WAZIRI MAKAMBA AIHAKIKISHIA SHELL UTAYARI WA SERIKALI KUTEKELEZA MRADI WA LNG.
Na Dorina G. Makaya - Dar-es-salaam.
Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba tarehe 26 Novemba 2021, amekutana
na Ujumbe kutoka Kampuni ya SHELL ulioongozwa na
Makamu wa Rais Mtendaji anaesimamia mradi wa kusindika gesi (LNG ) kwa
upande wa Mashariki ( Africa, Asia na Australia) Bwana Cederic Cremers ambae
amedhuru Tanzania kwa Mara ya Kwanza tangu kuchukua wadhifa huo mapema mwezi
August 2021.
Katika ujumbe huo, bwana Cremers aliongozana na Makamu wa Rais na mkazi wa
Shell Tanzania, bwana Jared Kuehl pamoja na mdau mwenzao bi Unni Fjaer kutoka
kampuni ya Equinor.
Lengo la kikao hicho ni utambulisho wa Makamu wa Rais Mtendaji wa SHELL pamoja
na kumhakikishia Waziri wa Nishati kuwa, Shell pamoja na Washirika wake
wamejizatiti katika kuhakikisha mradi wa LNG unatekelezwa katika ufanisi, uwazi
unaotakiwa na kwa wakati uliokusudiwa.
Waziri wa Nishati, ameuambia ujumbe kutoka Kampuni ya Shell kuwa, Serikali ya
Tanzania ipo tayari kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati kwa manufaa ya
pande zote mbili.
Waziri Makamba amebainisha kuwa, Serikali inautazama mradi wa LNG kwa mapana
zaidi na kuwa, mradi wa kusindika gesi asilia ni mradi unaotarajiwa kuleta
mabadiliko makubwa kiuchumi na kifedha pamoja na kuwajengea uwezo wazawa.
Aidha amesisitiza kuwa, pande zote mbili zihakikishe zinafanya haraka kuutekeleza mradi huu kwa wakati uliopangwa.
Pia Waziri Makamba amesema kuwa, yupo tayari kufanya kazi zaidi ili kuhakikisha
dhima ya Serikali ya kukamilika kwa mradi huu inatekelezwa.
Waziri wa Nishati
Mhe. January Makamba (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Shell, Cedric Cremers anayeshughulika na
Masuala ya LNG Mashariki ya Mbali (wa pili kutoka kushoto) alipofika. katika
ofisi ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar-es-Salaam tarehe 26 Novemba, 2021
kwa lengo la kujitambulisha kwa Waziri wa Nishati.
Wa kwanza kushoto ni Makamu wa Rais na Mwenyekiti Mkazi, Shell Tanzania Jared
Keuhl na wa kwanza kulia ni Makamu wa Raisi na Mwenyekiti Mkazi, Equinor AS
Unni Merethe Skorstad Fjær.
Waziri wa Nishati
Mhe. January Makamba akiwa na ujumbe kutoka Kampuni ya Shell na Washirika wake
walipofika katika ofisi ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar-es-Salaam tarehe
26 Novemba, 2021 kumtambulisha kwa Waziri wa Nishati, Makamu wa Rais wa
Kampuni ya Shell, Cedric Cremers anayeshughulika na Masuala ya LNG Mashariki ya
Mbali.
Comments
Post a Comment