4/30/2021

RAIS SAMIA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA CCM KWA ASILIMIA 100%

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mhe. Samia Suluhu Hassan amechaguliwa na Mkutano Mkuu Maalim wa CCM kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa kura 1862, sawa na ASILIMIA 100.

Mwenyekiti wa uchaguzi, SPIKA wa Bunge, Mhe. Job Ndugai ametangaza kwenye mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo APRILI 30, 2021.

Uchaguzi huo unafuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho hayati Dkt. John Pombe Magufuli Machi 17, 2021.








RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mhe. Samia Suluhu Hassan amechaguliwa na Mkutano Mkuu Maalim wa CCM kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa kura 1862, sawa na ASILIMIA 100.

Mwenyekiti wa uchaguzi, SPIKA wa Bunge, Mhe. Job Ndugai ametangaza kwenye mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo APRILI 30, 2021.

Uchaguzi huo unafuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho hayati Dkt. John Pombe Magufuli Machi 17, 2021.



    

KAMPUNI YA GREEN MILE SAFARI YAREJESHEWA KITALU CHA LAKE NATRON EAST.

Na Mwandishi Wetu - Dodoma

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ametoa hukumu ya Kitalu cha uwindaji cha cha Lake Natron East kilichoko wilayani Longido mkoani Arusha na kuagiza kampuni ya Green Mile Safari irejeshewe leseni ya umiliki wa kitalu hicho iliyofutwa mwaka 2019.

Akitoa maamuzi hayo Dkt. Ndumbaro amesema kitalu hicho kinarejeshwa kwa Kampuni hiyo hadi mwaka 2022 kufuatia kufanyika kwa maombi ya mapitio ya hukumu iliyoifanya Kampuni ya Green Mile ifutiwe umiliki wa kitalu hicho.

 Aidha,Dkt. Ndumbaro amesema kufuatia uchambuzi uliofanyika kuhusu uamuzi wa kufutiwa umiliki wa kitalu cha Lake Natron – East, amejiridhisha kuwa malalamiko ya muomba mapitio ambayo ni kampuni ya Green Mile Safari yana msingi wa kisheria, na barua ya Mhe. Waziri ya kufuta umiliki wa kitalu haikuzingatia sheria na misingi ya utawala bora

“Iandaliwe rasimu itakayotumiwa katika umilikishaji wa vitalu itakayoonesha masharti ya kufuata ‘Terms and condition’ za kufuatwa na wawekezaji wakati wote wa umiliki wa kitalu cha uwindaji na kuwepo kwa umakini wakati wa kuandika nyaraka za kiofisi, ili kujiepusha na ukinzani wa sheria na taratibu zilizopo”, amesisitiza Dkt. Ndumbaro

Waziri Ndumbaro ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) iweke utaratibu wa kushughulikia migogoro haraka pindi inapojitokeza kuepusha hali iliyojitokeza.

Amesema mgogoro huo ulizorotesha ustawi wa uhifadhi na biashara ya Utalii, kuchafua taswira ya Tanzania katika tasnia ya uwindaji wa kitalii na kupunguza michango maendeleo kwa wananchi hivyo ni vyema TAWA ikahakikisha kuwa sheria, kanuni na miongozo inazingatiwa katika kusimaia sekta ya uwindaji wa kitalii.

“ Naishukuru Kamati ya ushauri kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa kunishauri katika kufikia uamuzi wa suala hili kwa mujibu wa kifungu cha 38(15) cha Sheria ya Wanyamapori Na.5 ya mwaka 2009. Mtu yoyote ambaye hajaridhika na uamuzi huu, ana haki ya kukata rufaa kwa mujibu wa kifungu cha 38(16) cha Sheria ya Wanyamapori Na.5 ya mwaka 2009”.

Katika hatua nyingeine Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ndumbaro amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Arusha na Wilaya ya Longido kusimamia maamuzi ya Serikali katika suala hilo la kurejeshwa kwa leseni ya Kampuni ya Green Mile Safari katika Kitalu cha uwindaji cha Lake Natron – East.

Kabla ya kutoa uamuzi huo Dkt. Ndumbaro alifanya ziara katika eneo la kitalu hicho na kuzungumza na wananchi ambapo alijionea hali halisi ya kitalu chicho na rasilimali zilizopo katika eneo hilo la Kitalu pia alisikiliza pande zote zinazoguswa na mgogoro huo kabla ya kutoa uamuzi wake.




