PSSSF YAWAALIKA WANACHAMA NA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO KWENYE MAONESHO YA 5 YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA.

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ambao unashiriki katika Maonesho ya 5 ya teknolojia ya madini kwenye viwanja vya Bombambili mkoani Geita umewaalika Wanachama na wananchi wote wa Geita kutembelea banda lao ili kupata huduma zitolewazo na Mfuko huo.

Meneja wa PSSSF Mkoa wa Geita, Bw. Geofrey Kolongo amesema "miongoni mwa huduma zinazotolewa bandani hapa ni pamoja na elimu kuhusu Hifadhi ya Jamii, taarifa za michango ya wanachama, uhakiki kwa njia ya biometric pamoja na elimu jinsi ya kujiunga na PSSSF Kiganjani".

Maonesho haya ya teknolojia ya madini, yameanza tarehe 26 /09/2022 ns yatadumu kwa siku 13 hadi tarehe 08 Oktoba,2022.
PSSSF ina ofisi ya Kanda hapa Geita, Kanda ya Ziwa Magharibi Geita, Ofisi ya Geita ambayo ipo katika Soko la Madini ghorofa ya kwanza inasimamia mikoa ya Geita, Kagera, Shinyanga na Kigoma.





 


Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"