7/31/2021

MBUNGE NEEMA LUGANGIRA ATOA NENO FEDHA ZINAZOKUJA NCHINI KWA AJILI YA NGOs


MBUNGE wa Viti Maalumu CCM (NGOs Tanzania Bara) Neema Lugangira akizungumza  wakati wa  Uzinduzi wa Wiki ya Azaki imefanyika Jijini Dar es Salaam Julai 29 Julai 2021
MBUNGE wa Viti Maalumu CCM (NGOs Tanzania Bara) Neema Lugangira amesema umesema wakati kuhakikisha fedha za ufadhili ambazo zinatoka nje ya nchi zinazokuja nchini ziweze kufanyiwa kazi na kutelezwa na NGOs na CSOs kutoka ndani ya nchi,
Aliyasema hayo Siku ya Uzinduzi wa Wiki ya Azaki imefanyika Jijini Dar es Salaam Julai 29 Julai 2021 ambapo alisema takwimu zinaonyesha kwamba zile fedha ambazo zinazoingia kwa ajili ya Sekta ya Azaki ni asilimia 1 pekee yake ndio zinaekwenda kwa CSOs, NGOs ambazo zimeanzishwa na Watanzania.
Mbunge Lugangira alisema kwa sababu takwimu zinaonyesha asilimia 99 ya fedha zinazotoka nje zinapita kupitia mashirika ambazo sio ya kiserikali lakini ni ya Kimataifa huku akieleza ili miradi yetu iwe endelevu lazima NGOs/CSOs za ndani ziweze kushiriki katika utekelezaji wa miradi hiyo na ndio maana mara nyingi wanaona kuna miradi fulani ukishaasha ufadhili na mfadhili akishaondoka mradi unakuwa hauendelei.
Alisema pia mara nyingi Sekta ya Azaki wanahesabiwa kama sehemu ya Sekta Binafsi lakini Sekta Binafsi ni tofauti zaidi kwa sababu wale ni wafanyabiashara zaidi na wanapokwenda kuongea mwakilisha Sekta Binafasi hawezi kuwakilisha Sekta ya Azaki.
“Nimejaribu kutoa changamoto kama wadau mnatambulika kama sekta inayosimama inachangia kwenye maendeleo ili kufanya hivyo lazima waonyeshe mchango wao dhahiri ni upi ili waweze kutambulika”Alisema

Hivyo alisema ni matarajio yake itapoandaliwa wiki ya Azaki mwezi Octoba mwaka huu basi watapata majawabu kwenye eneo hilo na watafanya mikakati madhubiti ya kutoka asilimia 1 na iongezeka.
    

MHANDISI MASAUNI ARIDHISHWA NA UTENDAJI WA SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA

Msaada wenu tafadhali
Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, amelipongeza Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa kuongeza ufani na kuboresha utendaji kazi wa Shirika hilo na kufanikiwa kuongeza kiwango cha uwekezaji kutoka sh. bilioni 85 mwaka 2018/2019 hadi kufikia shilingi bilioni 245 Mwaka 2020/2021.

Mhandisi Masauni ametoa pongezi hizo alipotembelea Makao Makuu ya Shirika la Bima la Taifa Jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Shirika hilo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea Taasisi zote zilizochini ya Wizara ya Fedha na Mipango, baada ya kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo.

“Moja ya eneo lililonivutia ni namna Shirika hili lilivyoboresha huduma zake na  mapato kwa kutumia mifumo ya TEHAMA, kutoka asilimia 10 za miaka ya nyuma hadi kufikia asilimia 95 katika kipindi cha miaka miwili tu iliyopita” Alisema Mhe. Masauni

Ameuagiza uongozi wa Shirika hilo kuongeza ubunifu na bidii zaidi na kuhakikisha kuwa linakuwa Shirika bora zaidi la Bima hapa nchini, Ukanda wa Afrika Mashariki na nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Aidha, alitoa wito kwa wananchi kutumia huduma za Bima zinazotolewa na Shirka hilo la Umma na kuahidi kuwa Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kuliunga mkono na kulisaidia liweze kutimiza malengo yake ya kuwahudumia wananchi kikamilifu.

