Saturday, February 27, 2021

WAZIRI AWESO AAGIZA MKANDARASI KULIPWA FEDHA

 

Mh.Waziri akimtwisha ndoo mmoja wa wananchi wa kijiji cha kashangu Halmashauri ya Itigi mara baada ya kuzindua mradi huo.

Waziri na watendaji wa RUWASA pamoja na Viongozi wengine wa Wilaya ya Manyoni wakipanda juu ya Tanki la maji linalohudumiwa na mradi wa kintinku.

iongozi akiwemo Pius Chaya katikati wakiongozana na Mh.Waziri kutoka kwenye chanzo cha maji katika mradi wa kintinku Wilayani Manyoni..
Waziri akiteta jambo na Meneja wa RUWASA Mhandisi Lucas Said.

Mh.Waziri akizungumza mara baada ya kukagua chanzo cha mradi wa kintinku Wilayani Manyoni.

 Na Mwandishi wetu,Singida.

WAZIRI wa Maji,  Jumaa Aweso ametoa siku saba kwa Meneja wa wakala wa maji na usafi wa Mazingira Vijijini na mijini (RUWASA) Mkoa wa Singida kumlipa Mkandarasi anayejenga mradi wa maji uliopo katika Kijiji cha Kintinku Wilayani Manyoni.

Aweso alitoa kauli hiyo juzi wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja mkoani hapa ya kutembelea miradi pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa idara hiyo ya maji.

Baada ya Waziri kujionea utekelezaji mzuri wa mradi huo unaojengwa na Mkandarasi mhandisi Jumanne Werema kutoka kampuni ya (CMG)ambaye anadai zaidi ya shilingi milioni 700 huku mradi ukiwa katika hatua za mwisho Waziri akaagiza ndani ya wiki ijayo Mkandarasi huyo awe amelipwa fedha hiyo.

"Naagiza RUWASA Mkoa mlipeni huyu Mkandarasi fedha yake,haiwezekani Mkandarasi amefanya kazi nzuri namna hii na mradi umekamilika alafu asilipwe hela yake.Meneja mlipeni ndani ya wiki ijayo." alisema Aweso.

Aidha Aweso amempongeza Meneja wa RUWASA wa Wilaya ya Manyoni mhandisi Gabriel Gongi kwa kuokoa shilingi milioni 150 katika ujenzi wa mradi wa maji Kijiji cha Kashangu katika Halmashauri ya Itigi ambapo mradi huo umegharimu shilingi milioni 200 badala ya 350 kabla ya kutumia mfumo wa Force Account.

"Nakupongeza sana Meneja,hawa ndio Viongozi tunaowataka,umekuwa mwaminifu ungeweza kufanya vyovyote lakini kwa uzalendo ukatumia kiasi hiki. Hiyo pesa iliyobaki ikatumike sehemu nyingine ambapo mnaona kuna changamoto zaidi lengo letu ni kumtua mwanamke ndoo kichwani." na kuongeza.

"Hapo nyuma miradi ilikuwa inatumia gharama kubwa wakati wa kutekelezwa lakini kwa sasa watendaji wengi wamebadilika hongereni sana,hayo ndio Mh.Rais anayataka kuyaona. na wiki ya maji mkoa wa Singida tutazindua zaidi ya miradi 10 ya maji haya ni mafanikio makubwa." alisema Aweso


Hata hivyo aliwaomba wananchi wanaozunguka maeneo ya miradi kuilinda na kuitunza miradi hiyo ambayo imetumia pesa nyingi za Serikali ili iwasaidie  kwa sasa na hata vizazi vijavyo.

Awali akizungumza na wafanyakazi wa idara hiyo Aweso aliwapongeza kwa ushirikiano ambao umepelekea mafanikio makubwa ndani ya wizara na kusema kuwa lengo ni kuona kati ya wizara tatu zitakazo tajwa kuwa zimefanya vizuri wizara ya maji iwe miongoni.

"Ndugu zangu tufanye kazi kwa ushirikiano tuache songombingo..tubadili mitazamo, tufanye kazi usiku na mchana ili Wananchi wapate huduma bora


NAIBU WAZIRI GEKUL ATEMBELEA KAMPUNI YA TANGA FRESH NA MNADA WA NG’OMBE WA NDEREMA MKOANI TANGA

 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul ( wanne kutoka kulia) akiangalia bidhaa mbalimbali za maziwa zinazozalishwa na Kampuni ya Tanga Fresh alipotembelea kukagua shughuli za Kiwanda hicho kilichopo Mkoani Tanga mapema leo.

Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Ummy Mwalimu akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (wapili kulia) walipokutana katika kikao cha Wavuvi na Naibu Waziri huyo kilichofanyika Mkoani Tanga mapema leo lengo la kikao hicho ni kusikiliza kero za Wavuvi wa Mkoani Tanga.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul akikagua risiti aliyopewa mfanyabiashara aliyenunua Ng’ombe katika Mnada wa Nderema uliopo katika Halmashauri ya Mji, Handeni, Mkoani Tanga leo . Naibu Waziri alitembelea mnada huo kukagua shughuli zinazoendelea katika mnada huo. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (katikati) akiangalia Ng’ombe waliopelekwa katika Mnada wa Nderema kwa ajili ya kuuzwa. Naibu Waziri alitembelea mnada huo uliopo Katika Halmashauri ya Mji, Handeni, Mkoani Tanga leo  kwa lengo la kukagua shughuli zinazofanyika Mnadani hapo.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul ( wanne kutoka kulia) akiangalia bidhaa mbalimbali za maziwa zinazozalishwa na Kampuni ya Tanga Fresh alipotembelea kukagua shughuli za Kiwanda hicho kilichopo Mkoani Tanga mapema leo.

Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Ummy Mwalimu akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (wapili kulia) walipokutana katika kikao cha Wavuvi na Naibu Waziri huyo kilichofanyika Mkoani Tanga mapema leo lengo la kikao hicho ni kusikiliza kero za Wavuvi wa Mkoani Tanga.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul akikagua risiti aliyopewa mfanyabiashara aliyenunua Ng’ombe katika Mnada wa Nderema uliopo katika Halmashauri ya Mji, Handeni, Mkoani Tanga leo . Naibu Waziri alitembelea mnada huo kukagua shughuli zinazoendelea katika mnada huo. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul (katikati) akiangalia Ng’ombe waliopelekwa katika Mnada wa Nderema kwa ajili ya kuuzwa. Naibu Waziri alitembelea mnada huo uliopo Katika Halmashauri ya Mji, Handeni, Mkoani Tanga leo  kwa lengo la kukagua shughuli zinazofanyika Mnadani hapo.

NAIBU WAZIRI MABULA AIBANA MANISPAA YA IRINGA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi hati ya umiliki wa ardhi Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Jesca Msavatavangu wakati wa kikao kazi na watendaji wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Iringa mwishoni mwa wiki.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa Iringa aliowakabidhi hati wakati wa kikao kazi na watendaji wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Iringa mwishoni mwa wiki. (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA)
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi katika kikao kazi wakati wa ziara yake ya siku moja katika mkoa wa Iringa mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela
Watendaji wa Sekta ya ardhi katika mkoa wa Iringa wakifuatilia maelezo ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa kikao kazi kilichofanyika mkoani Iringa mwishoni mwa wiki.
Mkurugezi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Hamid Njovu akizungumza wakati wa kikao kazi baina ya watendaji wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Iringa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza wakati wa kikao kazi baina ya watendaji wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Iringa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula mwishoni mwa wiki.

NAIBU WAZIRI MABULA AIBANA MANISPAA YA IRINGA

Na Munir Shemweta, IRINGA   

Niabu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameibana Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kurejesha fedha kiasi cha shilingi milioni 418 ilizopewa na Wizara ya Ardhi kwa ajili ya mradi wa kupanga, kupima na kumilikisha viwanja katika manispaa hiyo.

Akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi na wakurugenzi wa halmashauri za mkoa wa Iringa katika kikao kazi kilichofanyika mwishoni mwa wiki, Dkt Mabula alisema fedha ilizopewa Manispaa ya Iringa ni mkopo kwa ajili ya kupima viwanja na siyo kwa ajili ya shughuli nyingine za halmashauri.

Alisema, baada ya kukamilisha zoezi upangaji na upimaji viwanja Manispaa ilitakiwa kurejesha fedha ilizokopeshwa na kiasi kinachopatikana kama faida walitakiwa kuendeleza shughuli za sekta ya ardhi katika halmashauri.

