).
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (wa pili kutoka kushoto) akijaribu makobasi “Sandals” alipotembelea Kikundi cha Disabled Living Art Group kinachojishughulisha na uzalishaji wa viatu vya Ngozi katika eneo la Machinga Complex, Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara wenye Ulemavu (UWAWADA) akieleza jambo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (wa pili kutoka kushoto) alipofanya ziara katika eneo la Machinga Complex ya kutembelea vikundi vya watu wenye ulemavu ambavyo vinajihusisha za shughuli za uzalishajimali.
 

    

WANAVYUO JIAMININI ELEZENI VITENDO VYA UKATILI NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA UNAOTOKEA MAENEO YENU.


Mkuu wa dawati la jinsia na watoto mkoa wa Arusha mrakibu msaidizi wa Polisi (ASP) Happiness Temu akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha ufundi Arusha kuhusiana na ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na uhalifu unaohusisha makosa ya mitandao katika kikao kilichofanyika katika bwalo la chuo hicho Jijini la Arusha.
Mlezi wa wanafunzi Bi. Stella Ngowa (aliyekaa katikati), Rais wa serikali ya wanafunzi katika chuo cha ufundi Arusha (aliyevaa koti jeusi) Bwana Issa Mohamed wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa katika kikao kilichojadili masuala ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na uhalifu unaohusisha makosa ya mitandao kilichofanyika katika bwalo la chuo hicho mapema leo Jijini Arusha.
Mmoja wa mshiriki akichangia mada katika kikao kilichojadili masuala ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na uhalifu unaohusisha makosa ya mitandao kilichofanyika katika bwalo la chuo cha ufundi Arusha  Jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinatolewa katika kikao kilichojadili masuala ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na uhalifu unaohusisha makosa ya mitandao kilichofanyika katika bwalo la chuo hicho  Jijini Arusha.

Na Vero Ignatus Arusha

Wanafunzi wa vyuo vikuu na vya kati wametakiwa kuwa na uwezo wa kujileza na kujiamini kueleza na kubainisha vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia vinavyotokea katika maeneo yao .

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa dawati la Jinsia na watoto mkoa wa Arusha Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Happiness Temu wakati akitoa elimu kwa wanafunzi wa chuo cha ufundi Arusha kuhusiana na masuala ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na uhalifu unaohusisha makosa ya mitandao katika kikao kilichofanyika katika bwalo la chuo hicho.

Alisema kuwa ngazi ya chuo ni sehemu muhimu yenye jamii kubwa ya wanafunzi ambao wametoka maeneo mbalimbali na kukutana ndani ya chuo wakiwa na tabia tofauti, hivyo kutokana na tabia hizo vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa  wanafunzi wamekuwa na aibu kuvieleza.

‘‘Wapo baadhi ya wanafunzi wanawafanyia wenzao vitendo vya kikatili na wanaona ni mambo ya kawaida na wale wanaofanyiwa ukatili wanaumia lakini kwa hofu wanaogopa kusema au  hawaelewi ni wapi wanaweza kupeleka malalamiko yao, tunawaasa wawe na uwezo wa kujieleza kwa sababu kuwa na jamii ya wasomi ambao ni waoga wa kujieleza kuhusiana na vitendo vya ukatili ama kuona aibu ni vibaya, hivyo tumefika hapa ili kuwajengea uelewa na uwezo ili waweze kutoka na kukemea vitendo hivyo kwenye jamii’’.  Alisema Mkuu huyo wa dawati la jinsia.

Aidha alisema ili kuweza kuisaidia jamii, ni wakati sasa wa kutengeneza watu ambao watatoka vyuoni wakiwa bora na wasiopenda masuala ya ukatili na wenye uwezo wa kukemea, hivyo waliona ni vyema elimu hiyo waitoe katika maeneo ya vyuo.

