CHONGOLO ACHANGISHA FEDHA KUJENGA NYUMBA YA BALOZI, GAVU AZUNGUMZIA KADI MPYA CCM ITAKAVYOTUMIKA BENKI, BIMA

 Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo ameendesha harambee ya ujenzi wa nyumba ya balozi wa Shina namba saba Kijiji cha Ilambilole kilichopo jimboni Isimani mkoani Iringa.
Chongolo ameendesha harambee hiyo Mei 30, 2023 baada ya kuelezwa kuwa balozi huyo amepanga nyumba na hivyo kukosa eneo zuri la kuendeshea vikao vya chama vya kikatiba.
"Kazi ya Chama Cha Mapinduzi ni kutenda kwa vitendo badala ya kupiga porojo majukwaani na kuwadanganya wananchi, " amesema Chongolo na kuongeza watashindanisha mashina yote wa CCM nchini.
"Na shina ambalo litafanya vizuri kwa kuingiza wanachama wapya ,kueneza sera za Chama hawataachwa bila kufanyiwa kitu katika mashina yao."
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Chongolo ametoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendegu kuhakikisha Wakala wa Umeme Vijijini(REA)wanapeleka umeme kwenye vijiji vyote vya Iringa Vijijini.
Chongolo amesema kwamba kwa sasa umeme sio hanasa bali ni maendeleo, hivyo ni muhimu REA wakahakikisha vijiji vyote vinakuwa na umeme.
Wakati huo huo Katibu wa NEC Oganaizesheni ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Issa Haji Gavu ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kadi za uanachama za CCM zinazotarajiwa kutoka kuanzia Agosti mwaka huu.
Amesema kadi hiyo ni ya kisasa na itakuwa na uwezo wa kutumika sehemu zaidi ya moja."Kadi hiyo itaunganishwa kwenye mifumo mbalimbali ili kupata huduma serikalini na sekta Binafsi."
Gavu amesema kadi hiyo ya uanachama itaweza kusoma katika mfumo wa bima ya afya, benki na hata katika baadhi taasisi zingine kupata huduma iwapo tayari umejiandikisha katika katika maeneo hayo.
"CCM ni Chama kikubwa hivyo ni lazima ifanye mambo yake kisasa ili mwanachama asilazimike kubeba kadi nyingi. Kadi hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba huduma zaidi ya 11, hivyo kupunguza usumbufu wa wana CCM watakaokuwa na kadi.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akihutubia wakati wa kikao maalum cha shina namba 7 kwa Balozi Rose Nzelemera, Ilambolile Kata ya Kising’a jimbo la Isimani mkoani Iringa.

Kikao maalum cha shina namba 7 kikiendelea kwa Balozi Rose Nzelemera, Ilambolile Kata ya Kising’a jimbo la Isimani mkoani Iringa,ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Chongolo ameshiriki sambamba na kupokea taarifa ya shina hilo ikiwemo changamoto mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi.

Balozi Rose Nzelemera akimkaribisha Mgeni Rasmi Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo na ujumbe wake pamoja na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kushika kikao hicho maalum cha shina.


Katibu wa NEC Oganaizesheni ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Issa Haji (Gavu ) akizungumza mbele ya kikao hicho kuhusu  kadi za uanachama za CCM zinazotarajiwa kutoka kuanzia Agosti mwaka huu.


Mbunge wa Jimbo la Isimani Mhe.William Lukuvi akizungumza mambo mbalimbali kuhusu jimbo lake mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniele Chongolo wakati wa kikao maalum cha shina namba 7 kwa Balozi Rose Nzelemera, Ilambolile Kata ya Kising’a jimbo la Isimani mkoani Iringa.

Mbunge wa Jimbo la Isimani Mhe.William Lukuvi akiwa pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Shina namba Saba wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati kikao kikendelea
 
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Ndugu Salim Abri Asas akizungumza jambo na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema kabla ya kuanza kwa kikao cha  namba 7 kwa Balozi Rose Nzelemera, Ilambolile Kata ya Kising’a jimbo la Isimani mkoani Iringa.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"