‘’Wizara imetoa fedha ili upime viwanja na kuuza na baadaye urudishe fedha lakini ninyi badala ya kurudisha fedha mmetumia kwenye mambo mengine, wenzenu Geita faida waliyopata katika mradi kama huu walinunua gari la idara ya ardhi, hatuwezi kutumia fedha kwa utaratibu huo’’ alisema Naibu Waziri Mabula.

Alizitaka halmashauri zote zilizokopeshwa fedha na Wizara ya Ardhi kwa ajili ya mradi wa kupanga, kupima na kumilikisha viwanja kuzirejesha kulingana na makubaliano ili kuwezesha halmashauri nyingine zenye uhitaji kukopa. Alisema halmashauri zitakazokaidi kuzirejesha fedha kwa wakati basi suala hilo litawasilishwa mamlaka husika ili wahusika wakatwe fedha hizo moja kwa moja.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa Hamid Njovu alimuahidi Naibu Wzairi wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa halmashauri yake itahakikisha inakamilisha kulipa deni hilo kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha 2020/2021.

Alisema, haikuwa nia ya halmashauri yake kutolipa deni hilo kwa wakati bali hali hiyo imesababishwa na changamoto ya malalamiko ya wananchi kutaka kuongezwa idadi ya viwanja 1000 wakati wakiendelea na zoezi hilo. Hata hivyo alisema Manispaa yake inadai takriban milioni 500 kwenye mradi huo.

‘’Mhe Naibu Waziri wa Ardhi naahidi kulipa deni hilo haraka iwezekanavyo na kila mwezi nitatoa milioni 50 za kulipa deni hilo’’ alisema mkurugenzi wa Mnaispaa ya Iringa Njovu.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alizitaka halmashauri nchini kulitumia Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika kujenga nyumba kwa ajili ya kupangisha watumishi.

Alisema, nyumba zitakazojengwa na Shirika la Nyumba zitakuwa kitega uchumi cha halmashauri kitakachoingizia mapato yatakayotumika katika kuendesha shughuli zake za kimaendeleo.

Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Muungano Saguya alisema, Shirika lake limekuwa likijenga nyumba kwa ajili ya kupangisha na kuuza kwa mkataba wa miaka mitatu hadi saba kwa sharti la kupatiwa ardhi isiyolipiwa fidia sambamba na kuwa na miundombinu kama ya maji, umeme na barabara.

Aidha, Saguya alibainisha kuwa, Shirika la Nyumba la Taifa kwa sasa halilazimishi kujenga nyumba zilizoko eneo moja kama makambi bali linajenga kulingana na mahitaji ya mteja na kutolea mfano wa nyumba zilizojengwa halmashauri ya Busekelo kuwa ni chaguo la mteja.

 

TAASISI TA UHASIBU SINGIDA YAZINDUA UMOJA WA WANAFUNZI WA FANI YA UNUNUZI NA UGAVI

 

Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania  (TIA) Tawi la Singida,  Dkt. James Mrema akisoma taarifa  wakati wa hafla ya kuzindua  rasmi umoja wa wanafunzi wanaochukua fani ya ununuzi na ugavi. 

Mwenyekiti wa umoja wa wanafunzi wanaochukua fani ya ununuzi na ugavi,  Evarist Peter akisoma taarifa ya umoja huo.

Mgeni  rasmi wa hafla ya kuzindua rasmi umoja wa wanafunzi wanaochukua fani ya ununuzi na ugavi  mkoani Singida,  Kaimu Afisa Vijana wa mkoa  huo, Frederick  Ndahani (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali. Kulia ni mkuu wa Taasisi hiyo, Singida na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji  Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Taasisi hiyo nchini,  Godfred Mbanyi  wakifuatilia taarifa ya umoja wa wanafunzi wanaochukua fani ya ununuzi na ugavi.


Mlezi wa umoja huo, Mhadhiri Msaidizi, Eliaichi Kyara, akifuatilia hafla hiyo.

Mgeni rasmi akihutubia wanafunzi wanaochukua fani ya ununuzi na ugavi katika Taasisi hiyo ya Uhasibu Tawi la Singida.

