Posts

Showing posts from May, 2023

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AKUTANA NA RAIS WA BURUNDI NDAYISHIMIYE

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na Rais wa Burundi Mheshimiwa Evariste Nayishimiye mara baada ya kuwasili Ikulu ya Bujumbura nchini Burundi kushiriki Mkutano wa Dharura wa 21 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) leo tarehe 31 Mei 2023. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Ikulu ya Bujumbura nchini Burundi leo tarehe 31 Mei 2023. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa 21 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika nchini Burundi.  

DKT. NCHEMBA AWAAGIZA WATAALAM WA UCHUMI WA KITAIFA NA KIMATAIFA KUTAFUTA SULUHU YA UPUNGUFU WA DOLA ZA MAREKANI KATIKA SOKO LA FEDHA

Image
 Na Farida Ramadhani-Dodoma Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewaagiza wataalamu wa Wizara ya Fedha na Mipango na ujumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kujadili namna ya kushughulikia athari za upungufu wa dola za Kimarekani katika mzunguko wa fedha ili kunusuru uchumi wa nchi zinazoendelea. Mhe. Dkt. Nchemba (Mb) ametoa maagizo hayo wakati wa kufungua kikao kilichowashirikisha wataalam kutoka Shirika la Fedha na Kimataifa (IMF) waliowasili nchini kwa ajili ya kufanya tathimini ya Program ya Huduma za Mikopo (EFC), kwa kushirikiana na wataalam wa ndani wa Serikali. Alisema mabadiliko ya Sera za Fedha nchini Marekani ya kubana matumzi na kupunguza dola kwenye mzunguko wa fedha, yameleta athari zinazoonekana mpaka kwenye nchi zinazoendelea, ikiwemo Tanzania. “Tumekuwa tukirejea Uviko na vita baina ya Urusi na Ukraini kama moja ya vitu vinavyoathiri uchumi wa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania lakini upungufu wa dola unaathiri uchumi kwa ki

PSSSF YAWAALIKA WANACHAMA KUTEMBELEA BANDA LAO MAONESHO YA UTALII NA BIASHARA TANGA 2023

Image
  Na Mwandishi wetu, Tanga.   Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetoa wito kwa wastaafu, wanachama wa Mfuko huo na wananchi kwa ujumla kufika kwenye banda lao katika Maonesho ya Biashara na Utalii katika viwanja vya Mwahako jijini Tanga ili kuhudumiwa na kupata Elimu ya Hifadhi ya Jamii. Maonesho hayo ambayo yamefunguliwa rasmi leo Mei 31, 2023, na Bw. Conrad John Milinga, Kaimu Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara timu ya PSSSF, ikiongozwa na Meneja wa Kanda ya Kaskazini Bi Vones Koka, iko tayari kuwahudumia wanachama na wananchi kwa ujumla. Akizungumzia Huduma zitolewazo na PSSSF katika band Hilo, Bi. Vones . Kola alisema mwanachama atafurahia huduma kama ambazo amekuwa akipata kwenye Ofisi za Mfuko zilizoenea kote nchini. Alizitaja kuwa ni pamoja na Mwanachama kupata taarifa za michango yake, Mstaafu kuhakiki taarifa zake, Elimu ya mafao yanayotolewa na Mfuko na fursa za uwekezaji." Alifafanua. Akieleza zaidi,  alisema muitikio wa watu kutembe

CHONGOLO ACHANGISHA FEDHA KUJENGA NYUMBA YA BALOZI, GAVU AZUNGUMZIA KADI MPYA CCM ITAKAVYOTUMIKA BENKI, BIMA

Image
  Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV. KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo ameendesha harambee ya ujenzi wa nyumba ya balozi wa Shina namba saba Kijiji cha Ilambilole kilichopo jimboni Isimani mkoani Iringa. Chongolo ameendesha harambee hiyo Mei 30, 2023 baada ya kuelezwa kuwa balozi huyo amepanga nyumba na hivyo kukosa eneo zuri la kuendeshea vikao vya chama vya kikatiba. "Kazi ya Chama Cha Mapinduzi ni kutenda kwa vitendo badala ya kupiga porojo majukwaani na kuwadanganya wananchi, " amesema Chongolo na kuongeza watashindanisha mashina yote wa CCM nchini. "Na shina ambalo litafanya vizuri kwa kuingiza wanachama wapya ,kueneza sera za Chama hawataachwa bila kufanyiwa kitu katika mashina yao." Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Chongolo ametoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendegu kuhakikisha Wakala wa Umeme Vijijini(REA)wanapeleka umeme kwenye vijiji vyote vya Iringa Vijijini. Chongolo amesema kwamba kwa sasa umeme sio hanasa bali ni maen

