RAIS SAMIA AMPONGEZA MWADHAMA PROTASE KARDINALI RUGAMBWA KWA KUSIMIKWA RASMI NA BABA MTAKATIFU FRACISKO

Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hasan, ametuma salamu za pongezi kufuatia kusimikwa rasmi na baba Mtakatifu Francisko kuwa Kardinali, Protase Kardinali Rugambwa (pichani) huko Vatican.

Rais ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii "Pongezi za dhati kwa Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, kwa kusimikwa rasmi na Baba Mtakatifu

Francisko kuwa Kardinali. Kauli mbiu ya utume wako ni "Enendeni ulimwenguni kote", ikiakisi mafundisho ya Yesu Kristo katika Injili ya Marko 16:15, juu ya utume unaojali watu wote, sehemu zote na wakati wote. Naungana na Watanzania wote kukuombea kheri, afya njema, na mafanikio katika utumishi wako.


 

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"