Akitoa taarifa ya utendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Dkt. Elirehema Doriye alisema katika kipindi kifupi cha miaka miwili iliyopita ambacho NIC imefanya mageuzi na mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa Shirika, Shirika limewekeza kiasi hicho cha shilingi bilioni 245 sawa na ufanisi wa silimia 136.05.

“Katika kipindi hicho pia Shirika limelipa madai mbalimbali ya Bima ya Maisha yaliyohakikiwa kwa wateja wetu, kiasi cha shilingi bilioni 15.8 kati ya shilingi bilioni 22.53 ambazo shirika  linadaiwa, hatua iliyosababisha kurejea kwa imani ya wateja na kuvutia wateja wapya kujiunga na huduma zinazotolewa na Shirika, na tunatarajia kulipa madeni yote kabla ya mwaka 2021 kuisha” Alisema Dkt. Doriye

Dkt. Doriye alimweleza Mhe. Masauni kwamba Shirika lake pia linazidai Taasisi na Mashirika mbalimbali ya Umma ambazo hazijalipia Bima za Maisha za mali zao kiasi cha shilingi bilioni 34.42 na kwamba fedha hizo zikipatikana zitaongeza mtaji wa Shirika na uwezo wa kuwahudumia wateja wao.

Aidha, alisema kuwa NIC inaandaa bidhaa mpya ikiwemo kuanzisha Bima ya Mifugo na kubuni bidhaa nyingi zaidi za Kilimo ili kuchangia juhudi za Serikali za kuinua sekta za ufugaji, kilimo na viwanda.

Mwish.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye, baada ya kukabidhiwa zawadi, alipofanya ziara katika Shirika hilo, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), akiipongeza Menejimenti ya Shirika la Bima la Taifa (NIC), kwa jitihada za kuimarisha utendaji na kutoa huduma bora kwa wananchi, alipotembelea Shirika la NIC, jijini Dar es Salaam.  

Baadhi ya Viongozi wa Menejimenti ya Shirika la Bima la Taifa (NIC), wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), alipokuwa akiwasisitiza kuongeza jitihada katika kutoa huduma ili kukabiliana na ushindani wa huduma za bima alipotembelea Shirika hilo, jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye, wakiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Shirika hilo, alipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea taasisi zilizochini ya Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es Salaam.

(picha na Wizara ya Fedha na Mipango, Dar es Salaam)

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye akielezea bidhaa mpya ambazo Shirika lake limejipanga kuzitoa kwa wananchi ili kukidhi uhitaji wao, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) (hayupo pichani), katika Shirika hilo, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Uthamini na Udhibiti wa Majanga wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bi. Annette Magogo, akieleza namna mpya ya kiutendaji inayofanywa na Shirika hilo, ambayo imeongeza imani kwa wananchi wa kulitumia Shirika hilo katika huduma za Bima, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) (kushoto) katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam.

    

RAIS SAMIA APOKEA NDEGE MPYA AINA YA BOMBADIER DASH 8-Q400 ILIYONUNULIWA NA SERIKALI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria kupokea Ndege Mpya aina ya Bombadier DASH 8-Q400 iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania na kukodishwa kwa  Shirika la Ndege la ATCL ilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 30  Julai, 2021. Wa pili kushoto ni Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango na wa tatu kulia ni waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasalimia Wananchi waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kumuunga Mkono kwenye mapokezi ya Ndege Mpya aina ya Bombadier DASH 8-Q400 iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania na kukodishwa kwa  Shirika la Ndege la ATCL ilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 30  Julai, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kupokea Ndege Mpya aina ya Bombadier DASH 8-Q400 iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania na kukodishwa kwa  Shirika la Ndege la ATCL ilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 30  Julai, 2021. IKULU.
 

    

USIKIVU WA TBC WAPANDA KWA ASILIMIA 14 NDANI YA MIEZI MIWILI

 

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent Bashungwa(Mb), na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.Dkt. Faustine Ndungulile (Mb);wakikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Kituo cha kurushia matangazo ya Redio ya TBC eneo la Kisaki - Morogoro leo Julai, 2021.