 

    

WAZIRI MCHENGERWA AONGOZA MKUTANO WA PILI WA MAWAZIRI WA NCHI WANACHAMA WA UMOJA WA AFRI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati Na. 8 ya Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati Na. 8 inayoshughulika na masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala akiongoza Mkutano wa Pili wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Maadili na Misingi ya Utumishi wa Umma na Utawala Afrika kwa njia ya mtandao.
Na Mary Mwakapenda-Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati Na.8 ya Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati Na. 8 inayoshughulika na masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala leo ameongoza Mkutano wa Pili wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Maadili na Misingi ya Utumishi wa Umma na Utawala Afrika kwa njia ya mtandao.

Mhe. Mchengerwa ameongoza Mkutano huo ili kupitia na kuidhinisha ajenda mbalimbali zilizowasilishwa na Mkutano wa Wataalamu uliofanyika tarehe 27 na 28 Aprili, 2021. 

Miongoni mwa ajenda zilizopitiwa na kuidhinishwa ni rasimu ya Nyenzo ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Miiko na Misingi ya Utumishi wa Umma na Utawala Afrika; ambapo iliridhiwa kuwa Tanzania, Afrika ya Kusini, Namibia, Cameroon na Kenya zitahusika katika kufanya majaribio ya Utekelezaji wa Nyezo husika. 

Ajenda nyingine ni kuchagua Wajumbe wa Kamati ya Uongozi wa Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba; ambapo walioidhinishwa ni Mwenyekiti kutoka Afrika Kusini, Makamu Mwenyekiti wa Kwanza kutoka Algeria, Makamu Mwenyekiti wa Pili kutoka Cameroon, Makamu Mwenyekiti wa Tatu kutoka Benin na Katibu kutoka Tanzania. 

Pia mkutano ulitathmini hali ya utiaji saini na uridhiwaji wa Mkataba wa Umoja wa Afrika na kupendekeza mbinu za kukuza uridhiaji wa pamoja wa Mkataba huo kwa nchi wanachama ambapo ilibainishwa kuwa, mpaka sasa mwenendo wa utiaji saini na uridhiwaji wa Mkataba miongoni mwa nchi wanachama, nchi 38 zimeshasaini, wakati nchi 19 tu zimeridhia na 19 zimewasilisha Nyaraka za kuidhinisha. 

Aidha, Mkutano uliridhia juu ya kuhimiza Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kusaini na kuridhia Mkataba wa Umoja wa Afrika na Kuziomba AAPAM na AMDIN na Taasisi zingine kuutangaza Mkataba huu kupitia mijadala na tovuti mbalimbali. 

Sanjali na hilo, wajumbe walipitia na kuridhia Azimio la Mkutano wa Pili wa Nchi Wanachama kwa kuwasilisha taarifa ya kwanza ya utekelezaji wa Mkataba kwa Kamishna wa Umoja wa Afrika ifikapo mwezi Januari, 2022, na kuiomba Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuandaa taarifa ya jumla kuhusu Utendaji wa Utumishi wa Umma katika Afrika ikiwa ni pamoja na kudumisha ushirikiano na mshikamano baina ya Nchi Wanachama. 

Mkutano kazi huo, ulihudhuriwa na Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika walioridhia Mkataba huu ambao ni Algeria, Benin, Burundi, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Mali, Namibia, Rwanda, Afrika ya Kusini, Mali, Ivory Coast, na Tanzania. Mkutano wa Tatu wa Nchi Wanachama utafanyika mwezi Aprili, 2022.

    

RAIS MWINYI AFUTURISHA DODOMA

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, leo amejumuika na mamia ya waislamu katika Iftari aliyoiandaa kwa ajili yao na kufanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Conversion centre, Jijini Dodoma,

 Katika hafla hiyo viongozi mbali mbali wa Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) walihudhuria, akiwemo Rais mstaafu wa awamu ya saba ya Serikali ya Mapinduzi ya  Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, Mama Maryam Mwinyi na Mama Mwanamwema Shein .

 Wengine ni pamoja na Makamo wa Pili Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla, Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa Serikali za SMZ na SMT, Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Said Ahmeid,  Wabunge, Wawakilishi, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa pamoja na wageni mbali mbali.

 Akitoa shukran kwa waalikwa, Dk. Mwinyi amesema amefarikijika sana na muitikio wa waumini hao, mbali na mialiko kutolewa katika kipindi kifupi.

 Amesema ameamua kuandaa futari hiyo Jijini Dodoma kwa kuzingatia  uwepo wa vikao vya Bunge na vikao vya Chama cha Mapinduzi wakati huu, akibainisha kuwa ni wakati muafaka wa kukutana na kufutari pamoja na waumini hao.

