NA. MWANDISHI WETU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amekea vitendo vya baadhi ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI nchini kukwepa na kusitisha matumizi ya dawa za kupunguza makali ya ugongwa huo huku wakipatwa na madhara zaidi. Ametoa kauli hiyo alipotembelea na kukagua shughuli za watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI kutoka katika Konga Jiji Mbeya, kukagua ujenzi wa Kituo cha Tiba na Matunzo (CTC) Chimala pamoja na ujenzi wa Kituo cha Tiba na Matunzo cha Zahanati ya Igawa Mbarali oktoba 27, 2021 Jijini Mbeya. Waziri alieleza kuwa, kumekuwa na kesi za watu kutoroka na kusitisha matumizi ya dawa hizo huku akieleza kuwa ni changamoto inayokwamisha mapambana dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI. “Wanaoishi na VVU wote acheni kutoroka dawa bali endeleeni kutumia dawa hizo ili kuendelea kufubaza makali na kuwa afya njema,”alisema waziri Mhagama Alisema ni wakati sasa jamii kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu umuhimu wa