Mtaalam wa Mitambo akitoa maelezo kwa  viongozi  mbalimbali waliohudhuria  kwenye ya uzinduzi wa Kituo cha kurushia matangazo ya Redio ya TBC eneo la Kisaki - Morogoro leo Julai, 2021.

Na John Mapepele, WHUSM
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe Innocent Bashungwa amesema hadi kufikia Mwezi Septemba, mwaka huu usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) utapanda kuzifikia Wilaya 120 sawa na 76% kutoka Wilaya 103 ambapo ni sawa na 64% za usikivu wa sasa ili kuhahakikisha wananchi wote wanapata habari kwa uhakika.
Mhe. Bashungwa ameyasema hayo leo Julai 30, 2021 kwenye uzinduzi wa kituo cha kurushia matangazo ya redio eneo la Kisaki mkoani Morogoro ambapo amesema katika Bajeti ya Maendeleo ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021, TBC inatekeleza miradi ya upanuzi wa usikivu katika Wilaya za Karagwe (Kagera), Same (Kilimanjaro), Sikonge (Tabora), Kahama (Shinyanga), Bunda (Mara), Nkasi (Rukwa) na Kasulu (Kigoma)ambapo amefafanua kuwa kukamilika kwa miradi hii kutawezesha usikivu wa TBC kufikia 76% ya nchi nzima.

“Nataka kuwahakikishia wananchi wote kuwa Serikali ya awamu ya Sita chini ya Uongozi shupavu wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakusudia kupanua usikivu wa redio za TBC nchi nzima” amesisitiza Mhe. Bashungwa
Ameyataja maeneo mengine ambayo miradi inaendelea kutekelezwa kwa ushirikiano wa TBC na UCSAF kuwa ni pamoja na wilaya za Ngara (Kagera), Kyela (Mbeya), Ruangwa (Lindi), Kilombero/Mlimba (Morogoro), Ludewa (Njombe), Tanganyika (Katavi), Makete (Njombe), Uvinza (Kigoma), Mbinga (Ruvuma) na Ngorongoro (Arusha).
Pia ametoa wito kwa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kupeleka miundombinu ya umeme kwa vituo vyote ambavyo vinatumia genereta mfano Karagwe ili kuendelea kupunguza gharama za uendeshaji wa miradi hii.
“Kabla ya mradi kuanza kutekelezwa TBC, TANESCO na UCSAF kaeni pamoja mjadiliane namna ya kutekeleza miradi hii kwa ufanisi ili kutatua shida zinazowakabili wananchi wetu kwa kukosa huduma ya Habari na Mawasiliano” amesisitiza Mhe. Bashungwa
Kwa upande mwingine ameiomba Wizara ya Ujenzi kupitia TANROADS na TAMISEMI kupitia TARURA waone namna ya kuwezesha kufikika eneo hilo la mradi wa Kisaki kwa urahisi zaidi.
“Ombi hili ni sambamba na maeneo mengine yenye mitambo ya kurusha matangazo ambayo miundombinu yake haiko vizuri mfano eneo la Mnyusi- Tanga, Imagi – Dodoma, Matogoro – Songea na Mlima kampuni – Katavi)”. Ameongeza Mhe. Bashungwa.
Amesema kuwa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (Ibara 125) inaelekeza Serikali kuhakikisha kuwa inawekeza katika uimarishaji wa miundombinu ya utangazaji kwa TBC.
Mhe. Bashungwa amefafanua kuwa kwa namna ya pekee ibara ya 125 (f) inalekeza kuwa Serikali itahakikisha kuwa “inaimarisha Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kwa kulijengea uwezo wa rasilimaliwatu, fedha na vifaa vya kisasa ili liweze kufikisha matangazo ya redio na televisheni nchini kote kwa ubora na usikivu mzuri....”.
Aidha amesema Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka mitano (2020/2021 - 2025/2026) umeainisha vipaumbele vyake katika uwekezaji wa miundombinu ya Utangazaji ya TBC, ikiwemo upanuzi wa usikivu wa redio, pamoja na miundombinu yake.
Ameisihi Menejimenti ya Shirika hilo kuendelea kuwa wabunifu katika kuhabarisha umma na kuwahakikishia kwamba Wizara yake itaendelea kuwapatia msaada wowote wanaohitaji ili kutimiza malengo yake. Amelitaka TBC kuhakikisha linaandaa maudhui yatakayokidhi matakwa ya jamii nzima ya watanzania katika kukuza uzalendo, kudumisha mila na desturi za Watanzania na kulinda tunu za Taifa.
Pia amelipongeza TBC kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuwahabarisha wananchi wa makundi yote, ambapo amesema anatambua jitihada zinazofanywa za kukamilisha uzinduzi wa chaneli mpya ya televisheni ya TBC2 itakuwa mahususi kwa ajili ya vipindi vya vijana, michezo na burudani ambayo ujenzi wa studio zake umekamilika Mikocheni, Dar es Salaam.
Amewashukuru wadau wote ambao wanafanikisha utekelezaji wa mradi wa usikivu wa TBC hapa nchini. Amewataja baadhi ya wadau hao kuwa ni pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya jamii,Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kuendelea kufadhili miradi hii ya Upanuzi wa Usikivu ambayo inatarajiwa kutatua changamoto za Usikivu hivyo kuwezesha wananchi kupata huduma ya habari na Mawasiliano kwa urahisi zaidi.
Amesema uzinduzi wa kituo hiki ni hatua muhimu katika kutekeleza malengo Serikali katika kufisha habari kwa wananchi wote, mahala popote kwa lengo la kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha kwa njia ya redio, televisheni na mitandao ya kijamii. TBC kikiwa ni chombo cha Utangazaji cha Umma, kimetekeleza jukumu hili kwa vitendo.
Matangazo ya Redio za TBC kupitia kituo hiki yanatarajiwa kuwafikia wananchi katika vijiji vya Mvuha, Dhutumi, Bwakila Chini, Dakawa, Mngazi, Milengwelengwe, Sesenga, Nyalutanga, Mdokonyole, Gomelo, Kisaki Station, Matambwe, Kolelo, Lukange, Mgata, Ngerengere, Singisa na kwingineko). Maeneo mengine yatakayonufaika na mradi huu ni katika Wilaya za jirani za Kilombero, Rufiji na Kilwa.
“Kuzinduliwa kwa matangazo ya Redio katika kituo hiki cha Kisaki, ni utekelezaji wa Ilani ya CCM (2021 – 2025), ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu kuzinduliwa kwake”.amesisitiza Mhe. Bashungwa.