 Aidha, Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwawezesha waumini hao kutekeleza vyema ibada hiyo muhimu ya funga, na kusema kukutana kwao huko ni jambo la kheri.

 Nae, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Sheikh Mustafa Rajab Shaaban amemuombea dua Rais Dk. Mwinyi pamoja na kumtakia kheri nyingi kwa Mwenyezi Mungu kwa maandalizi mazuri ya iftari hiyo.

 Alitumia fursa hiyo kumtakia rehma yeye na familia yake , akibainisha wema mkubwa aliowafanyia waumini waliotikia mwaliko wake.

 Akinukuu hadithi ya Mtume Muhamad (SAW), Sheikh Rajab amesema Mtume ameelekeza kuwalipa wema watu  wanaofanyia wenzao mambo wema na pale wasipokuwa na cha kuwalipa, basi ni vyema wakawaombea dua, hivyo dua hiyo ni jambo lililosadifu.

 Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi, yuko Jijini Dodoma kwa vikao mbali mbali vya Chama cha Mapinduzi, ambapo kesho April 30, 2021, Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama hicho watapiga kura ya kumthibitisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho kufuatia kifo cha Mwenyekiti wake, Rais  Dk. Joseiph Pombe Magufuli.







 






    

4/29/2021

UZINDUZI WA MKUTANO WA WADAU WA AFUA ZA VVU NA UKIMWI DODOMA

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Protabas Katambi akikagua banda la Epidemic Control (EPIC) wakati wa Mkutano wa Mwaka wa wadau wanaotekeleza Afua za VVU na UKIMWI zinazowalenga wasichana Balehe na Wanawake Vijana unaofanyika leo April 29 jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Protabas Katambi akizungumza na Vijana wakati wa Mkutano wa Mwaka wa wadau wanaotekeleza Afua za VVU na UKIMWI zinazowalenga wasichana Balehe na Wanawake Vijana unaofanyika leo April 29  jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Protabas Katambi akikagua banda la Amref Tanzania wakati wa Mkutano wa Mwaka wa wadau wanaotekeleza Afua za VVU na UKIMWI zinazowalenga wasichana Balehe na Wanawake Vijana unaofanyika  April 29  jijini Dodoma. Picha na Raymond Mushumbusi WAMJW
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Protabas Katambi akikagua banda la Tanzania Youth Alliance (TAYOA) wakati wa Mkutano wa Mwaka wa wadau wanaotekeleza Afua za VVU na UKIMWI zinazowalenga wasichana Balehe na Wanawake Vijana unaofanyika  leo April 29  jijini Dodoma.
Baadhi ya Vijana waliohudhuria Mkutano wa Mwaka wa wadau wanaotekeleza Afua za VVU na UKIMWI zinazowalenga wasichana Balehe na Wanawake Vijana unaofanyika leo April 29  jijini Dodoma
.
 Na Raymond Mushumbusi WAMJW Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi,amesema kuwa utafiti unaonesha  katika watu 72,000 wanaopata maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi  kwa mwaka asilimia 40 ni vijana na kati ya  hao asilimia 80 ni wasichana wenye umri kati ya  miaka 15-24.
Hayo ameyasema leo April 29,2021 akifungua mkutano wa mwaka wa wadau unaotekeleza afua za VVU na Ukimwi zinazowalenga wasichana balehe na wanawake vijana unaofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

Mhe.Katambi amesema kuwa Katika utafiti huo watu 72,000  wanapata maambukizi mapya kwa mwaka na kati yao 40% ni vijana; kati ya hao vijana 80% ni wasichana wa umri wa miaka 15 – 24 ikimaanisha  kuwa kila kundi la vijana 10 wenye maambukizi 8 kati yao ni vijana wa kike na 2 ni vijana wa kiume.

 ''Ni  muhimu kuwahimiza vijana na watu wote kupima ili kujua hali zao, kutumia dawa kwa waliogundulika  na VVU na kuepuka maambukizi ikiwa bado hawajapata maambukizi''amesema Katambi

Aidha, Katambi amesema  kupitia matokeo ya utafiti wa 2016/17 Serikali iliona umuhimu wa kufanya jitahada za pamoja na wadau katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI, hususani katika kundi la vijana wa kike.

“ Nimeelezwa kuwa kuna juhudi zinazofanywa kupitia miradi ya DREAMS initiatives wenye lengo la kuwafikia mabinti balehe na wanawake vijana wenye umri wa miaka 15 - 24 wakiwemo waliozaa kwenye umri mdogo, wanaoishi na maambukizi ya VVU, wenye mahusiano na mpenzi zaidi ya mmoja, walioolewa katika umri mdogo, mabinti waliocha shule, na mabinti wanaoongoza kaya katika jamii na walio ndani ya shule”amesisitiza Katambi.

