Wednesday, March 31, 2021
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AMTEUA BALOZI HUSSEIN A. KATTANGA KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi wa
Tanzania nchini Japan, Mhe. Hussein A. Kattanga kuwa Katibu Mkuu Kiongozi
kuchukua nafasi ya aliyekuwa akishika wadhifa huo Balozi Dkt. Bashiru Ali
Kakurwa ambaye ameteuliwa kuwa Mbunge.
Rais
amefanya mabadiliko hayo wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Makamu wa Rais Mhe.
Dkt. Philip Mpango Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma Machi 31, 2021.
Rais
pia amefanya mabadiliko kwenye baraza la Mawaziri ambapo Mhe. Mwigulu Nchemba
ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango akitokea wizara ya Sheria na Katiba.
Rais
amemuhamisha Mhe. Ummy Mwalimu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na kumpeleka
Ofisi ya Rais-TAMISEMI, huku aliyekuwa Waziri kwenye ofisi hiyo Mhe., Selemani
Jafo amehamishiwa Ofisi ya Makamu wa Rais.
Waziri
wa Mambo ya Nje, Profesa Palamagamba Kabudi amehamishiwa Wizara ya Sheria na
Katiba ambapo Waziri wa Mambo ya Nje sasa atakuwa Balozi Liberata Mulamula
ambaye awali aliteuliwa na Rais kuwa Mbunge.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kushuhudia Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akiapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akiapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akitia saini Hati ya Kiapo mara baada ya kuapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.DKT. PHILIP MPANGO AAPISHWA KUWA MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA
DKT. Philip Isdor Mpando ameapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Alasiri Machi 31, 2021.
Mhe, Mpango ameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Pia katika hafla hiyo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar MheHemed Suleiman na Spika wa Bunge Mher. Job Ndugai sambamba na viongozi wa juu wa serikali.