Mgeni rasmi Frederick  Ndahani (Wa pili kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi na viongozi.Kulia  ni Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Tawi la Singida, Dkt. James Mrema na wa tatu kutoka kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji  Bodi ya Ununuzi na Ugavi wa Taasisi hiyo nchini, Godfred Mbanyi na kushoto ni Mlezi wa umoja huo, Mhadhiri Msaidizi, Eliaichi Kyara na Afisa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  (TAKUKURU) Mkoa wa Singida, Samson Julius.


Na Dotto Mwaibale, Singida.


TAASISI ya  Uhasibu Tanzania (TIA) Tawi la Singida imefungua rasmi umoja wa wanafunzi wanaochukua fani ya ununuzi na ugavi ili kuwaweka pamoja na kutengeneza mahusiano mazuri na bodi ya ununuzi na ugavi (PSPTB)


Akisoma taarifa ya umoja huo wa wanafunzi wanaochukua fani hiyo kabla ya kuzinduliwa Mwenyekiti  wa umoja huo Evarist Peter alisema umoja huo uliundwa tangu mwaka 2017 ambapo unajumuisha vyuo 14 hapa nchini vinavyotoa fani hiyo huku wanafunzi wakiwa 590.

"Tunatarajia kupata mafunzo mbalimbali yatakayo tusaidia kukuza ujuzi wetu wa fani ya ununuzi na ugavi ambapo tunatarajia kuleta wataalamu kutoka maeneo na taasisi mbalimbali ikiwemo bodi yetu ya ununuzi na ugavi na wakala wa ununuzi na ugavi (GPSA) na hii ni kwa maslahi yetu na taifa kwa ujumla." alisema Peter.

Mlezi wa umoja huo, Mhadhiri Msaidizi, Eliaichi Kyara alisema lengo la kuanzishwa kwa umoja huo ni pamoja na kuwawezesha wanafunzi wa fani husika kupata warsha na mafunzo mbalimbali ya ununuzi na ugavi,kuwakutanisha na kuwaweka pamoja wanafunzi wanaochukua fani hiyo hapa nchini,kupata uelewa na kutengeneza mahusiano mazuri na bodi ya ununuzi na ugavi pamoja na kutengeneza fursa ya wanafunzi hao kujiajiri na kuajiriwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi hiyo Tawi la Singida,  Dkt. James Mrema alisema licha ya kuwepo fursa ya chuo hicho mkoani hapo, mwitikio wa wakazi wa mkoa huo ni mdogo kwani wanachuo wengi wanaosoma chuoni hapo wanatoka mikoa mingine.

"Wakazi wa mkoa huu hawachangamkii fursa ya kuwepo taasisi hiyo kwa mamlaka yako tunakuomba uone namna ya kuwahamasisha wazazi ili kuwaleta watoto wao wanaohitimu kidato cha nne na sita nakuomba kwa nafasi yako kuzielekeza halmashauri za mkoa huu kutupatia fursa ya kuendesha mafunzo mbalimbali kwa watumishi wake ili kuwajengea uwezo kwa lengo la kuboresha ufanisi na utendaji wenye tija katika maeneo yao."alisema Mrema.

Akizindua umoja huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Kaimu Afisa Vijana wa Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani aliwaagiza wanafunzi hao kuhamasishana ili wafuate maadili na miiko ya masuala ya ununuzi na ugavi ili wakati wanapopata ajira waweze kuwatumikia watanzania kwa moyo wa kizalendo.

"Bodi ya ununuzi na ugavi endeleeni kuwakumbusha wanafunzi wanaochukua fani hii ili wafuate maadili na miiko mbalimbali ya ununuzi na ugavi awamu hii ya tano kama kuna mtu anafikiri akiajiriwa anaenda kupiga hela hiyo afute nafasi hiyo haipo." alisema na kuongeza.

"Niwaombe wanafunzi kupitia fursa hii mlioipata na mtakapopata ajira serikalini mkasimamie fedha za Serikali,mnao wajibu wa kuisadia jamii kufuata taratibu za manunuzi na ugavi." alisema Ndahani.

Aidha amewaambia kwa kushirikiana na viongozi wa umoja huo atangalia namna na wao kupata nafasi ya kwenda kujifunza masuala ya manunuzi na ugavi katika ofisi ya mkuu wa mkoa ili waendelee kupata uzoefu zaidi wa kivitendo.