Hata hivyo Katambi amesema kiwango cha ushamili kimeendelea kupungua sambamba na kiwango cha maambukizi mapya na vifo vitokanavyo na ukimwi.

Amesema wastani wa kitaifa wa ushamili wa VVU ni asilimia 4.7 ambapo mkoa wa Njombe umekuwa kinara kwa kuwa na asilimia 11.4 ukifuatiwa na Mikoa ya Iringa asilimia 11.3,Mbeya asilimia 9.3 na Mkoa wa Dodoma maambukizi yameongezeka kutoka asilimia 2.9 hadi kufikia asilimia 5.

Pia Katambi ametaja miradi  inayolenga kutoa elimu ya kujikinga na VVU  kuwa ni pamoja na mradi wa  DREAMS unaotekelezwa katika Mikoa 4 Halmashauri (12), Mradi wa Ujana Salama unatekelezwa katika Mikoa 4 na Halmashauri (11) na mradi wa Timiza Malengo unatekelezwa Katika Mikoa 5 na Halmashuri (18).

 Katambi amesema kuwa '' Niwambie Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutekeleza miradi ya maendeleo inayolenga kuwalinda Wasichana Balehe na Wanawake Vijana na vijana kwa jumla kwa kuimarisha utoaji wa huduma za afya na kijamii hususani kwenye kupunguza maambukizi ya VVU hasa kwa vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa''amesema Katambi

Hata hivyo  Katambi amesema kuwa malengo ya nchi ni  kufikia sifuri ya maambukizi mapya ya VVU, sifuri ya ubaguzi na unyanyapaa utokaonao na UKIMWI na sifuri ya vifo vitokanavyo na UKIMWI ifikapo 2030. 

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS),Dk.Leonard Maboko amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kuwaleta wadau na kuona wamefikia wapi na wamekutana na changamoto zipi pamoja na kuzitatua.

"Sisi TACAIDS kazi yetu ni kuratibu na ndio maana hapa kuna taasisi kazi yetu kubwa ya hili kundi ni kuratibu kila mwaka hivyo hichi kikao ni cha kuwaleta hawa wadau kuona wamefikia wapi na wamekutana na changamoto zipi pamoja na kuzitatua,ili kujadiliana tulipotoka tulipo na tunapoelekea,"amesema Maboko.

Dkt.Maboko amesema kuwa  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa aliagiza Tacaids ifanye kazi na vijana ambapo alidai kwa sasa wanafanya kazi nao hususan wasanii.

Hata hivyo Dkt.Maboko amesema kuwa takwimu zinaonesha vijana ni kundi lenye Changamoto katika maambukizi ya Ukimwi.

"Tulianzisha Kijiji Maalum kwa vijana ambayo inalenga masuala ya vijana na haya yote yalikuwa ni maagizo ya Waziri Mkuu na yalitokana na

"Maambukizi mapya asilimia 40 yalikuwa yanatokea kwa vijana lakini asilimia 80 ya hao vijana ni wa kike,kwa umaalumu kabisa ndio maana hili kundi likapewa msisitizo huu.Takwimu zilituonesha hivyo tukaona kuna haja ya kuweka mkazo katika hili,"amesema

Awali ,Balozi Mwakilishi wa wasichana balehe na wanawake vijana Rosemari Shani akisoma risala amesema kuwa wanakabiliwa na changamoto za upungufu wa vituo vya kutolea huduma kwa vijana,ukosefu wa soko la uhakika wa bidhaa wanazozalisha,uelewa mdogo wa jamii kuhusu kinga za VVU.

"Elimu zaidi iendelee kutolewa tunaomba uziimize Halmashauri ziendelee kutoa mikopo kwa wanawake.Sisi Kama wasichana tunakuahidi kufanya juhudi kujiunga na Veta na Sido ili kukuza ujuzi.Tutaendelea kuwajibika katika familia zetu,"amesema 

Hata hivyo amesema kuwa  wanajivunia kumpata Rais mwanamke,Samia Suluhu Hassan kwani hiyo ni chachu kubwa kwao kuendelea kusoma na kufanya kazi kwa bidii.

"Tunajivunia kumpata Rais mwanamke jambo hili ni chachu kubwa kwetu.Tunaishukuru Serikali na wadau ambao wanatusaidia tunatarajia mambo mazuri,"amesema