Posts

Showing posts from January, 2023

RAIS SAMIA AZINDUA TUME YA KUANGALIA JINSI YA KUIMARISHA TAASISI ZA HAKI JINAI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai nchini Mhe. Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othman pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Sefue mara baada ya kuzindua Tume hiyo Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 31 Januari, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma kabla ya kuzindua Tume ya kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai tarehe 31 Januari, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mwenyekiti wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai nchini Mhe. Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othman, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Sefue pamoja na Katibu wa  Sekretarieti ya Tume hiyo Bw. Kailima Ramadhani, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 31 Januari, 2023. Ra

SERIKALI YACHUKUA HATUA KUKABILIANA NA MFUMUKO WA BEI

Image
  Na Haika Mamuya, WFM , Dodoma. BUNGENI Waziri wa Fedha na Mipa n go ,  Mh. Dk t.  Mwigulu Lameck Nchemba ,  amesema  S erikali haijajificha kwenye vita ya Ukraine na  U rusi ,  uviko  na  mabadiliko ya tabianchi   katika suala la mfumuko wa bei  nchini kwa kuwa  mambo  hayo ni  halisia na  S erikali  imeendelea kuchukua hatua. Dkt. Nchemba amebainisha hayo Bungeni jijini Dodoma, wakati akitoa taarifa kwa Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Mrisho Gambo, aliyesema kuwa Serikali inajificha katika vita ya Ukraine na Urusi katika suala la mfumuko wa bei. Dk t. Nchemba alisema kuwa Serikali  imechukua hatua ambazo  nchi nyingi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika  hazijazifikia  “K wa ujumla  hamna nchi imechukua  hatua ya  kutoa bilioni 100 kila mwezi kwa ajili ya kupunguza gharama ,  nd i o maana hata nchi  j irani zinakimbilia Tanzania kuchukua vitu ”, alisema Dkt. Nchemba . Alisema kuwa  Serikali i me ondoa tozo na kodi zote katika mafuta ya kula na ikachukua nusu  ya gharama  ya bei  ya

SERIKALI IMEANZA KUFANYIA KAZI MABORESHO YA MISHAHARA VYUO VIKUU - MHE. KATAMBI

Image
BUNGENI, DODOMA SERIKALI imeanza kufanyia kazi suala la maboresho ya mishahara kwenye vyuo vikuu kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi, ameyasema hayo leo bungeni alipokuwa akijibu maswali ya nyongeza Mbunge wa Viti maalum, Dkt.Thea Ntara ambaye ameuliza mchakato wa mkataba namba 189 umefikia wapi ili kuboresha mishahara ya wafanyakazi wa majumbani na pia amehoji kuboresha mishahara kwa wakuu wa vyuo vikuu. Akijibu maswali hayo, Mhe.Katambi amesema suala hilo la maboresho la mishahara linaangalia viwango kulingana na hali ya kiuchumi na uhalisia wa kidunia wa sasa. Aidha, amesema Serikali ilishaanza kuufanyia kazi mkataba wa kimataifa namba 189 ikiwa ni maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Amesema mkataba huo kuna vipengele bado vinaendelea kufanyiwa kazi ambavyo vipo vinavyoendana na hali ya uchumi na uhalisia wa kimazingira na kitamaduni. “Seri

USAJILI WA HATI ZA ARDHI: PUNGUZENI URASIMU

Image
NA Anthony Ishengoma. Dodoma Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi amewataka Wasajili Wasaidizi wa hati kote nchini kuzingatia maadili ya kazi zao lakini pia kuhakikisha wanafikia viwango au vigezo walivyojiwekea kama ilivyo katika mkataba wa utoaji huduma kwa wateja wa Wizara ya Ardhi. Dkt. Kijazi pia amewataka watendaji hao kupunguza urasimu na mlolongo wa taratibu ambazo hazina tija katiza zoezi zima la utoaji hati kwani baada ya tathimini ya robo mbili za mwaka wa fedha Wizara yake imebaini kasi ya utoaji hati bado iko chini sana. Katibu Mkuu Kijazi alisema hayo jana wakati akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kufungua kikao kazi cha siku mbili kinachoendelea Jijini Dododoma kwa wasajili hao kujipanga upya na kuangalia namna bora ya kuboresha sekta yao ikiwemo uboreshaji wa makusanyo wa mapato ya serikali. Dkt. Kijazi aliongeza kuwa kuna baadhi ya sababu ambazo pia zinatokana na watendaji wenyewe na hivyo kuwataka wabainishe sababu zinaz

TAMKO LA KAMATI YA SERA YA FEDHA

Image
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Emmanuel Tutuba. (Picha ya Maktaba).  

SERIKALI YATOA MIKOPO YA SH. BILIONI 165 KWA WAKULIMA

Image
Na Farida Ramadhani, WFM, Dodoma Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa mkopo wa shillingi billioni 164.9 kwa Sekta ya Benki na Taasisi za Fedha nchini uliowanufausha wakulima wadogo 5,385 na Vyama vya Ushirika na Masoko (AMCOS) 21. Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Halima Mdee aliyetaka kujua makundi yaliyonufaika na mkopo wa shilingi trilioni moja iliyoahidiwa kutolewa na Serikali katika sekta ya kilimo pamoja na masharti yake. Mhe. Nchemba alisema utoaji wa mkopo huo ambao takwimu zake zinaishia tarehe 31 Disemba 2022, ulikuwa ni utekelezaji wa hatua za ziada za kisera zilizochukuliwa na Serikali ikiwemo kuanzisha mkopo maalum wa shilingi trilioni moja kwa benki na taasisi za fedha nchini ili kuchochea mikopo nafuu kwa Sekta Binafsi hususan Sekta ya Kilimo. Alisema Masharti ya mkopo huo maalum yalikuwa kuchochea mnyororo wa thamani katika kilimo cha

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMANNE JANUARI 31, 2023

Image