    

SERIKALI ITAHAKIKISHA ZAO LA MKONGE LINAIMARIKA-RC MALIMA

 

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua ukarabati wa Mashine za kuchakata mkonge ambapo awali zilikua chakavu hali iliyokua ikisababisha kushuka kwa uzalishaji wa zao la Mkonge.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Balozi Alli Siwa akizungumza
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sisalana Elizaberth Kalambo akielezea jambo
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima
NA OSCAR ASSENGA, KOROGWE

SERIKALI Mkoani Tanga imesema itahakikisha zao la Mkonge linaimarika kutokana na ongezeko la mahitaji ya bidhaa zitokanazo na zao hilo duniani yanayolenga kuachana na matumizi ya bidhaa za Plastiki ambazo zina athari kwa Jamii. 

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima wakati wa ziara yake ya kukagua ukarabati wa Mashine za kuchakata mkonge ambapo awali zilikua chakavu hali iliyokua ikisababisha kushuka kwa uzalishaji wa zao la Mkonge. 

Mkuu huyo wa mkoa alisema kwa miaka mingi nguzo ya uchumi ya Mkoa huo ilikuwa zao la Katani na miaka 50 iliyopita Tanga ilikuwa inazalisha tani 150,000 lakini baada ya marekebisho na nguvu kubwa mkoa wa Tanga inazalisha tani 35000.

Alisema hivi sasa Serikali ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu imeweka mkakati wa makusudi wa kuzalisha zao la Mkonge Kitaifa kutoka Tani 35,000 hadi kufikia Tani 120,000.

Aidha alisema mkakati huo unasimamiwa na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa ambao wakuu wa mikoa na wadau wengine wote wamekuwa ni sehemu ya mpango huo mafanikio yake yapo hapa wilayani Korogwe.