Hata hivyo aliwataka wanafunzi hao kubadili fikra kuwa kusoma sio lazima kuajiriwa wanaweza kujiajiri wenyewe kupitia taaluma walioipata,hivyo wafikiri nje ya boksi ili kujikwamua kiuchumi.

"Taaluma ya ununuzi na ugavi ni taaluma muhimu sana kwa familia, jamii na taifa kwa ujumla hivyo mkaanzishe miradi mbalimbali itakayowasaidia kiuchumi..naamini kwa taaluma yenu mtaisimamia vyema miradi hiyo." alisema Ndahani.

RAIS MAGUFULI, AMUAPISHA DKT. BASHIRU KAKURWA, KUWA KATIBU MKUU KIONGODI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Balozi kabla ya kumuapisha tena kuwa Katibu Mkuu Kiongozi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 27 Februari 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Kamishna wa Maadili Jaji wa Mahakama ya Rufani, Sivangilwa Sikalaliwa Mwangesi kushoto alipokuwa akiongoza Kiapo cha Maadili kwa Viongozi wa Umma kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Kamishna wa Maadili Jaji wa Mahakama ya Rufani, Sivangilwa Sikalaliwa Mwangesi kushoto alipokuwa akiongoza Kiapo cha Maadili kwa Viongozi wa Umma kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akizungumza mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Februari 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


 

WANANCHI WA LUSHOTO WAISHUKURU SERIKALI KUWAREJESHA SHUGHULI ZA UZALISHAJI KATIKA KIWANDA CHA KUCHAKATA CHAI CHA MPONDE TEA ESTATE


Na: Mwandishi Wetu – Lushoto

Wananchi wa Lushoto katika Wilaya ya Bumbuli wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwarejesha shughuli za uzalishaji katika kiwanda cha Mponde Tea Estate kilichopo kata ya Mponde, Wilayani Lushoto.

Shukrani hizo wamezitoa wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara kiwanda hapo ikiwa ni maagizo yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majiliwa kuwa kiwanda hicho kianze kazi.

Waziri Mhagama alieleza habari hizo njema za Serikali kwa wananchi hao kuwa hivi sasa ni kuwa Serikali yao imeamua kufufua kiwanda hicho ili wakulima wa chai waendelee kulima zao hilo la chai litakaloleta manufaa kwa wakazi wa Bumbuli na Wilaya ya Lushoto kwa Ujumla.

“Serikali imeamua kurejesha matumaini kwa wakazi wa Bumbuli na Wilaya ya Lushoto kwa kuanzisha shughuli za uzalishaji katika kiwanda cha Mponde Tea Estate ili kuhakikisha kilimo cha zao la chai kinaleta tija na kusaidia wakulima wa zao waliopo katika maeneo haya wananufaika zaidi,” alisema Mhagama

Alieleza kuwa, Serikali inatambua changamoto zilizokuwa zikiwakabili wakazi wa eneo hilo waliokuwa wakijihusisha na kilimo cha Chai, hivyo Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kuanzisha shughuli za uzalishaji katika kiwanda hicho ili kuwezesha wanabumbuli na Lusho kwa ujumla kuongeza uzalishaji wa zao hilo kwa kuwa wanasoko la hukakika katika kiwanda hicho.

Aliongeza kuwa, Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020 – 2025 imeweka zao la Chai kuwa moja wapo ya zao la kimkakati na hivyo uzalishaji wa zao hilo kwa sasa hapa nchini ni zaidi ya tani 37,000 lakini Serikali imejipanga kuongeza zaidi uzalishaji wa zao hilo ifikapo 2025 uzalishaji kufikia tani zaidi ya 60,000.

Sambamba na hayo Waziri Mhagama alieleza kuwa Kikosi kazi kipo tayari kwa ajili ya kuhakikisha kiwanda kinaanza shughuli za uzalishaji ambapo timu ya kwanza itahusisha mafundi wabobezi ambao watahusika na kuboresha mitambo ya kiwanda hicho ili kianze uzalishaji haraka huku wakiwa na mkakati wa kujenga kiwanda kipya katika eneo hilo, timu ya pili itakuwa ikiangalia masuala ya utawala ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia shughuli za kiwanda hicho, huku timu ya mwisho ikiwa na jukumu la kuwawezesha wakulima kuongeza tija ya uzalishaji wa zao hilo la chai.