Naye rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho Bwana Issa Suleiman Mohamed kwa niaba ya wanafunzi  wa chuo hicho alitoa shukrani kwa jeshi la polisi mkoa wa Arusha kupitia kitengo cha dawati la jinsia na watoto kwa elimu  waliyoitoa kuhusiana na masuala ya ukatili na uhalifu unaotokana na matumizi mabaya ya mitandao.

Alisema elimu hiyo imekuja katika muda muafaka kwakuwa asilimia kubwa ya wanafunzi wanatumia mitandao na hawana uwelewa kuhusu uhalifu wa kimtandao pamoja na masuala ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia ambapo watahakikisha elimu hiyo inawafikia wanafunzi wote chuoni hapo.

‘‘Kama wanafunzi tutaangalia ni namna gani tunahamasishana ili kujiepusha na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na matumizi mabaya ya mitandao ambayo inaweza kutupelekea katika makosa ya uhalifu wa mitandao’’. Alisema  Issa

Aliendelea kusisitiza kwa kuwa wanafunzi wanatoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi, anaimani elimu waliyoipata itasambaa maeneo yote kwani watakuwa mabalozi wazuri wa kuieleza jamii kuepukana na makosa hayo.

Huo ni mwendelezo wa elimu ambazo dawati hilo la jinsia na watoto mkoa wa Arusha linatoa katika maeneo mbalimbali ikiwemo mashuleni, vyuoni na maeneo mengine yenye mikusanyiko ya watu kwa lengo la kuhakikisha jamii inapata uelewa kuhusiana vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.
    

12/30/2020

DKT. NDUGULILE AZIPA SIKU 30 TAASISI ZA UMMA ZINAZODAIWA NA TTCL KULIPA MADENI

Na Prisca Ulomi, WMTH

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amezipa siku 30 taasisi za umma zinazodaiwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kulipa madeni kwa Shirika hilo ili liweze kujiendesha, kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma ya mawasiliano ya sauti na data kwa taasisi za Serikali, sekta binafsi na wananchi ili kukuza uchumi na kuchangia pato la taifa.

Dkt. Ndugulile ameyasema hayo wakati wa ziara yake alipotembelea TTCL kwa lengo la kufahamiana na kuzungumza na wajumbe wa Bodi, Menejimenti na wafanyakazi wa TTCL, Dar es Salaam ambapo aliambatana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo A. Mathew na Mejimenti ya Wizara hiyo

Ameongeza kuwa zaidi ya taasisi 20 za Serikali zinadaiwa na TTCL zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 30 ambapo zipo taasisi zinatumia huduma za mawasiliano za TTCL na zinakusanya mapato ya zaidi ya shilingi bilioni moja kwa mwezi ila hawako tayari kulipa huduma za TTCL

Vile vile, ametoa onyo kali kwa kampuni zinazohujumu miundombinu ya TTCL ili ishindwe kutoa huduma za mawasiliano kwa wateja wake kuwa waache tabia hiyo mara moja na wafanye biashara kwa misingi ya ushindani, vinginevyo Serikali itawachukulia hatua kali 

Aidha, amesisitiza kuwa kwa watakaoiba nyaya za shaba za TTCL na kuuza kama chuma chakavu nao waache mara moja kwa kuwa watahusishwa na uhujumu uchumi kwa kudhoofisha utendaji kazi wa TTCL na kwa watakaobainika watachukuliwa hatua kali na Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama

Amewataka watendaji wa Wizara kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kufanya utafiti na tathmini ya kubaini mchango wa Sekta hii aidha wa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja katika kukuza uchumi na kuchangia pato la taifa kwa kuwa taasisi za Serikali, sekta binafsi na wanachi wanatumia huduma za mawasiliano ya data na sauti na kuendesha shughuli mbali mbali za kiuchumi na kijamii kwa kutumia TEHAMA

Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo A. Mathew amewataka watumishi wa TTCL kuwa wabunifu na kuacha kufanya kazi kwa mazoea na wajenge utaratibu wa kufuata na kuwahudumia wateja huko waliko badala ya kusubiri wateja kuwafuata ofisini

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba amesema kuwa amepokea maelekezo ya Waziri, Dkt. Ndugulile na ametoa rai kwa watumishi wote wa TTCL kujituma ili kuongeza upatikanaji wa huduma ya mawasiliano yenye kasi ya brodibandi kutoka asilimia 49 mwaka 2020 hadi kufikia asilimia 80 mwaka 2025 .