Alisema ili kufikia Tani 100,000 za Mkonge wanaweza kufikia huko kwa kushirikiana na wawekezaji wakubwa wakiwemo Mohamed Interprises Limited, Amboni Platation,

Kwale, Palet.

Mkuu huyo wa mkoa aliekeza lakini bodi inajua na ina maelekezo ya Waziri Mkuu na Serikali juu ya mkakati huo maana yake wanataka kuwa na uzalishaji wa mkonge mkulima ashiriki kama mmiliki wa uzalishaji huo na sio kama manamba na namna ya kufanya hivyo ni kupitia kwa vyama vya ushirika Amcos kama serikali, Mrajis wa vyama wataanza kuwa na uwezo wa uongozi na rasimali ili iweze kuwa na uzalishaji mkubwa zaidi.

Alisema vyama vya Ushirika (AMCOS) wana ubia katika uzalishaji na Kampuni ya Sisalana ambayo inamilikiwa na Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF) hivyo Sisisala lazima ijengewe uwezo wa kupokea  zao linalotoka kwa Mkulima kutokana na kwamba hivi sasa Sisalana wanapokea Tani 6000 kwenye Amcos zote na wana uwezo wa kupokea tani 11000 

Aliseam hivyo yeye amefika na timu yake kuweza kutengeneza mkakati ili hizo tani 11000 ziwafikie Sisalana na zipate kuchakatwa na mkulima aweze kupata haki yake pamoja licha ya kwamba huko kuna changamoto za pande zote mbili za Amcos na Sisalana na nyengine ambazo lazima utatuzi wake upatikana kwa Serikali ikiwemo suala la miundombinu inayopitisha

Awali akizungumza Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Balozi Alli Siwa alisema sheria ya kuanzishwa kwa mfuko huo inawaruhusu kuingia kwenye uwekezaji ndio maana wameshiriki kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa kwenye Corona ambazo zinamilikiwa na Kampuni ya SISALANA ambayo ni kampuni tanzu ya NSSF.

Alisema kampuni hiyo imepewa dhamana ya kuendesha Corona tano kwa madhumuni ya kuweza kurejesha fedha za wanachama ambapo wanaendesha shughuli za biashara hiyo kwa kushirikiana na Amcos kazi yao kubwa ni kuchakata majani ya katani ili Amcos ziweze kuuza brashi ambayo inaitwa Singa na wao wanaweza kupata tozo kwa ajili ya kuchakata.

Alisema hilo limewapelekea kwenye biashara ya mkonge na kwao hiyo haitoshi kuchakata kutokana na kwamba itawachelewesha kurudisha fedha zao wanazotaka kuzipata na pili wanataka biashara hiyo iwe na maana katika kutunishia mfuko wa Pensheni ili waweze kuwa na uwezo mkubwa wa kulipa pensheni kila inapohitajika kwa wanachama wao.

Naye kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sisalana Elizaberth Kalambo alisema walianza kazi yao kwa kufanya ukarabati katika mitambo katika kiwanda cha Usambara na baada ya hapo watahamia Mwelya ili kuhakikisha mitambo inakuwa katika hali nzuri.

Alisema wakati wanafanya ukarabati na matengenezo kwenye mitambo hivyo wanaomba wakulima wa mkonge wanaosimamiwa na Amcos tano za Mwelya, Magoma, Hale, Ngombezi na Magunga wanaomba wakulima wawape ushirikiano ili waweze kufanya maboresho.

Alisema kwa sababu wanapofanya matengenezo makubwa wanasimamisha uzalishaji kwa muda wa usipoungua wiki mbili mpaka tatau hivyo wanasisitiza kwa wakulima waongeze kasi ya upelekaji wa majani kwa kupeleka awamu mbili ili kuepuka hasara watakazokutana nazo wakati wanaposimamisha uzalishaji kwa siku hizo.