“Katika ziara hii nimeambatana na wataalam kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo TIRDO, Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na Benki ya Kilimo kwa lengo la kuhakikisha kiwanda hiki kinaanza kuzalisha na kuwanufaisha wakulima wa chai katika wilaya ya Lushoto na wakazi wa mponde,” alisema Mhagama

Aidha, Waziri Mhagama amewasisitiza wakulima wa zao hilo la chai katika Halmashauri ya Bumbuli na Wilaya ya Lushoto kwa ujumla kutatua migogoro iliyopo ndani ya AMCOS zao ili wafufue mashamba yao kwa kuwa hivi sasa wamepata sehemu ya uhakikaka ya kupeleka zao la chai ambalo litachakatwa.

Kwa Upande Wake, Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Mhe. January Lugangika alieleza kuwa Kata 18 zilizopo katika wilaya hiyo zinalima zao la chai na asilimia kubwa ya wakulima wa zao hilo wanamatumaini makubwa na kiwanda hicho katika kuwainua kiuchumi kutokana na ajira watakazo zipata kiwandani hapo pamoja na kuuza malighafi hiyo ya zao la chai.

Naye, Mbunge wa Bumbuli Mhe. January Makamba amewataka wananchi hao kuchangamkia fursa ya kuzalisha zao la chai kwa wingi kwa kuwa Serikali yao imeamua kuanzisha uzalishaji katika kiwanda cha Mponde Tea Estate.

“Migogoro iliyojitokeza katika kiwanda hiki hapo awali ilichangia kudhorotesha uchumi wa wakazi wa maeneo haya kwasababu wananchi wengi waliacha kulima zao la chai baada ya kiwanda hicho kufungwa ila kuanzishwa shughuli za uzalishaji katika kiwanda hicho itahamasisha wakulima wengi kulima zao la chai na kunufaika kiuchumi,” alisema Makamba

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo Bw. Juma Msilimu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kurejesha matumaini kwa wananchi hususan wakulima wanaojishughulisha na kilimo cha zao la chai wa halmashauri ya Bumbuli na Wilaya ya Lushoto kwa ujumla kutokana na uwepo wa kiwanda hicho cha Mponde Tea Estate.  

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akihutubia wananchi wa Bumbuli Wilayani Lushoto alipofanya ziara katika kiwanda cha Mponde Tea Estate kilichopo kata ya Mponde, Wilayani Lushoto ikiwa ni utekelezaji wa Maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majiliwa. Kulia ni Mbunge wa Bumbuli Mhe. January Makamba.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akihutubia wananchi wa Bumbuli Wilayani Lushoto alipofanya ziara katika kiwanda cha Mponde Tea Estate kilichopo kata ya Mponde, Wilayani Lushoto.
Sehemu ya Wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati alipowasili kwenye Kijiji cha Mponde Wilayani Lushoto kukagua Kiwanda cha Chai cha Mponde.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akijadiliana jambo Mbunge wa Bumbuli Mhe. January Makamba (kushoto).
Mbunge wa Bumbuli Mhe. January Makamba akielezea historia fupi ya kiwanda hicho cha Mponde Tea Estate kilichopo kata ya Mponde, Wilayani Lushoto wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiangalia mtambo maalum unaotumika kuchomea kuni kwa ajili ya kuchakata chai “Boiler”.   Wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa Bumbuli Mhe. January Makamba.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akipokea maelezo kuhusu namna mitambo ya kiwanda cha hicho chai cha mponde inavyofanya kazi. Kushoto ni Bw. Juma Msilimu ambaye alikuwa mtumishi wa kiwanda hicho kabla hakijafungwa akitoa maelezo hayo. Kulia ni Mbunge wa Bumbuli Mhe. January Makamba.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akieleza jambo wakati alipokuwa akikagua sehemu ya Vyombo vya Usafiri ikiwemo Matrekta yaliyokuwa yakitumika katika mashamba ya chai ya kiwanda hicho cha Mponde Tea Estate kilichopo kata ya Mponde, Wilayani Lushoto.