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo A. Mathew akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Faustine Ndugulile (anayesikiliza) alipotembelea Shirika hilo, Dar es Salaam. 

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Waziri Kindamba kuhusu mtambo wa zamani wa kupiga simu kwenye chumba cha makumbusho cha Shirika hilo wakati wa ziara yake ya kutembelea Shirika hilo, Dar es Salaam.

Mhandisi wa Mtandao wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Amina Daudi akitoa maoni yake kwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt.Faustine Ndugulile (hayupo pichani) wakati wa kikao na wafanyakazi alipotembelea Shirika hilo, Dar es Salaam 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Waziri Kindamba akifafanua jambo kwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa kwanza kulia) kuhusu mitambo ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano wakati wa ziara yake kwenye Shirika hilo, Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo A. Mathew
Mkurugenzi Msaidizi wa Miundombinu ya TEHAMA wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Nikusubila Maiko akifafanua jambo kwa Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kulia) wakati akikagua mitambo ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano wakati wa ziara yake kwenye Shirika hilo, Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo A. Mathew

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Waziri Kindamba akiambatana na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) na Naibu Waziri wake, Mhandisi Kundo A. Mathew (wa kwanza kulia) wakati wa ziara yake ya kutembelea Shirika hilo, Dar es salaam

    

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK HUSSEIN ALI MWINYI AWATUNUKU SHAHADA WAHITI WA SUZA LEO D

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ametawazwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Ndg. Mwita Mgeni Mwita na (kulia kwa Rais) Makamu Mkuu wa Chuo Dkt.Zakia Mohamed Abubakar, hafla hiyo imefanyika wakati wa Mahafali ya 16 ya SUZA yaliofanyika katika ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja leo30/12/2020.(Picha na Ikulu)
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais Mstaaf Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee na Naibu Spika Mhe Mgeni Hassan Juma, wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika hafla ya Mahafali ya 16 ya SUZA yalifanyika leo 30-12-2020, katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akihutubia wakati wa hafla ya Mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja leo 30-12-2020.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akihutubia wakati wa hafla ya Mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja leo 30-12-2020.
WAHITIMU wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) wakishangilia wakati Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwahutubia katika hafla ya Mahafali ya 16 ya SUZA  yaliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu.
WAHITIMU wa Shahada ya Utabibu wakila kiapo cha Uaminifu baada ya kutunukiwa Shahada yao na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) katika mahafali ya 16 ya SUZA  yaliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi, akimtunuku Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa Katika Sayansi za Tiba Rais Mstaaf wa Zanzibar Awamu ya Saba Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, katika Mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) yaliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu leo 30-12-2020.(Picha na Ikulu)



 

    

CHAMURIHO AKAGUA VIGWAZA

Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya sehemu ya mzani katika mradi wa Kituo cha pamoja cha Ukaguzi (OSBP), Vigwaza Mkoani Pwani.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi, Dkt. Leonard Chamuriho, akimsikiliza Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Pwani Mhandisi Wilicis Mwageni, wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi wa Kituo cha pamoja cha Ukaguzi (OSBP), alipokagua mradi huo mkoani Pwani.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Pwani, Mhandisi Wilicis Mwageni, alipokuwa akikagua maendeleo ya mradi wa Kituo cha pamoja cha Ukaguzi (OSBP), Mkoani Pwani .
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi  Dkt.Leonard Chamuriho, akifafanua jambo kwa Wahandisi alipotembelea na kukagua mradi wa Kituo cha pamoja cha Ukaguzi (OSBP), mkoani Pwani,  ambao kwa sasa umefikia asilimia 90.