    

7/30/2021

RC KUNENGE AWAONGOZA WANANCHI MKOA WA PWANI KUCHANJA CHANJO DHIDI YA UVIKO 19 MJINI KIBAHA

 MKUU wa mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge, amepata chanjo ya UVIKO 19 leo Julai, 30 2021. Akichanjwa chanjo hiyo katikà viwanja vya kituo cha Afya Mkoani, kilichoko Kibaha Mjini, Mhe. Kunenge amewaasa Wanachi wa Mkoa huo kuwa ugonjwa upo na kuwataka kuchukua tahadhari wakati wote, amewataka Kuvaa barako, kunawa mikono kwa maji tiririka na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.

Amemshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuonyesha njia kwa kupata chanjo. "nimechanja kwa hiari yangu mwenyewe mpaka sasa najisikia vizuri sijaona shida yeyote," alisema RC KUNENGE na kuongeza......Wananchi waje wachanje kwa hiari yao tunachotafuta ni salama tumepata chanjo kidogo tunaendelea kuratibu upatikanaji wa nyingi zaidi na tutaitoa bila usumbufu na bila malipo. "Chanjo hii kwa sasa itatolewa kwa makundi ya Kipaumbele kama vile watoa huduma ya afya, watu wenye umri kuanzia miaka 50 na kuendelea kama ambavyo muongozi wa Wizara ya Afya kuhusu Chanjo hiyo unavyosema.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge, akichanjwa Chanjo dhidi ya Uviko 19 leo Julai 30, 2021 ikiwa ni uzinduzi wa Chanjo hiyo kwa wananachi wa Mkoa huo.


    

RAIS SAMIA AKUTANA NA MJUMBE WA RAIS FELIX TSHESEKEDI WA DRC IKULU DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika mazungumzo na Mjumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Felix Antoine Tshisekedi, ambaye  ni Waziri wa Fedha wa Nchi hiyo Mhe. Nicolas Kazadi Kadino, mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 30 Julai, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkaribisha Mjumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Felix Antoine Tshisekedi, ambaye  ni Waziri wa Fedha wa Nchi hiyo Mhe. Nicolas Kazadi Kadino, mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 30  Julai, 2021.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Felix Antoine Tshisekedi ulioongozwa na Waziri wa Fedha wa Nchi hiyo Mhe. Nicolas Kazadi Kadino, ulipowasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 30  Julai, 2021. Picha na Ikulu

    

JK ACHUKUA "USUKANI" TAASISI YA MFUKO WA WASHIRIKA WAFADHILI WA ELIMU DUNIANI (GPE)

 

Viongozi,  Rais Uhuru Kenyata wa Kenya, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania  Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali  Zanzibar, Mhe. Simai Mohammed Said na Viongozi kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika  Mkutano Mkuu wa Mfuko wa Washirika Wafadhili wa Elimu Duniani ( GPE) uliofanyika London ,Uingereza

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Washirika Wafadhili wa Elimu Duniani -Global Partnetship in Education (GPE).


Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) Mwenyekiti wa Mfuko wa Washirika Wafadhili wa Elimu Duniani -Global Partnetship in Education (GPE), akiwa katika Picha ya pamoja na WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Tekanolojia, Profesa Joyce Ndalichako(kushoto) na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar, Mhe. Simai Mohammed Said, wakati wa mkutano huo.
Rais mstaafu wa Tanzania na Mwenyekiti anayefuata wa GPE, Dkt. Jakaya Kikwete, akizungumzia kwenye mkutano wa Kimataifa kuhusu masuala ya Elimu jijini London nchini Uingereza Julai 29, 2021. amemuahidi mtangulizi wake kuwa wataimarisha Taasisi ili kusaidia mabadiliko chanya katika mfumo wa Elimu duniani.
 

    

RAIS MSTAAFU KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA KIMATAIFA UNAOJADILI MASUALA YA ELIMU

 

Rais mstaafu wa serikali ya awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akihutubia mkutano wa Kimataifa kuhusu Elimu jijini London nchini Uingereza Julai 29, 2021. Rais mstaafu Kikwete ni Makamu Mwenyekiti Mteule wa Bodi ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE). Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka nchi za kiafrika akiwemo Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Rais Muhamaadu Buhari wa Nigeria, Rais Nana Akufo-Addo wa Ghana, Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, Rais wa Togo Faure Gnassingbe na mwenyeji Waziri Mkuu wa Uingereza, Borris Johnson.