WAZIRI MHAGAMA AIPONGEZA WCF KWA KUIPATIA VITENDEA KAZI (COMPUTERS) TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI CMA
NA KHALFAN SAID, K-VIS BLOG, MBEYA WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama ameupongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa kuipatia vitendea kazi (computers) Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ili kuharakisha shughuli za usuluhishi wa migogoro ya kikazi. Pongezi hizo zimetolewa na Mhe. Waziri wakati akikabidhi computer 10 kwa Mkurugenzi Mkuu wa CMA, Bw.Shanes Nungu katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) jijini Mbeya Novemba 29, 2021. “Tunashuhudia hapa Workers Compensation Fund (Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi) unafanya kazi nzuri ya kuiwezesha CMA ili itekeleze majukumu yake sawasawa jambo hili lina tija katika utendaji.” Alifafanua Mhe. Waziri. Kipekee napenda kuwashukuru sana sana wakuu wote na viongozi wa taasisi zote Dkt. John Mduma Mkurugenzi Mkuu wa WCF na ndugu Shanes Nungu Mkurugenzi Mkuu wa CMA kwa kuona umuhimu wa kufanya kazi kama serik