TAASISI YA NEPHROPLUS KUSAIDIA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA KUSAFISHA DAMU KWA BEI NAFUU.
HYDERABAD, INDIA Waziri wa afya Mhe. Ummy Mwalimu ameueleza uongozi wa Taasisi Nephroplus kuwekeza nchini ili kusaidia kupunguza gharama za kusafisha damu. Waziri Ummy amesema hayo wakati akihitimisha ziara yake nchini India kwa kutembelea taasisi ya Nephroplus. Waziri Ummy amesema Tanzania ina uhitaji mkubwa wa huduma za kuchuja damu ndio sababu ya Serikali imeamua kutafuta wadau wa kushirikiana nao kuwezesha kupunguza gharama ili kuwafikia watanzania wengi wenye uhitaji hasa kwa watu wasio na bima ya Afya. "Serikali iko tayari kuingia makubaliano ya ushirikiano na Taasisi hii kwa kuwa mapendekezo ya gharama zao ni za chini na hivyo kila mwananchi mwenye uhitaji ataweza kumudu gharama za huduma hiyo muhimu". Amesema Waziri Ummy. Ameongeza kuwa Uwekezaji huu utasaidia kuboresha upatikanaji wa huduma za uchujaji wa damu kwa wagonjwa wa figo kwa gharama nafuu nchini. Taasisi ya Nephroplus iliyopo mjini Hyderabad nchini India inayojishughulisha na utoaji wa huduma za kuchuja d