NAIBU WAZIRI MABULA AIBANA MANISPAA YA IRINGA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi hati ya umiliki wa ardhi Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Jesca Msavatavangu wakati wa kikao kazi na watendaji wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Iringa mwishoni mwa wiki.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa Iringa aliowakabidhi hati wakati wa kikao kazi na watendaji wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Iringa mwishoni mwa wiki. (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA)
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi katika kikao kazi wakati wa ziara yake ya siku moja katika mkoa wa Iringa mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela
Watendaji wa Sekta ya ardhi katika mkoa wa Iringa wakifuatilia maelezo ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa kikao kazi kilichofanyika mkoani Iringa mwishoni mwa wiki.
Mkurugezi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Hamid Njovu akizungumza wakati wa kikao kazi baina ya watendaji wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Iringa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza wakati wa kikao kazi baina ya watendaji wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Iringa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula mwishoni mwa wiki.

NAIBU WAZIRI MABULA AIBANA MANISPAA YA IRINGA

Na Munir Shemweta, IRINGA   

Niabu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameibana Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kurejesha fedha kiasi cha shilingi milioni 418 ilizopewa na Wizara ya Ardhi kwa ajili ya mradi wa kupanga, kupima na kumilikisha viwanja katika manispaa hiyo.

Akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi na wakurugenzi wa halmashauri za mkoa wa Iringa katika kikao kazi kilichofanyika mwishoni mwa wiki, Dkt Mabula alisema fedha ilizopewa Manispaa ya Iringa ni mkopo kwa ajili ya kupima viwanja na siyo kwa ajili ya shughuli nyingine za halmashauri.

Alisema, baada ya kukamilisha zoezi upangaji na upimaji viwanja Manispaa ilitakiwa kurejesha fedha ilizokopeshwa na kiasi kinachopatikana kama faida walitakiwa kuendeleza shughuli za sekta ya ardhi katika halmashauri.

‘’Wizara imetoa fedha ili upime viwanja na kuuza na baadaye urudishe fedha lakini ninyi badala ya kurudisha fedha mmetumia kwenye mambo mengine, wenzenu Geita faida waliyopata katika mradi kama huu walinunua gari la idara ya ardhi, hatuwezi kutumia fedha kwa utaratibu huo’’ alisema Naibu Waziri Mabula.

Alizitaka halmashauri zote zilizokopeshwa fedha na Wizara ya Ardhi kwa ajili ya mradi wa kupanga, kupima na kumilikisha viwanja kuzirejesha kulingana na makubaliano ili kuwezesha halmashauri nyingine zenye uhitaji kukopa. Alisema halmashauri zitakazokaidi kuzirejesha fedha kwa wakati basi suala hilo litawasilishwa mamlaka husika ili wahusika wakatwe fedha hizo moja kwa moja.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa Hamid Njovu alimuahidi Naibu Wzairi wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa halmashauri yake itahakikisha inakamilisha kulipa deni hilo kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha 2020/2021.

Alisema, haikuwa nia ya halmashauri yake kutolipa deni hilo kwa wakati bali hali hiyo imesababishwa na changamoto ya malalamiko ya wananchi kutaka kuongezwa idadi ya viwanja 1000 wakati wakiendelea na zoezi hilo. Hata hivyo alisema Manispaa yake inadai takriban milioni 500 kwenye mradi huo.

‘’Mhe Naibu Waziri wa Ardhi naahidi kulipa deni hilo haraka iwezekanavyo na kila mwezi nitatoa milioni 50 za kulipa deni hilo’’ alisema mkurugenzi wa Mnaispaa ya Iringa Njovu.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alizitaka halmashauri nchini kulitumia Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika kujenga nyumba kwa ajili ya kupangisha watumishi.

Alisema, nyumba zitakazojengwa na Shirika la Nyumba zitakuwa kitega uchumi cha halmashauri kitakachoingizia mapato yatakayotumika katika kuendesha shughuli zake za kimaendeleo.

Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Muungano Saguya alisema, Shirika lake limekuwa likijenga nyumba kwa ajili ya kupangisha na kuuza kwa mkataba wa miaka mitatu hadi saba kwa sharti la kupatiwa ardhi isiyolipiwa fidia sambamba na kuwa na miundombinu kama ya maji, umeme na barabara.

Aidha, Saguya alibainisha kuwa, Shirika la Nyumba la Taifa kwa sasa halilazimishi kujenga nyumba zilizoko eneo moja kama makambi bali linajenga kulingana na mahitaji ya mteja na kutolea mfano wa nyumba zilizojengwa halmashauri ya Busekelo kuwa ni chaguo la mteja.

 

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"