Posts

Showing posts from August, 2022

RAIS WA ZAMANI WA URUSI MIKHAIL GORBACHEV AFARIKI DUNIA

Image
 RAIS wa mwisho wa uliokuwa Muungano wa Kisovyeti (Soviet Union) au USSR, Mikhail Sergeyevich Gorbachev amefariki dunia leo Agosti 31, 2022 akiwa na umri wa miaka 91. Vyombo vya habari vya kimataifa vimeripoti kuwa Gorbachev amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu. Mikhail Gorbachev alikuwa mmoja wa watu mashuhuri katika siasa kwenye karne ya 20. Aliongoza kuvunjwa kwa Muungano wa Kisovyeti ambao ulikuwepo kwa karibu miaka 70 na ulikuwa umetawala sehemu kubwa za Asia na Ulaya Mashariki. Hata hivyo, alipoanzisha mpango wake wa mageuzi mwaka 1985, nia yake pekee ilikuwa ni kufufua uchumi wa nchi yake uliodumaa na kurekebisha michakato yake ya kisiasa. Juhudi zake zikawa kichocheo cha mfululizo wa matukio ambayo yalileta mwisho wa utawala wa kikomunisti, sio tu ndani ya USSR, lakini pia katika mataifa mengine. Mikhail Sergeyevich Gorbachev alizaliwa tarehe 2 Machi 1931 katika mkoa wa Stavropol kusini mwa Urusi. Wazazi wake wote walifanya kazi katika mashamba ya pamoja na Gorbachev aliwas

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATANO AGOSTI 31, 2022

Image
 

RAIS SAMIA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA WAANDAMIZI NA MAKAMANDA WA POLISI WA MIKOA NA VIKOSI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camilius Wambura pamoja na Makamanda wengine wa Jeshi hilo mara baada ya kufungua Kikao Kazi cha Makamanda hao . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu mara baada ya kufungua Kikao Kazi cha Makamanda hao kilichofanyika kwenye Chuo cha Polisi (CCP) Mkoani Kilimanjaro tarehe 30 Agosti, 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati akifungua Kikao Kazi Cha Maafisa Wakuu Waandamizi wa Makao Makuu ya Polisi na Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi kilichofanyika katika Chuo cha Polisi (CCP) Mkoani Kilimanjaro tarehe 30 Agosti, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi wengine katika picha ya pamoja na Maafisa Wakuu Waandamizi wa Makao

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMANNE AGOSTI 30, 2022

Image