TAASISI YA NEPHROPLUS KUSAIDIA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA KUSAFISHA DAMU KWA BEI NAFUU.

HYDERABAD, INDIA

Waziri wa afya Mhe. Ummy Mwalimu ameueleza uongozi wa Taasisi Nephroplus kuwekeza nchini ili kusaidia kupunguza gharama za kusafisha damu.

Waziri Ummy amesema hayo wakati akihitimisha ziara yake nchini India kwa kutembelea taasisi ya Nephroplus.

Waziri Ummy amesema Tanzania ina uhitaji mkubwa wa huduma za kuchuja damu ndio sababu ya Serikali imeamua kutafuta wadau wa kushirikiana nao kuwezesha kupunguza gharama ili kuwafikia watanzania wengi wenye uhitaji hasa kwa watu wasio na bima ya Afya.

"Serikali iko tayari kuingia makubaliano ya ushirikiano na Taasisi hii kwa kuwa mapendekezo ya gharama zao ni za chini na hivyo kila mwananchi mwenye uhitaji ataweza kumudu gharama za huduma hiyo muhimu". Amesema Waziri Ummy.

Ameongeza kuwa Uwekezaji huu utasaidia kuboresha upatikanaji wa  huduma za uchujaji wa damu kwa wagonjwa wa figo kwa  gharama nafuu nchini.

Taasisi ya Nephroplus iliyopo mjini Hyderabad nchini India inayojishughulisha na utoaji wa huduma za kuchuja damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo imedhamiria kuwekeza katika huduma za upatikanaji wa huduma za kuchuja damu nchini. 

Taasisi hiyo ina jumla ya vituo vya kusafisha damu takriban 325 katika miji 20 nchini India na nje ya India. Aidha, taasisi hiyo ina jumla ya mashine za kusafishia damu zipatazo 4500. 

Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Bwana Vikram  Vupalla ameeleza kuwa wamekuwa na mafanikio makubwa kwenye nchi wanazotoa huduma  za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo. 

Pia, ameeleza nia yake ya kuja kuwekeza na kutoa huduma za kusafisha damu nchini kwa gharama nafuu.

Vupall amesema kuwa ili aweze kuwekeza nchini anahitaji ushirikiano wa Wizara ya Afya na Serikali ya Tanzania katika kufanikisha uwekezaji huo.





Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"