Posts

Showing posts from March, 2024

MAKAMU WA RAIS DKT MPANGO AUNGANA NA WAUMINI WENGINE WA KIKRISTO KWENYE IBADA YA SIKUKUU YA PASAKA

Image
DODOMA  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango leo tarehe 31 Machi 2024 wameungana na waumini mbalimbali kushiriki Ibada ya Sikukuu ya Pasaka katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Damu  Azizi ya Yesu – Kisasa Mkoani Dodoma. Akitoa salamu za Sikukuu ya Pasaka mara baada ya kushiriki Ibada hiyo, Makamu wa Rais ametoa wito kwa watanzania kutumia sikukuu ya Pasaka kutambua hakuna ushindi bila kujitoa muhanga kwaajili ya wengine, familia, wahitaji na Taifa kwa ujumla. Amesema ni lazima kujitoa muhanga kwa kutimiza wajibu vizuri kwa kufanya kazi kwa bidii kwaajili ya maendeleo ya nchi ya sasa na vizazi vijavyo. Makamu wa Rais amesema ni muhimu kutumia sikukuu ya Pasaka kujifunza kushinda ubinafsi na kuhakikisha haki na huduma zinatolewa bila kuomba rushwa. Makamu wa Rais ametoa wito kwa viongozi na watumishi wa serikali kuwa kielelezo cha kujitoa muhanga kwaajili ya kuwatumikia watu wengine. Amese

KUTOKA MAGAZETINI LEO MACHI 31, 2024

Image
 

KUTOKA MAGAZETINI LEO MACHI 30, 2024

Image
 

NCHIMBI MSIBANI KWA ASKOFU GACHUMA

Image
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, amewasili wilayani Tarime, Mkoa wa Mara, kushiriki mazishi ya Askofu wa Kanisa la New Life Gospel Community Church (NLGCC), Jimbo la Mara Kaskazini, Bi. Francisca Mwita Gachuma, ambaye ni mwenza wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa, Ndugu Christopher Mwita Gachuma. Baada ya kuwasili msibani nyumbani kwa marehemu Mtaa wa Bomani, Tarime Mjini, leo Ijumaa, Machi 29, 2024, na kupokelewa na Viongozi wa Chama na Serikali, Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk. Nchimbi alipata fursa ya kuweka saini kitabu cha maombolezo na kuwapatia pole wafiwa, wakiongozwa na Familia ya Mzee Gachuma, pamoja na kushiriki ratiba ya awali ya msiba, kabla ya mazishi yatakayofanyika Machi 30, 2024, huko Komaswa, Tarime.

DIB YATANGAZA NEEMA KWA WALIOKUWA WATEJA WA BENKI YA WANANCHI MERU (MERU COMMUNITY BANK)

Image
ARUMERU  BODI ya Bima ya Amana imetangaza kwamba wale wote waliokuwa wateja katika Benki ya Wananchi Meru (Meru Community Bank) ambao hawajachukua amana zao zilizokuwa chini ya Shilingi 1,500,000 wafike katika tawi la Benki ya Biashara  Tanzania (TCB) tawi la Meru au Tawi la Benki Kuu Arusha kwa ajili ya kurudishiwa amana zao. Hayo yalisemwa na Meneja Uendeshaji wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB), Nkanwa Magina wakati wa mfululizo wa mafunzo kuhusiana na uwepo wa DIB, Majukumu ya DIB na mfumo wa DIB, mafunzo yakielekezwa kwa makundi mbalimbali wilayani Meru hususani kwa viongozi wa Vijiji, na wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za serikali, Pia makundi mengine ni pamoja na wafanyabiashara kwenye minada na masoko mbalimbali ya wazi ambayo yapo katika vitongozji vya King’ori, Kikatiti, Maji ya Chai, Usa River na Leganga. Aidha mafunzo hayo yaliendeshwa kwa takriban wiki nzima na kufikia tamati leo. Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Arumeru Dkt. Amani Sanga, aliishu