MBINU ZA TOLEWA KWA MAOFISA NA ASKARI KUKABILIANA NA MAJNAGA

Image
  Na Mwandishi wetu Jeshi la Polisi-Dar es salaam. Chuo cha Taaluma ya Polisi Dae es salaam (DPA) kimeendelea kutoa elimu na mafunzo mbalimbali kwa maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali katika kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapotokea. Akitoa taarifa hiyo leo Mei 30,20223 Mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Dkt. Lazaro Mambosasa amesema kuwa chuo hicho kimekuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa kozi mbalimbali wawapo chuoni hapo. Ameendelea kueleza kuwa lengo la kutoa elimu hiyo ni kujenga uwezo kwa maofisa,wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wa Jeshi hilo na makundi mengine ya wahitaji ambapo amebainisha kuwa ni vyema kila askari kuwa na vifaa wezeshi ili kukabiliana na majanga hayo pindi yanapotokea. Mbali na hilo Mkuu wa chuo hicho ametumia fursa hiyo kumpa pole mkufunzi wa chuoni hapo aliyepata majanga ya kuunguliwa moto nyumba yake, ambapo amebainisha kuwa kutokana na changamoto hiyo aliyoipata w

“SERIKALI KUJENGA VITUO MAALUM VYA UREKEBU” WAZIRI MHAGAMA

Image
  Na Mwandishi Wetu – Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama, amesema  Serikali imejenga vituo maalum vya urekebu na ufundi stadi ili kuwasadia vijana  na wale wote wanaoathirika baada ya kutumia dawa za kulevya. Ameyasema hayo mapema leo Mei 30 2023, Bungeni  Dodoma  wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu hali ya dawa za kulevya ya mwaka 2022 ambapo amessema kwa mujibu wa utafiti unaonyesha  uwepo wa kiwango kikubwa cha uzalishwaji na ulimaji wa bangi. Waziri Mhagama alisema, kwa mwaka ujao wa  fedha  2023/2024 Serikali imetenga bajeti ya shilingi Bilioni nane nukta saba (Bilioni 8.7)  zitakazotumika kujenga vituo vya urekebu na ufundi stadi, vitakavyosaidia kubadilisha tabia za vijana wanaotumia dawa  za kulevya, “Vituo hivyo vitakuwa na kazi kubwa ya kuwaondoa kwenye matumizi ya dawa na kuwapa shunguli nyingine watakazotakiwa kuzifanya zitakazotokana na shughuli za ujuzi, ambazo watafundishwa kwenye

RC SINGIDA :UKAMILISHAJI WA MIRADI YA MAENDELEO NI JAMBO LA KUFA NA KUPONA

Image
    Mkuuwa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akizungumza na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida wakati alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mkhandi kilichopo wilayani humo leo May 30, 2023. Kulia ni Mkuu wa wilaya hiyo, Mhandisi Paskas Muragili na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Omari Mande. ........................................................   Na Dotto Mwaibale, Singida MKUU wa Mkoa wa Singida,Peter Serukamba amesema kazi ya kumalizia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika wilaya zote mkoani hapa ni la kufa na kupona na kuwa kazi hiyo ifanyike usiku na mchana kutokana na umuhimu wake. Serukamba ameyasema hayo leo May 30, 2023 wakati alipokuwa katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea na kukagua ukamilishaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida na kuhimiza miradi yote iwe imekamilika kabla ya Julai 1, 2023 kwa viwango vinavyotakiwa na kulingana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa. &q

DC IRAMBA AGUSWA NA ADHA YA WANANCHI KIJIJI CHA MSAI KUKOSA ZAHANATI

Image
  Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda (katikati) akishiriki kufyatua matofali wakati wa mfululizo wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo aliyoifanya Kata ya Shelui na Mtoa wilayani humo jana May 29, 2023 akiwa ameongoza na wataalam, watendaji wa Kata na Tarafa pamoja  na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama. ......................................................  Na Mwandishi Wetu, Iramba MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda amesema atafanya mawasiliano na wahusika wa sekta ya afya ili ziweze kupatika fedha za kumalizia ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Msai Kupatikana kwa fedha hizo na kukamilika kwa ujenzi wa zahanati hiyo kutawaondolea adha wananchi ya kutembea umbali mrefu kwenda kupata huduma za matibabu maemo mengine. Mwenda ameyasema hayo  wakati alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Kata yaMtoa na Shelui pamojana kusikiliza kero za wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi. Aki