PROF. MAKUBI AELEKEZA KUIMARISHA UCHUNGUZI WA UGONJWA WA EBOLA MIPAKANI.

Na WAF- KAGERA.

Katibu mkuu Wizara Prof. Abel Makubi ameelekeza Wataalamu wa afya katika mipaka kuimarisha huduma za uchunguzi wa magonjwa ikiwemo ugonjwa wa Ebola ili kuweza kuutambua na kuuzuia endapo utaingia nchini.
Prof. Makubi ametoa rai hiyo, mapema leo wakati akitembelea  Mpaka wa Tanzania na Uganda -MTUKULA na kukagua zoezi la uchunguzi wa abiria wanaoingia nchini Tanzania.
Katika ziara hiyo aliyoambatana na Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Prof.  Makubi ameshuhudia upimaji wa kutumia Thermoscans ikiwa ni moja ya njia ya kutambua hali ya maambukizi endapo mgonjwa atatokea.
Hata hivyo, Prof. Makubi ameelekeza kutumika kwa dodoso la kutambua dalili za ugonjwa wa Ebola kama njia nyingine ya kutambua hali ya maambukizi endapo mgonjwa atatokea.
Kwa upande mwingine, Prof. Makubi amekutana na wakazi wa mpakani katika eneo la Mtukura, huku akielekeza Wataalamu wa Afya kutoa elimu kwa wakazi hao juu ya namna bora ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Ebola ili usiingie nchini.
Aidha, Prof. Makubi ameendelea kuhimiza kuwekwa kwa mifumo ya kunawa mikono katika mitaa, maeneo ya vituo vya abiria, daladala, sehemu za ibada, ofisi na majumbani ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kupambana dhidi ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola. 





Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"