WAZIRI UMMY ATEMBELEA DAR ES SALAAM KUANGALIA UTAYARI WA KUIKABILI EBOLA

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Ally Mwalimu ameridhishwa na kiwango cha maandalizi ya utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola endapo utaingia jijini Dar es Salaam.

Mhe. Ummy Ameyasema hayo Oktoba 30, 2022 alipotembelea jiji hilo endapo jiji la Dar es Salaam litapata wagonjwa.

Hata hivyo alisema bado kuna kazi ya kufanya katika maandalizi na utayari.

“Shirika la Afya Duniani WHO limeahidi kuleta nchini Tanzania wataalamu ambao waliwahi kutoa matibabu kwa wagonjwa wa Ebola ikiwamo huko Liberia na kusisitiza hadi sasa Tanzania haina mgonjwa wa Ebola” amesema Waziri Ummy.

Alisema "Ebola ni tishio jana Waziri wa Afya wa Uganda ameniambia wamepata wagonjwa wapya 5 inafanya idadi ya waliopata maambukizi hayo tangu mlipuko {Septemba, 2022) kufikia sasa ni jumla ya watu 126."

Mhe. Waziri Ummy alibainisha kuwa inatia wasiwasi  baada ya Ugonjwa wa Ebola kufika Jijini Kampala na Entebbe, kuna mwingiliano mkubwa wa shughuli za kiuchumi na kijamii kati Uganda na Tanzania KATIKA mini hiyo.

 "Kuibuka kwa Ebola Uganda kunaiweka Tanzania katika hatari ya kupata mlipuko huu ni lazima tuchukue hatua madhubuti za kujikinga." Alisisitiza.







Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"