Posts

Showing posts from September, 2022

PSSSF YAWAALIKA WANACHAMA NA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO KWENYE MAONESHO YA 5 YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA.

Image
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ambao unashiriki katika Maonesho ya 5 ya teknolojia ya madini kwenye viwanja vya Bombambili mkoani Geita umewaalika Wanachama na wananchi wote wa Geita kutembelea banda lao ili kupata huduma zitolewazo na Mfuko huo. Meneja wa PSSSF Mkoa wa Geita, Bw. Geofrey Kolongo amesema "miongoni mwa huduma zinazotolewa bandani hapa ni pamoja na elimu kuhusu Hifadhi ya Jamii, taarifa za michango ya wanachama, uhakiki kwa njia ya biometric pamoja na elimu jinsi ya kujiunga na PSSSF Kiganjani". Maonesho haya ya teknolojia ya madini, yameanza tarehe 26 /09/2022 ns yatadumu kwa siku 13 hadi tarehe 08 Oktoba,2022. PSSSF ina ofisi ya Kanda hapa Geita, Kanda ya Ziwa Magharibi Geita, Ofisi ya Geita ambayo ipo katika Soko la Madini ghorofa ya kwanza inasimamia mikoa ya Geita, Kagera, Shinyanga na Kigoma.  

KUTOKA MAGAZETINI LEO IJUMAA SEPTEMBA 30, 20

Image
 

RAIS SAMIA AHUTUBIA KWENYE UZINDUZI WA CHAMA CHA MAWAKILI WA SERIKALI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Mawakili wa Serikali kabla ya kuzindua Chama cha Mawakili wa Serikali, nembo na Mfumo rasmi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 29 Septemba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kwenye laptop kuzindua mfumo rasmi wa Kieletroniki wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (OAGMIS), nembo  ya Ofisi hiyo pamoja na Chama cha Mawakili wa Serikali katika Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 29 Septemba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitembelea mabanda mbalimbali likiwemo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kujionea shughuli mbalimbali pamoja na huduma zitolewazo na Ofisi hizo kabla ya kuhutubia na kuzindua Rasmi Chama cha Mawakili

MFUKO WA MAENDELEO WA ABU DHABI KUENDELEA KUFADHILI MIRADI YA MAENDELEO TANZANIA

Image
NA BENNY MWAIPAJA, ABU DHABI Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), umeahidi kutoa mkopo nafuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania ukiwemo mradi wa umeme wa Benaco-Kyaka, mkoani Kagera na ujenzi wa makazi ya watumishi ya gharama nafuu Visiwani Zanzibar, inayokadiriwa kugharimu dola za Marekani milioni 420. Ahadi hiyo imetolewa Mjini Abu Dhabi na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi (Abu Dhabi Fund for Development), Mhe. Mohammed Saif Al Suwaidi, wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Makao Makuu ya Mfuko huo, mjini Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu. Mhe. Mohammed Saif Al Suwaidi alimweleza Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa miradi mingine ya kimkakati iliyowasilishwa na Serikali ya Tanzania kwenye Mfuko huo ukiwemo wa Ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere na Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) itatafutiwa ufadili kupi

PROF. MAKUBI AELEKEZA KUIMARISHA UCHUNGUZI WA UGONJWA WA EBOLA MIPAKANI.

Image
Na WAF- KAGERA. Katibu mkuu Wizara Prof. Abel Makubi ameelekeza Wataalamu wa afya katika mipaka kuimarisha huduma za uchunguzi wa magonjwa ikiwemo ugonjwa wa Ebola ili kuweza kuutambua na kuuzuia endapo utaingia nchini. Prof. Makubi ametoa rai hiyo, mapema leo wakati akitembelea  Mpaka wa Tanzania na Uganda -MTUKULA na kukagua zoezi la uchunguzi wa abiria wanaoingia nchini Tanzania. Katika ziara hiyo aliyoambatana na Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Prof.  Makubi ameshuhudia upimaji wa kutumia Thermoscans ikiwa ni moja ya njia ya kutambua hali ya maambukizi endapo mgonjwa atatokea. Hata hivyo, Prof. Makubi ameelekeza kutumika kwa dodoso la kutambua dalili za ugonjwa wa Ebola kama njia nyingine ya kutambua hali ya maambukizi endapo mgonjwa atatokea. Kwa upande mwingine, Prof. Makubi amekutana na wakazi wa mpakani katika eneo la Mtukura, huku akielekeza Wataalamu wa Afya kutoa elimu kwa wakazi hao juu ya namna bora ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Ebola ili usiingie nchini. Aidha, Prof. Makubi